30th August 2014
Fredy Felix Minziro
Michuano hiyo inayoshirikisha michezo tofauti kutoka kwa timu mbalimbali za majeshi za Ukanda huo, inafikia ukingoni kesho.
Akizungumza na NIPASHE jana, Minziro alisema kipa Shaaban Dihile na
wachezaji Damasi Makwaya na George Minja ambao wana mchango mkubwa JKT
Ruvu ni miongoni mwa wachezaji wake walio Zanzibar.
Kutokana na kuwepo kwa hali, alisema Minziro, hatoweza kutaja
kikosi cha kwanza mpaka Septemba Mosi ambapo wachezaji hao watakuwa
wameungana na wenzao katika maandalizi ya ligi kuu ya Bara inayoanza
Septemba 20.
Alisema anaendelea na mazoezi ya kila siku kwa timu hiyo, ikiwemo
kuinoa safu ya ushambuliaji zaidi ambayo ikiimarika itaipa nafasi JKT
Ruvu kupachika mabao zaidi kwenye ligi kuu.
"Tumecheza mechi nyingi za majaribio, zimenisaidia kiasi kikubwa kufanya marekebisho kwa wachezaji wangu," alisema Minziro.
Alisema bado anaendelea kutafuta mechi nyingine za majaribio kabla ya ligi kuu kuanza.
Minziro alisema JKT imesajili wachezaji chipukizi na wazoefu, ambao
anaamini wakiungana pamoja, kikosi hicho kitafanya maajabu kwenye ligi
kuu ya Bara.
Alisema chipukizi waliopo wameonyesha uwezo mkubwa katika mazoezi
na mechi za kirafiki ambazo wamecheza, na akaeleza zaidi kuwa hali hiyo
inampa moyo wa kujiamini kuwa timu itafanya vizuri msimu huu.
JKT inafungua pazia la ligi kuu ya Bara dhidi ya Mbeya City iliyoshika nafasi ya tatu mwaka jana
No comments:
Post a Comment