Ndugu zangu,
Nimeyaandika haya kufuatia mada niliyoianzisha juu ya hamu inayojengeka kwenye jamii ya kutamani udikteta.
Nimemjibu ndugu Galinoma kama ifuatavyo;
"Galinoma,
foleni za unga haikumaanisha udikteta. Dunia ilikuwa tofauti na sasa.
Dunia ilikuwa kwenye vita baridi na mapambano ya kiitikadi; Ujamaa dhidi
ya Ubepari. Mimi ni Mjamaa, na zaidi ni Social Democrat.
Nimekulia
katikati ya mapambano hayo ya kiitikadi. Nchi yetu wakati huo ilipitia
mitihani migumu mitano kama taifa; Mtihani wa kwanza; migogoro miwili ya
mafuta duniani.
Ni kati
ya 70 na 73. Mtihani wa kwanza wa mafuta ni mwaka 1970. Wa pili mwaka
1973. Mtihani wa tatu ni ukame wa mwaka 74. Watanzania tulikula 'Unga wa
Yanga' kwa maana ya unga wa njano. Mtihani wa nne ni kuvunjika kwa
jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1977. Mtihani wa tano ni Vita vya
Kagera 1978-79.
Ndani ya
miaka kumi nchi yetu ilipitia mitihani migumu mitano. Nilikuwa na miaka
kumi na moja pale Kinondoni Biafra, nilipomsikia kupitia redio, Julius
Nyerere akitangaza vita dhidi ya dikteta Idd Amin aliyetuvamia na
kuchukua sehemu ya ardhi yetu.
Usiku ule
niliyaona magari ya kijeshi yakipita nje ya nyumba yetu, Morocco rd,
yakitokea kambi ya Lugalo kwenda mpakani. Ndio, nimeishi na kushuhudia
mwaka ule wa 79, pale uwanja wa taifa, mbali ya kumpoteza rubani wetu
kwenye ndege ya kivita iliyokuwa ituangukie uwanjani, lakini rubani
akajitahidi aende akaanguke nayo nje ya uwanja, Julius Nyerere alitoa
hotuba muhimu yenye kutuandama hadi leo. Alirudia kusema kuwa vita si
lelemama, na kwamba Watanzania tujiandae kufunga mikanda kwa miezi kumi
na nane. Na hakika imekuwa zaidi ya miaka 18, na hadi leo tuna makovu ya
vita. Ni makovu ya kiuchumi.(T.K)
Naam,
ndani ya miaka kumi nchi yetu ilipitia mitihani mitano migumu. Nyerere
hakuwa dikteta, alijenga uongozi wa kitaifa uliojenga ushawishi na
mshikamano wa kitaifa tukaweza, hata kwa tabu, kuvuka mitihani hiyo
mitano na tukabaki kama taifa.
Ndio
maana leo, inashangaza, wakati tumepoteza ndugu zetu kupambana na
kumng'oa dikteta Idd Amin, tunajadili hamu ya kuwa na rais dikteta.
Historia ni mwalimu mzuri, tuipitie historia yetu. Uganda wamekuwa na
dikteta Idd Amin kwa miaka 8, lakini, hata Amin hakumaliza rushwa kwa
vifaru vyake vya jeshi. Badala yake alisambaza hofu kwa Waganda na
kuwaandama na hata kuwapoteza wapinzani wake.
Na kwa vile , kama taifa, tumepigana na kumshinda dikteta, basi, tusikubali kumkaribisha wenyewe dikteta ndani ya ua wetu...
Maggid Mjengwa.
59 mins · Like
Maggid Mjengwa.
59 mins · Like
Joey
Galinoma Nashukuru kwa somo lililojitosheleza sana. Nadhani somo
litasaidia kuelimisha wengine waliochangia uzi huu. Usiku mwema.
33 mins · Unlike · 1
33 mins · Unlike · 1
Maggid
Mjengwa Asante sana Galinoma kwa kunielewa. Tofauti za kimawazo ni jambo
la siha kwa jamii ili iendelee, ingawa kwenye udikteta yaweza kuwa
nongwa!
No comments:
Post a Comment