Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Saturday, April 4, 2015

Raheem Sterling kucheza dhidi ya Arsenal

Raheem Sterling
Raheem Sterling ataanzishwa katika mechi dhidi ya Arsenal siku ya jumamosi licha ya onyo kutoka kwa Brendan Rodgers kwamba kilabu hiyo ya Anfield inakabiliwa na changamoto ya kuwazuia wachezaji wake wazuri kuondoka.
Mkufunzi huyo wa Liverpool amethibitisha kuwa Raheem atachukua mahala pake dhidi ya Arsenal licha mchezaji huyo wa miaka 20 kukiri kwamba anahusishwa na kilabu ya Arsenal.
Sterling ambaye anarejea katika mchuano muhimu wa Liverpool ambao huenda ukaaamua iwapo kilabu hiyo itacheza katika kombe la vilabu bingwa Ulaya amekataa mkataba wa pauni 100,000 kwa wiki.
Hatahivyo Rodgers atamuanzisha mchezaji huyo dhidi ya kilabu hiyo inayopanga kumnunua mwishoni mwa msimu huu.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG