linapokuja suala
la kuzidi kiasi tunapata matatizo ya msingi ambayo
huleta madhara
kwa watu wanaoendekeza sana ngono.
Kuna watu ambao
hawezi kulala bila kufanya mapenzi na huku wengine
wakikosa uwezo wa
kuvumilia hata kwa siku mbili au tatu.
Mtu anaweza kuwa
na mke na kujikuta kila siku anatumia ‘chakula cha
usiku’ kwa sababu
tu hakuna wa kumkataza na kwamba ana haki ya kufanya
hivyo kwa sababu
amelipa mahari.
Hilo linaweza kuwa jambo jema kwa upande
mwingine, lakini uchunguzi
unaonyesha kuwa
watu wengi kati ya watu wanaolalamika kupoteza hisia za
kimapenzi hutoka
katika kundi la watu wapenda ngono.
Pamoja na tatizo
hilo, yapo madhara mengine mengi ambayo mtu asiyekuwa
na kiasi katika
tendo la ndoa anaweza kukabiliana nayo, hivyo ni vema
tukajifunza ili
tusiwe watu wa kuendekeza miili kiasi cha kulazimika
kufanya mapenzi
kila tunapokutana hata kwenye nguzo ya umeme na chini ya
miti kwa vile tu miili
imetaka kufurahika.
Twende pamoja
katika kutazama madhara hayo kwa kina.
KUPOTEZA HAMU YA
TENDO.
Watu wenye pupa
za kufanya mapenzi hupoteza haraka hisia za kimapenzi
kwa wapenzi wao
kutokana na sababu za kisaikolojia zinazoweza kujitokeza
wakati wa
ufanyaji wa tendo la ndoa mara kwa mara.
Sababu hizo
zinaweza kuwa ni pamoja na zile za kumzoea mwenza kiasi cha
kukosa msisimko
hata anapomuona akiwa mtupu.
Aidha kukinai
haraka staili za kimapenzi kunatajwa kujitokeza kutokana
na kukutana mara
kwa mara kwa aina zile zile za mapenzi na pengine
sehemu moja,
kitanda kimoja na chumba kile kile, jambo ambalo linaweza
kumfanya mhusika
asione jipya kutoka kwa mwenza wake na hivyo kupoteza
hamu naye na
kuhisi kama hawezi tena kushiriki tendo la ndoa kikamilifu.
KUUJAZA MWILI
TAMAA KUBWA.
Tabia ya kufanya
mapenzi mara kwa mara huongeza uzalishaji wa homoni
mwilini na
kuufanya mwili uwe na msukumo mkubwa wa kutaka kuridhishwa
kwa tendo la ndoa
bila kukosa na hivyo kumfanya mhusika asiwe mtu mwenye
uwezo wa kuzuia
tamaa na kukosa chaguo la nani wa kufanya naye mapenzi
na kwa wakati
gani?
Watu
wanaojiendekeza katika kufanya mapenzi mara kwa mara ndiyo wale
ambao kila
wanayemtazama barabarani humtamani bila kujali hadhi yake.
Hawa ndiyo wanaobaka, kusaliti ndoa zao hata
kwa watumishi wa ndani au
kufanya mapenzi
na watoto wao wa kuwazaa kwa vile akili zao huwa
zimeathirika kwa
tamaa ya mapenzi.
Unapokuwa mtu wa kufanya mapenzi mara kwa mara
huwezi kuwa na uwezo wa
kuzuia tamaa yako.
Mumeo akiondoka siku mbili unatamani kuwa hata na
houseboy ili
akukate kiu ya penzi.
KUPOTEZA RAHA
KAMILI YA TENDO.
Raha ya tendo
hutegemea sana hisia iliyokuzwa kutokana na mapenzi sahihi
na kiu ya kufanya
mapenzi, hivyo basi ukiwa mtu wa kufanya mapenzi kila
mara unaweza
kupoteza msisimko wa tendo na kujikuta unapata furaha
ambayo haikutoshi
kumaliza tamaa yako.
Kama ni mapenzi utakuwa unayafanya kwa mazoea
tu na msisimko wako
utakuwa mdogo!
KUPOTEZA NGUVU ZA
MWILI.
Madhara mengine
yanayoweza kupatikana kwa kufanya mapenzi mara kwa mara
ni pamoja na
kupoteza nguvu nyingi za mwili.
Kama tujuavyo tendo la ndoa hasa kwa wanaume
huwafanya watumie nguvu
nyingi, hivyo
kuufanya mwili uchoke. Aidha lishe inapokuwa ndogo kwa
wafanya mapenzi
mwili hukosa nguvu za kutosha kuhimili misukosuko ya
kimaisha.
Sambamba na hilo
mbegu za uzazi zinazotoka kwa wanaume wanaofanya
mapenzi mara kwa
mara huwa dhaifu.
KUPATA MAGONJWA.
Kama
tulivyojifunza kuwa watu wanaofanya mapenzi mara kwa mara huwa na
tamaa na hujikuta
wanafanya mapenzi holela ambayo huweza kuwasababishia
magonjwa ya zinaa
ukiwemo ukimwi, lakini ufanyaji wa mapenzi usiokuwa na
msukumo wa
kutosha hasa kwa wanawake huwafanya waishiwe msisimko na
kuzifanya sehemu
zao za siri kutotoa ute unaoweza kuwakinga na michubuko
wakati wa
kujamiiana na hivyo kuwasababishia michubuko itakayoweza
kuleta maambukizi
ya haraka ya magonjwa ya zinaa ukiwemo ukimwi.
No comments:
Post a Comment