- Written by Tupambane Blog
Engineer
Carlos Mkindi ambaye ni mkurugenzi wa mkundi production akiongea na
vyombo vya habari kuhusiana na Tamasha kubwa la upendo kwa mama
linalotarajiwa kufanyika jijini Arusha katika uwanja wa Sheikh Amri
Abeid tarehe 02-11-2014
Engineer
Carlos Mkindi ambaye ni mkurugenzi wa mkundi production akiongea na
wanahabari kuhusiana na Tamasha la Upendo kwa mama ambalo linalenga
kutoa mitaji kwa zaidi ya akina mama 50 wajasiriamali ili kuwawezesha
kujiajiri pamoja na kuwaombea na kuwashukuru kwa moyo wa upendo
waliyonayo kwa kujitoa katika kusimamia familia na malezi
Mratibu wa Tamasha la Upendo kwa mama Bw. Linus Kilembu akiongelea maandalizi ya Tamasha kuwa limekamilika kwa asilimia 90. (T.K)
Engineer
Carlos Mkindi mwenyekiti wa Tamasha la upendo ambaye ni mkurugenzi wa
mkundi production akifanyiwa mahojiano na wanahabari katika studio za
mkundi production zilizopo njiro mkoani Arusha
Ndani ya
mwezi ujao wa Kumi na Moja (November) Tarehe 2 itakuwa ni siku yenye
Neema kwani Arusha Kutashushwa Baraka ya Kumthamini na kumuonyesha
Upendo Mama Wa Kitanzania na Duniani Kote.
Hadi sasa
Maandalizi ya Tamasha la Upendo kwa Mama Yamekamilika ambapo Tarehe 2
November 2014 Ndani ya Viwanja vya Sheikh Amri Abeid Kutafanyika tamasha
hilo lililobarikiwa jina la UPENDO KWA MAMA ambapo Tamasha hilo
litaongozwa na waimbaji wa Nyimbo za Injili wakubwa kutoka humu Nchini
na Nchi Jirani ya Kenya.
Wasanii
hao wa Injili Watakaoongoza Tamasha la UPENDO KWA MAMA Sara K kutoka
Nchini Kenya na Cristina Shusho kutoka Tanzania, huku likipambwa na
Ambwene Mwasongwe, Baraka Maasa, Eng calros Mkundi, Ester Bukuku, Matha
Mwaipaja, Nesta sanga, Meth Chengula, Matumaini, Eline Patrick bila
kuwasahau waimbaji wengine kutoka Mkoani Arusha pamoja na Kwaya
Mbalimbali.
Lengo
hasa la tamasha hilo la UPENDO KWA MAMA ni kutoa Mitaji kwa zaidi ya
akina mama 50 wajasiriamali ili kuwaongezea uwezo wa kujiajiri, vilevile
utakuwa ni wakati mwafaka wa kuwashukuru wakinamama wote kwa upendo
walionao ukiambatana na kujitolea katika kusimamia Familia na malezi ya
watoto.
Kama
Mtanzania au Usiyekuwa Mtanzania mwenye Mapenzi na mama Basi unaalikwa
Kufika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha Tarehe hiyo na
utashuhudia Tamsha hilo kwa Kuchangia Kiingilio Kidogo tu ambacho ni Sh.
3,000/= (Elfu Tatu ya Kitanzania)
Tamasha
la UPENDO KWA MAMA limeandaliwa na Mkundi Production ya Jijini Arusha na
wao kama kamati ya maandalizi ya Tamasha la UPENDO KWA MAMA wanatoa
nafasi kwa watanzania, Taasisi na Mashirika yote ambayo yako tayari
kuungana na Studio ya Mkundi kwa Ufadhili wa hali na mali ili
kufanikisha tamasha hili la UPENDO KWA MAMA
No comments:
Post a Comment