Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Friday, February 20, 2015

BREAKING NEWS: MFANYAKAZI WA GAZETI LA MWANANCHI APIGWA RISASI

MFANYAKAZI wa Kampuni ya Mwananchi Communications, Patrick Pella amevamiwa na majambazi wenye silaha na kupigawa risasi, kujeruhiwa na kisha kuporwa fedha zake mchana huu maeneo ya Tabata-Relini jijini Dar.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Pella anadaiwa kuporwa kiasi cha Sh. Mil 2 alizokuwa nazo akiwa ametoka kuzichukua kwenye mashine ya kutolea fedha (ATM) Tawi la NMB liliyopo jirani na Azam TV, Barabara ya Mandela.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala, Mary Nzuki.
Mtandao huu ulimtafuta Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala, Mary Nzuki kuelezea zaidi tukio hilo, lakini simu yake iliita bila kupokelewa.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG