- Written by Tupambane Blog
- Tuma Maoni
-
Share on facebook Share on gmail Share on twitter
Bomu lililotengenezwa kienyeji kama linavoonekana katika picha.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela akipata maelekezo kutoka kwa
mtaaram wa mabomu ambaye ni kamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa
Tanzania(JWTZ) kabla ya kulitegua bomu hili.
Hili ni
eneo la tukio ambalo limezungushiwa mkanda huu wa pilisi uliandikwa
hairuhusiwi kupita eneo hili,Lakini chini ya huo mti kama inavoonekana
katika picha kukiwa na udongo umetifuliwa ndipo mahara ambapo lilitegwa
bomu hili la kutengenezwa kienyeji pia hapo ndipo huwa wanakaa askari wa
Usalama barabarani kwa kujikinga na jua ama kupumzika pindi wanapokuwa
kazini.(Martha Magessa)
Bomu lililotengenezwa kienyeji
Mtaaramu toka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania akiweka vifaa vyake vya kutegulia bomu hilo lililo tengenezwa kienyeji.
Mtaaramu
toka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania akiwa anaonyesha umahili
wake alionao aweze kulitegua bila kuleta madhara yoyote yale katika
jamii
Jeshi la
polisi kwa kushirikiana na Jeshi la Ulinzi la wananchi Tanzania(JWTZ)
wamefanikiwa kulipua bomu lililotegwa katika eneo la kituo cha kurushia
matangazo kilichopo mshangano cha shirika la utangazaji Tanzania (TBC)
Songea Mkoani Ruvuma siku ya jana majira ya saa moja jioni.
Bomu hili
linalosadikiwa kutengenezwa kienyeji nawatu wasiojulikana lilitegwa
hatua zinazokadiliwa thelathini kutoka kitika kituo kilipo katika eneo
ambalo askari wa usalama barabarani wanakaa kwa ajili kufanya kazi zao
za kila siku.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela amesema kwamujibu wa wataalamu
wa milipuko kutoka jeshi la Ulinmzi la wananchi wa Tanzania bomu hili
linaonekakana limetengenezwa kienyeji.
ameitaka
jamii kutoa ushrikiano kwa jeshi la polisi ili liweze kuwabaini watu
waliowalipua kwa bomu lililotengenezwa kienyeji askari polisi
watatu wakiwa katika doria katika kata ya misufini manispaa ya songea.
Msikhela
amesema Jeshi la polisi linafanya jitihada za kuwapata watu hawa
wanaohusika na mtandao huu wa utegaji wa mabomu na ulipuaji, Aidha
ameitaka jamii kutoa ushrikiano kwa Jeshi la Polisi ili liweze kuwabaini
watu wanaousika na matukio ya namana hii.
Na hii ni
mara ya pili katika manispaa ya songea kutokea kwa matukio haya ambapo
tarehe Oktoba 16 mwaka huuaskari watatu wa jeshi la polisi katika wilaya
ya Songea mkoani Ruvuma, walijeruhiwa kwa kitu kinachosadikiwa kuwa ni
bomu la kutupwa kwa mkono ambalo lilisadikiwa kutengenezwa kienyeji,
katika eneo la matarawe mjini songea mkoani Ruvuma.
Askari
hao walikutwa na mkasa huo saa moja na nusu usiku wakati wakiwa katika
doria ambao ni WP Felista Abel, PC John Kaduma na PC Ramadhani Ally
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Joseph Mkirikiti akizungumza na
mtandao huu wa demasho kwa njia ya simu amesikitishwa na kitendo hicho
cha utegeji wa Mabomu ikiwa nikutaka kuhatarisha amani iliyopo katika
mkoa huu wa Ruvuma.
Aidha
amesema serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama
watahakikisha wanawasaka na kuwakamata walewote wanaohusika na vitendo
hivi.
No comments:
Post a Comment