Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Friday, October 24, 2014

Kuelekea uchaguzi Mkuu 2015: Serikali yaongeza kata mpya 51 Kanda ya Ziwa

  • Written by  Tupambane blog
  • Print
  • Email
  • Add new comment
PindaMWANZA: Serikali imetangaza kata mapya zaidi ya 51 zilizoongezeka hivyo kubadili eneo la Utawala katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na kufanya mikoa ya kanda ya ziwa kuwa na ongezeko la kata na mitaa.
Kwa mujibu wa tangazo la serikali Na 300 lililotolewa Agosti 22 mwaka huu na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) imeonyesha maoeneo hayo kwa baadhi ya mikoa ya Kanda ya Ziwa Mwanza ya Kagera, Shinyanga, Mara, Simiyu na Geita.
Mkoa wa Mwanza Wilaya ya Ilemela, Manispa ya Ilemela, awali ilikuwa na Kata tisa za Kirumba, Kitangiri, Nyamanoro, Pansiasi, Ilemela, Sangabuye, Bugogwa, Nyakato na Buswelu ambapo Kata 11 mpya zilizoongezwa baada ya kugawanywa kutokana na mapendekezo ya Manispaa hiyo yaliyowasilishwa TAMISEMI.
Alizitaja Kata 11 mpya kuwa ni Kata za Mecco, Buzuruga, Nyansaka, Ibungilo, Kiseske, Kayenze, Shibula, Kawekamo, Kahama, Kiseke, Nyamhongolo jumla zikiwa na mitaa 172 ikijumuisha ya zamani na mipya.
Wilaya ya Nyamagana, Halmashauri ya Jiji la Mwanza, awali ilikuwa na Kata 12 za Nyamagana, Isamilo, Mirongo, Mbugani, Pamba, Igogo, Mkuyuni, Butimba, Mkolani , Buhongwa, Mahina na Igoma na mitaa 110 na sasa Kata mpya sita zimeongezeka baada ya kugawanywa na kuundwa Kata za Luchelele, Lwanhima, Nyegezi, Mabatini, Kishiri na Mhandu ambapo jumla zitakuwa 18 zenye mitaa 175.
Mkoa wa Mara, Wilaya Musoma Mjini, Manispaa ya Musoma, iliyokuwa na Kata 13 na kufikia  16 ambazo ni Kata ya Bweri, Rwamlima (mpya), Kigera, Kwangwa (mpya), Makoko, Mwisenge, Nyakato, Mshikamano (Mpya), Buhare, Iringo, Kamunyonge, Kitaji, Mkendo, Mwigobero, Nyamatare na Nyasho.
Wilaya ya Tarime, Halmashauri ya Mji wa Tarime awali ulikuwa na Kata sita na baada ya kugawanywa zimeongezeka mbili na kuwa jumla ya Kata nane ambazo ni Bomani, Nyamisangura, Sabasaba, Turwa, Nkende (mpya), Kenyamanyori (Mpya) na Kitare ambazo jumla zitakuwa na mitaa 73.
Mkoa wa Simiyu, Halmashauri ya Mji wa Bariadi, awali haikuwa na mitaa wakati wa uchaguzi Mkuu 2010 hivyo baada ya kuanzishwa sasa imepata mitaa 92 na kutoka katika Kata 10 zilizopo za Bunamhala, Bariadi, Malambo, Nyangokolwa, Isanga, Sima, Somanda, Guduwi, Nyakabindi na Mhango.
Mkoa wa Geita, Halmashauri ya Mji wa Geita, ilikuwa na Kata saba za Kalangalala, Mtakuja, Kasamwa, Bung’wangoko, Bulela, Nyanguku na Ihanamilo na sasa baada ya baadhi kugawanywa zimeundwa Kata mpya tano za Buhalala, Nyankumbu, Bombambili, Mgusu, Kanyala na kuwa na jumla ya mitaa 50 vijiji 13 na vitongoji 47 katika mapendekezo yaliyopitishwa.
Mkoa wa Shinyanga, Halmashauri ya Mji wa Kahama, awali ilikuwa na Kata sita za Kahama Mjini, Malunga, Zongomela, Nyihogo, Mhongolo na Mwenda kulima ambazo baada ya kugawanywa zimefikia Kata 20 ambapo Kata 14 mpya ni Nyandekwa, Majengo, Nyasubi, Nyahanga, Busoka, Isagehe, Mondo, Kagongwa, Kinaga, Kilango Iyenze, Ngogwa na Wendele  ikatayokuwa na jumla ya mitaa 32, vijiji 42 na vitongoji 218.
Manispaa ya Shinyanga inazo Kata 17 ambazo ni Kambarage, Lubaga, Chamaguha, Ibinzamata, Shinyanga Mjini, Ndala, Masekelo, Kitangili, Ngokolo, Ndembezi, Mwawaza, Kizumbi, Ibadakuli, Kolandoto, Old Shinyanga, Mwamalili na Chibe ambapo haikuwa na mitaa na sasa mitaa 55, Vijiji 17 na Vitongoji 84 kwa mjibu wa mapendekezo yaliyopitishwa na TAMISEMI.
Mkoa wa Kagera, Manispaa ya Bukoba inazo Kata 14 za Kashai, Bilele, Hamugembe, Miembeni, Bukoba Mjini, Ijuganyondo, Kibeta, Kitendaguro, Nshambya, Rwamishenye, Buhembe, Nyanga, Kahororo, Kagondo, ambapo iliwasilisha mapendekezo ya kuongeza idadi ya ya Kata na mitaa lakini zimebaki kama ilivyokuwa 14 za awali na mitaa 66.
Mkoa wa Tabora,  katika uchaguzi wa mwaka 2010 ilikuwa na Kata 28 na sasa imeongezeka Kata moja na kufikia 29 ambapo Kata za zamani ni Ipuli, Kitete, Chemchem, Mwinyi, Ng’ambo, Kidongochekundu, kiloleni, Mapambano, Mtendeni, Malolo, Tambuka-Reli, Isevya, Gongoni, Kanyenye, Mbugani, Cheyo, Ndevelwa na Kalunde.
Zingine ni Kata za Uyui, tumbi, Itonjanda, Ikomwa, Ifucha, Kabila, Misha, Kakola, Itetemia na Ntalikwa ambapo sasa imeongezeka Kata ya Mpela kufikia 29 ambazo zitakuwa na jumla ya mitaa 135, vijiji 32 na vitongoji 145.
Hatua hii inatokana na mapendekezo ambayo yalipelekwa na baadhi ya vikao vya Halmashauri za Majiji, Manispaa na Halmashauri za Miji kupitia Kamati za Ushauri za Mikoa (RCC) husika ambapo TAMISEMI imelidhia na kupitisha ambapo sasa zitahusika katika uchaguzi mkuu wa serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu wa Rais, Madiwani na Wabunge mwaka 2015 kote nchini.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG