Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Sunday, April 5, 2015

Garissa:Kenya kuomboleza kwa siku tatu

Uhuru Kenyatta
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza siku tatu za maombolezi ya kitaifa kufuatia shambulizi la chuo kikuu cha Garissa ambapo takriban wanafunzi 148 waliuawa huku wengine 79 wakijeruhiwa.
Akihutubia taifa siku moja baada ya shambulizi hilo,rais Kenyatta amesema kuwa serikali yake itawachukulia hatua kali waliotekeleza shambulizi hilo.
Amasema kuwa waliopanga na kufadhili shambulizi hilo wako katika jamii na kwamba serikali itapata habari ya wahusika ili kukabiliana na wahalifu hao.
Amewataka wazazi,viongozi wa kidini pamoja na wale wa kisiasa kuchukua jukumu kufuatia vijana kupewa mafunzo ya itikadi kali na kwamba serikali yake haitakubali uongozi wa kidini kuanzishwa nchini Kenya na kuongezea kuwa atatea sera za kidemokrasia za taifa kwa gharama yoyote ile.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG