Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Tuesday, March 3, 2015

Mama wa Katibu wa Mbunge afariki Dunia, wilayani Kibaha mkoani pwani

              

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
…………………………………………………….
MAMA wa Katibu wa Mbunge wa Viti Maalum Al Shaimar Kweigyir
Semeni Kingaru, anayeitwa Kibibi Haji Pembe, amefariki Dunia leo saa tano
asubuhi akiwa na umri wa miaka 80.
Semeni Kingaru kulia ambaye ni Katibu wa Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaimar Kweigyir, akiwa na mama yake mzazi Bi Kibibi Haji, ambaye amefariki Dunia leo asubuhi, wilayani Kibaha, mkoani Pwani.
 
Mama huyo amefariki nyumbani kwake kijiji cha
Misugusugu,wilayani Kibaha, mkoani Pwani, baada ya kuugua kwa muda mrefu.
 
Mtoto wa marehemu huyo Kingaru ambaye ni Katibu wa mbunge Al
Shaimar aliuambia mtandao huu kuwa mama yake atazikwa kesho saa 10 jioni kijijini
hapo kwa ajili ya kumsitiri.
 
Alisema kuwa kwa wanaopenda kushiriki kwenye msiba huo
watalazimika kushuka katika kituo cha kijiji cha Misugusugu ambapo ndipo sehemu
atakapozikwa marehemu mama yake.
 
Msiba huo wakati unatokea, Kingaru alikuwa nchini Uganda
katika majukumu yake na kulazimika kusitisha shughuli hizo kwa ajili ya kuwahi
msiba wa mama yake.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG