Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Wednesday, July 8, 2015

ZANTEL YASAIDIA CHAMA CHA MAALBINO TANZANIA KUTOA ELIMU KWA UMMA


Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Pratap Ghose akikabidhi hundi ya shilingi milioni tano kwa Mwenyekiti wa Chama cha Maalbino Tanzania, Bwana Ernest Kimaya.
Mwenyekiti wa Chama cha Maalbino Tanzania, Ernest Kimaya akizungumza na waandishi wa habari leo juu ya ushirikiano na kampuni ya Zantel leo. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Pratap Ghose na Mkurugenzi wa Masoko wa Zantel, Bi Progress Chisenga,

Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Pratap Ghose (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo juu ya ushirikiano wao na chama cha Maalbino Tanzania. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa Zantel, Bi Progress Chisenga, na Mwenyekiti wa Chama cha Maalbino Tanzania, Ernest Kimaya
Kampuni ya simu za mikononi ya Zantel leo imekisaidia Chama cha Maalbino Tanzania katika mpango wake wa kusambaza elimu juu ya ulemavu wa ngozi kwa jamii pamoja na msaada wa jumla ya shilingi milioni 5 ambao unalenga kusaidia uendeshaji wa shughuli zake hapa nchini.
Zantel kwa kushirikiana na Chama Cha Maalbino kitajikita kutoa elimu hii kwa kusambaza ujumbe mfupi kwa wateja wake pamoja na kutumia vipindi vyake inavyodhamini ili kupeleka ujumbe kwa jamii kiujumla.
Pamoja na hiyo pia, Zantel inajipanga kutumia mikutano ya wafanyakazi pamoja na matamasha ili kuhakikisha ujumbe kuhusu ulemavu wa ngozi unawafikia watu wengi zaidi

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG