Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Thursday, February 5, 2015

NATO kuongeza nguvu Mashariki mwa Ulaya

Wanajeshi wa NATO wakiwa kwenye Doria
Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg amesema kuwa Urusi inaendelea kukiuka Sheria za kimataifa wakati huu mapigano yakiendelea nchini Ukraine.
Kauli hiyo imetolewa wakati Mawaziri wa Ulinzi kutoka jumuia ya NATO walipokutana mjini Brussels kujadili namna ya kuliimarisha Jeshi hilo, hatua ambayo inaelezwa kuwa kubwa tangu baada ya Vita baridi.
Wakati huohuo,Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani,John Kerry anatarajiwa kufanya mazungumzo mjini Kiev wakati ambapo Marekani inafikiria uwezekano wa kupeleka Silaha kuisaidia Ukraine kupambana na Waasi wanaounga mkono Urusi.
Kikosi cha Wanajeshi 5000 kinatarajiwa kutangazwa, na maeneo watakayokuwa,Stoltenberg amesema mabadiliko haya yanatokana na Mazingira ya kiusalama yalivyo kutokana na kile alichokiita ushari wa Urusi.
Nato pia itaweka wazi mipango yake ya kuanzisha Matawi nchiniEstonia,Lithuania,Latvia,Poland,Romania na Bulgaria.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG