Kocha
mkuu wa timu ya Taifa ya Wanawake Tanzania (Twiga Stars), Rogasian
Kaijage ametangaza kikosi cha wachezaji thelathini (30) kitakachoingia
kambini siku ya jumapili kujiandaa na mchezo wa kufuzu Mataifa Afrika
dhidi ya Zambia mwezi Machi mwaka huu.
Kaijage
ametangaza program yake ya mazoezi itakayochukua takribani wiki nne (4)
ili kuhakikisha wachezaji wanakua tayari kwa ajili ya mchezo huo
utakaochezwa kati ya Machi 21, 22 mwaka huu, huku akipanga kucheza
mchezo mmoja wa kirafiki kabla ya kuelekea Lusaka Zambia kwenye mchezo
wa awali.
Twiga
Stars ambayo itakua kambini katika Hosteli za Shirikisho la Mpira wa
Miguu nchini TFF zilizopo Karume, imeingia moja kwa moja katika hatua ya
pili kucheza na Zambia kufuatia kuwa na matokeo mazuri katika msimamo
wa viwango vya soka la wanawake barani Afrika.
Wachezaji
walioitwa ni, Asha Rashid, Esther Chaburuma, Fatuma Bushiri, Fatuma
Hassan, Fatuma Mustapha, Fatuma Omari, Eto Mlenzi, Mwajuma Abdallah,
Sofia mwasikili, Zena Khamis, Mwanahamis Omar, Fatuma Khatibu, Fadhira
Hamad, Anastazia Anthony, Shelder Boniface.
Wengine
ni Thereza Yonna, Happines Hezron, Amina Ally, Donizia Daniel, Fatuma
Issa, Vumilia Maarifa, Maimuna Hamisi, Najiati Abbasi, Stumai Abdallah,
Ziada Ramadhani, Zuwena Aziz, Irene Joseph (Mfunzo – Zanzibar), Dawa
Haji Vuai (JKU – Zanzibar), Belina Julius na Amina Ramadhani.
No comments:
Post a Comment