Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Saturday, February 14, 2015

Boko Haram lashambulia Chad

Wanajeshi wa Chad nchini Nigeria
Kundi la jihad lililoko Nigeria, Boko Haram, kwa mara ya kwanza limeshambulia Chad.
Wakuu nchini humo wanasema kuwa, wapiganaji wa Boko Haram walivuka ziwa Chad kwa maboti usiku na kushambulia kijiji cha Ngouboua, kilichoko kandokandoya ziwa hilo.
Liliwauwa watu, kuchoma moto vijiji vyao na kuiba mali.
Wapiganaji wa kundi la boko haram walishambulia taifa la Chad
Chifu wa eneo hilo ni miongoni mwa waliouawa.
Majeshi ya Chad yanasemekana kuwarudisha nyuma wapiganaji hao ambao wanadhibiti eneo kubwa la ziwa hilo upande wa Nigeria.
Majeshi ya Chad yamekuwa yakikabiliana na Boko Haram nchini Nigeria taifa hilo ni la nne kushambuliwa na wapiganaji hao wa kiislamu

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG