Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Thursday, April 23, 2015

AJALI YAUA MAUJAJI 17 , YAJERUHI 27 NEPAL


Taswira kutoka eneo la ajali.
MAUJAJI 17 wa dhehebu la Kihindu kutoka India wamepoteza maisha leo katika ajali ya basi walilokuwa wakisafiria katika Wilaya ya Dhading karibu na Mji wa Kathmandu nchini Nepal.
Katika ajali hiyo, maujaji 27 wamejeruhiwa huku watano kati yao wakiripotiwa kuwa katika hali mbaya, Ubalozi wa India nchini Nepal umeeleza. 
Basi hilo lilikuwa likitoka Kathmandu kwenda Mji wa Gorakhpur. Maujaji hao walikuwa wakirejea nyumbani baada ya kumaliza kuhiji katika Hekalu la Pashupatinath mjini Kathmandu.
Kupitia mtandao wa Twitter, Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi ametuma salamu za rambirambi kwa ndugu na jamaa waliopoteza maisha katika ajali hiyo huku akieleza kuwa watu wao waliopo katika ubalozi wa India nchini Nepal wamefika eneo la tukio mapema na kwa sasa wapo katika kila hospitali walipopelekwa majeruhi wa ajali hiyo na wanatoa huduma zinazostahili. 
Kutokana na taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Basudev Ghimire ni kwamba basi hilo lilipoteza mwelekeo na kupinduka kisha kudondoka chini umbali wa mita 150 kutoka barabarani.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG