bado
ni tete kwa mwenyekiti wa vijana waliofuzu mafunzo ya Jeshi la Kujenga
Taifa (JKT) lakini wakakosa ajira, George Mgoba kufuatia kutekwa kwake
na kujeruhiwa vibaya hivi karibuni na watu ambao bado hawajajulikana.
Mwenyekiti
wa vijana waliofuzu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) lakini
wakakosa ajira, George Mgoba akiwa katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili .
Mgoba
ambaye mpaka juzi alikuwa bado amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa
Ilala, Amana jiijini Dar es Salaam baada ya kujeruhiwa, simulizi yake
inaonesha kichwani kumejaa msongo mkubwa wa mawazo kutokana na watu
waliomteka kumlazimisha kufanya mapenzi na mwanamke mmoja.
Kwa
mujibu wa Mgoba, mwanamke huyo alikuwa mweupe, ana umri wa kati na
wakati wanamlazimisha kufanya naye mapenzi yeye hakuonesha kukerwa,
inaonekana alikuwa anajua.
“Kilichonishinda
kufanya naye mapenzi yule mwanamke ni mwili kuishiwa nguvu na pia
sehemu zangu za siri zilikuwa zina maumivu makali sana. sijajua nia yao
ilikuwa nini kama ningefanikiwa,” alisema Mgoba.
Habari
kutoka chanzo kimoja ndani ya jeshi la polisi, mwanamke huyo alitakiwaa
kutumika maalum ili Mgoba aseme kila kitu kwa maswali ambayo angeulizwa
na waliomteka.
“Ile
ni njia ya kupata ukweli, huwa inatumika. Mtu anaweza kupewa mwanamke
afanye naye mapenzi kwa lengo la kumchunguza. Si unajua wanaume
wanapobanwa kwenye kona ya mahaba wanajiachia hata kwa mambo ya siri wao
wanasema tu,” kilisema chanzo hicho.
Kikaendelea:
“We unadhani Samson (kwenye Biblia), kama si yule mwanamke wake Delila
angesema siri ya nguzu zake?”Baadhi ya watu wameunganisha kitendo cha
kutekwa kwa Mgoba kilichotokea Ijumaa iliyopita, Mabibo Dar na kwenda
kutupwa mkoani Pwani ni harakati zake za kuwaongoza wenzake kuandamana
kwenda Ikulu, Dar kwa lengo la kuonana na Rais Kikwete kudai wapewe
ajira.
Juzi
saa mbili na nusu asubuhi, Uwazi lilifika Hospitali ya Amana baada ya
kuwepo kwa taarifa kwamba, Mgoba ataongea na waandishi wa habari. Hata
hivyo, mpaka Uwazi linaondoka saa tisa, Mgoba hakufanya hivyo huku
polisi wanaomlinda na wauguzi wanaomtibu wakidai hawana mamlaka ya
kumruhusu majeruhi huyo kuzungumza na vyombo vya habari.
No comments:
Post a Comment