Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Friday, February 20, 2015

HIZI NI BAADHI YA JUMBE ZA BAADHI YA WASANII WA BONGO MOVIES WAKIONYESHA KUGUSWA NA WIMBI LA MAUAJI YA NDUNGU ZETU WENYE ULEMAVU WA NGOZI

Hizi ni baadhi ya jumbe za baadhi ya Wasanii wa Bongo movies wakionyesha kuguswa na wimbi la mauaji ya ndungu zetu wenye ulemavu wa ngozi
Shamsa Ford:
“Yaani hata sijui nisemeje maana kila nikifikilia mwanadamu anayefanya ukatili huu wa kuwaua walemavu wa ngozi naumia sana.kikubwa naomba Mungu wote wanaohusika na huu unyama wakamatwe.. inshaallah Mwenyezi Mungu atasimamia kwa hili”.
Riyama Ally:
“Kiukweli siwezi kulala leo bila kusema haya nitakayosema.. hawa ni wenzetu na wanastahili tabasamu zaidi ya wanalolitoa wenyewe wanahitaji mapenzi yetu ya ziada.. lakini wapi binaadamu wenye uchu na tamaa za madaraka, pesa, biashara kukua haraka na mengi mengineyo wameupa kisogo utu na kuondoa japo kwa uchache tabasamu dogo walilonalo... tunakwenda wapi jamani kwa kukata viungo vya wenzetu... nani wa kumlaumu wa kwanza ni wewe mwenye tamaa ya madaraka..pesa.. whatever.. lakini pili mganga wako aliyekudanganya ukalete kiungo hicho ili ufanikiwe.. nyie wote na mungu anawaona adhabu dhidi yenu wala hajaisahau hajalala mungu...na anawaona inshallah.. poleni ndugu zetu mlioathirika kwa namna moja au nyingine kwa janga ili.. mungu ibariji africa mungu ibariki tz tupe roho za imani inshallah.. amen. Plz piga vita mauaji ya albono kwa pamoja tunaweza....”.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG