Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Tuesday, February 3, 2015

Rais wa Nigeria anusurika bomu

o
Rais Goodluck Johnathan wa Nigeria akihutubia uma katika kampeni za uchaguzi
Bomu limelipuka kazkazini mwa Nigeria nje ya uwanja mmoja wa soka ambapo rais Goodluck Johnathan alikuwa amehutubia mkutano wa kampeni za uchaguzi.
Walioshuhudia wanasema kuwa mlipuko huo ulitokea katika eneo moja la kuegesha magari dakika chache tu baada ya rais huyo kuondoka katika uwanja huo uliopo mji wa Gome.
Goodluck Johnathan
Bwana Johnathan anafanya kampeni za kutaka kuchaguliwa tena katika uchaguzi unaotarajiwa tarehe 14 mwezi Februari,lakini anakabiliwa na changamoto kubwa ya usalama kutoka kwa kundi la Boko Haram huku kundi hilo likiimarisha mashambulizi yake.
Siku ya jumapili watu watano waliuawa na bomu huko Gombe.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG