Mwanamke mmoja wa Ufaransa KLOR BOR amepata ujanja wa kuwapa mwamko
wanachi wa mji mkuu wa nchi hiyo Paris dhidi uharibifu wa vipande vya
sigara vilivyomalizika kuvutwa ambavyo vinatupwa tupwa ovyo njiani hasa
ktk mitaa iliyokaribu na maeneo ya treni ya chini ya ardhi yaani Metro.
Mwanadada huyo ametengeza vazi la sketi alilolitengeneza mwenyewe kwa
maelfu ya vipande vya sigara.
***kionjo***
Umuhimu mkubwa wa afya nchini Italia sio kwa binaadam peke yake, bali
mpaka miti imepewa kipaumbe ktk kuwa na afya nzuri. Nchini humo miti
midogo2 imezungushiwa kipande cha kitambaa chepesi kwa ajili ya
kuihifadhi miti hiyo isipigwe na baridi ya hali ya hewa, ili iweze kukua
vizuri ktk mazingira yake ya kiasili. Lakini cha ajabu zaidi ni kuwa
vitambaa vilivyozongewa miti hiyo vina rangi ya kijani ili miti hiyo
isitafautiane na mengine.
Aina ya ajabu ya mazoea mabaya yaliyomkumba Mmarekani aitwae PITAMIST
HANDERSON ambayo yanamsababishia kula sabuni na shampoo za kukogea tokea
alipokuwa mtoto mdogo. Hapo mwanzo alikuwa anapenda harufu na hatimaye
mapenzi yameongezeka zaidi na akaamua aonje ladha ya sabuni hizo. Baada
ya kuonja ikampendezesha ladha na akaendelea kula sabuni hizo mpaka
akawa na mazoea nazo hadi leo hii. Na anakula vipande vitano vya sabuni
kwa wiki. Na baada ya kupita miezi kadhaa ya mazoea haya ameamua kuomba
msaada wa madaktari ili aondokane na mazoea haya.
Na ktk habari za kusisimua kabisa ….. ni kuwa kitabu kimoja chenye jina
la “MAMBO YANAYOWASHUGHULISHA MNO WANAUME” kilichotungwa na profesa
SHARIDAN SAIMON kimetawala mitaani. Cha kushangaza ni kuwa … kurasa za
kitabu hichi ni tupu yaani hazijaandikwa hata neno moja wala picha wala
alama yoyote ile. Lakn kwa namna ya ulivyo muundo wake wa kuvutia kati
ya anuani na vilivyomo ni muundo haujawahi kukuwepo hapo kabla. Kitabu
hichi kimepanda chati na kuwa miongoni mwa vitabu vilivyouzwa sana na
kimekuwa juu hata kuvishinda baadhi ya vitabu mashuhuri duniani.
Na hatimae nchini Marekani wakati mkimbiaji MERY mwenye umri wa miaka 72
ameshinda vita vilivyokuwa vikali kati yake na mamba, akipigania
kumuoko mbwa wake kutoka ktk kinywa cha mamba. Kwani alimuona mbwa wake
aitwae JERY mwenye miaka 11 yupo kinywani mwa mamba. Akaamua kumrukia
mamba huyo mgongoni na kuanza kumpiga kichwani mpaka akamuacha mbwa
wake. Na akafanya haraka kumkimbiza hospitali ambapo alipatiwa matibabu.
Na Mery amesema yeye sio shujaa, bali jambo kubwa alilolitaka ni
kumuokoa mbwa wake.
|
|
|
No comments:
Post a Comment