Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Friday, February 27, 2015

Ujerumani yaridhia kuinusuru Ugiriki

Waandamanaji waliharibu Mali mjini Athens
Bunge la Ujerumani limeunga mkono kuongezwa kwa muda wa miezi minne zaidi kuisaidia Ugiriki kifedha.
Muda uliridhiwa kuongezwa na wakopeshaji wa kimataifa juma lililopita baada yaUgiriki kuwasilisha mipango ya kufanya mabadiliko ya kiuchumi ambayo yalitakiwa kuidhinishwa na Nchi wanachama wa Euro.
baadhi ya Wabunge wa Ujerumani wameshuku kuhusu mpango huo ambao unaelezwa kuwa utaweza kupita kirahisi.
Hatua hii inakuja baada ya Polisi na Waandamanaji kupambana wakati wa Maandamano mjini Athens siku ya Alhamisi.
Waandamanaji waliharibu Mali mjini Athens
Hizi ni vurumai za kwanza tangu Chama cha Mrengo wa kushoto cha Ugiriki Syriza kuongoza Serikali kuu ya Ugiriki.
Wanaharakati waliwarushia mabomu ya Petroli na mawe Polisi na kuchoma motomagari baada ya Matembezi yaliyohusisha mamia ya Waandamanaji.
Mpango wa kupata mkopo pia umetikisa Chama cha Syriza.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG