Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Friday, February 13, 2015

Nigeria:Rais akana kuchelewesha uchaguzi

rais Goodluck Johnathan wa Nigeria
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan amekana kwamba alishauriwa kuhusu kuahirishwa kwa uchaguzi wa urais nchini humo siku ya jumamosi.
Maafisa wa uchaguzi walichukua hatua hiyo kufuatia ushauri wa wasiwasi wa maafisa wa usalama kuhusu mashambulizi ya wapiganaji wa Boko Haram kazkazini mashariki alisema.
Kucheleweshwa kwa uchaguzi kwa kipindi cha wiki moja sio kitu kikubwa alisema katika rininga ya taifa hilo.
Upinzani unadai kwamba bwana Johnathan alilazimisha uchaguzi huo kucheleweshwa kwa kuwa alikuwa anaogopa kushindwa.
Uchaguzi huo umeahirishwa hadi 28 mwezi machi.
Wachanganuzi wanasema kuwa uchaguzi huo ndio ulio na ushindani mkali tangu uongozi wa kijeshi ulioisha mwaka 1999.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG