SAA LA 25
Ilipoishia...
Haikuchukua muda
tax ilifika mahali panapotakiwa. Zai alilipana kulijongea geti kubwa la nyumba
hiyo. Baada ya kubofya kengele mlango ulifunguka wenyewe nae akaingia ndani,
hakuwa mgeni na nyumba hiyo ambayo amekwishafika mara kadhaa, moja kwa moja
alipitiliza sebuleni na kulakiwa na mwenyeji wake Mr Dam Dam. Wakiwa juu ya
kochi kubwa lililo sebuleni hapo makumbatiano hayakuwa haba na mabusu motomoto
kabla hawajakokotana chumbani.
“Darlin,
nina shida mwenzio” zai alianza ubembe wake kwa mwanaume huyo
“Sema, nakusikiliza
darling, hakuna shida itakayokuwa ngumu mbele ya pesa.” Zai alimueleza
Dam Dam mambo yote juu ya Kautipe kuwekwa ndani kwa kosa la kushukiwa kuwa na
biashara ya bangi, lakini kila alipotaka kumjuza kuhusu Ashura roho yake
ilisitasita.
“Ok, nimekuelewa, sasa siku
ya kesi wewe utamuwekea dhamana ya shilingi milioni moja, sawa?” Damdam
alimueleza Zai huku akimchezea chuchu zake zilizochongoka kama mshale. Zai
aliitika kwa kichwa akaona kuwa hapo moja amelimaliza na linalobaki endelea...
“Ok, nimekuelewa,
sasa siku ya kesi wewe utamuwekea dhamana ya shilingi milioni moja, sawa?” Damdam
alimueleza Zai huku akimchezea chuchu zake zilizochongoka kama mshale. Zai
aliitika kwa kichwa akaona kuwa hapo moja amelimaliza na linalobaki
angemshirikisha mwingine kumsaidia.
“Nashukuru Damdam.”
Zai alimshukuru mwanaume huyo na kumkumbatia, bila kusita Damdam naye
alimkumbatia Zai kwa bashasha kubwa na mapenzi yao yamuda mfupi kuchukua nafasi
yake juu ya kochi hilo kubwa huku wakisindikizwa kwa muziki laini uliotoka
kwenye spika kubwa za kisasa ambazo Damdam alizinunua alipokuwa katika moja ya
safari zake huko Uchina.
€ € € €
“Mgonjwa wenu hali
yake si nzuri, amepooza mwili, hivyo hana uwezo wa kufanya lolote kwa nguvu
zake” Dakta Msola aliwaeleza ndugu wa mzee Njiku, walipokuja kumtazama
hospitalini hapo. Sura za huzuni zilitawala nyuso za ndugu hawa walitazamana
kwa muda bila kupata chochote cha kuongea.
“Kwa vyovyote
wamemloga” Dada wa Mzee Njiku alianza kubwabwaja kama kawaida yake huku akitoka
nje ya chumba cha daktari kilichopo katika wodi hiyo.
“Hivi wewe kwa nini
unapenda kuamini uchawi?” kaka yake alimuuliza kwa hasira.
“Mimi najua,
wamemloga kaka yangu” aliendelea kusisitiza kaui yake
“Sasa wewe mwema
kwako nani?” kakaye aliuliza tena
“Hamna mwema, wote
wachawi tu. Yule mkewe wa kwanza alimloga kulipiza kisasi, na huyu nae mchawi
sasa anataka kurithi mali, na hazipati”, aling’aka dada yule huku akirusharusha
mikono yake kwa hasira.
“Jamani ndugu yetu
ndiyo huyo, tunamsaidiaje? Maana sasa hana hata pa kuishi” ndugu wa mzee Njiku
walikusanyika kuzungumza machache juu ya mgonjwa wao. Kila mtu alikuwa mzito
kutoa maamuzi ya nini cha kufanya, nani amchukue kumtunza, kila mmoja
alijesemea moyoni ‘nani abebe mzigo huo’. Baada ya mawili matatu
kuzungumzwa waliafikiana kumsafirisha nyumbani kijijini.
Wakiwa katika
mazungumzo hayo gari ya mama Minja ilisimama taratibu mbele ya jengo hilo la
hospitali, mama Njiku, mke wa ndoa wa mzee Njiku aliteremka na moja kwa moja
akamuendea shemeji yake.
“Asante kwa ujumbe,
niliupata ila nilikuwa mbali, namuomba mume wangu niondoke nae, nitamtunza
mwenyewe, huyu ni mume wangu” mama Njiku alisema maneno hayo ambayo yalimgusa
kila mmoja wao, wakikumbuka walivyomwita mchawi, walivyomfukuza kama
mbwa na kumthamini mwanamke mwengine ambaye sasa wameona yaliyompata kaka yao.
Kaka wa mzee Njiku alimwita pembeni mama Njiku na kumueleza majibu yote ya
daktari bila kumficha. Mama Njiku aliyapokea majibu hayo na moja kwa moja
alimuendea daktari kwa mazungumzo ya kina.
“Licha ya kupooza,
mumeo ameathirika na gonjwa la ukimwi, hivyo nizuri hata wewe kufanya vipimo
kwa uhakika zaidi”, Mama Njiku hakuonekana kushtuka kwa jambo hilo kwani
alilitegemea muda wowote kutokea, alitulia kimya akiwa kajishika tama, mawazo
yake yalimrudisha nyuma kabisa enzi za wawili hao wakiwa katika mtafaruku
mzito…
“Sawa, mi ntaondoka ntakuacha, lakini kumbuka maradhi
mume wangu, hao unaowathamini leo hujui wangapi walifanywa hivyo” Mama Njiku
alikuwa akiongea huku akitoa machozi akimueleza kwa uchungu baada ya kupokea
kipigo kikali kutoka kwa mumewe…
…aligutuka
aliposikia mlio wa chupa ya dawa iliyoanguka kwa bahati mbaya na kupasuka. Mama
Njiku alikubali kufanya vipimo ili kuhakikisha afya yake, baada ya majibu
kutoka aligundulika hakuwa na maambukizi. Alinyanyuka kutoka katika meza ile na
kuingia wodini kumuona mumewe. Aliketi pembeni kabisa ya Mzee Njiku
walitazamana uso kwa uso, machozi yaliwalenga wote wawili kila mmoja alijikuta
ana haki ya kumsamehe mwingine. Mzee Njiku hakuwa na uwezo hata wa kuongea
kutokana na hali yake, moyoni alitamani atamke japo neon moja la msamaha kwa
mkewe lakini haikuwa hivyo, aliongea ndani ya moyo wake
Nisamehe mke wangu
Yote ni makosa yangu
Ulifungwa moyo wangu
Sikujua nifanyalo
Niombee kwa wanangu
Sahau kauli zangu
‘mefika safari yangu
Ya kuuacha ulimwengu
Enyi waume wenzangu
Jifunzeni toka kwangu
Niliivunja nyumba yangu
Mapenzi yalihadaa
Jihadhari na rafiki
Wengi wao wanafiki
Wabilah tawfiq
Watakupoteza hakika
Moyo wangu waniuma
Kwa niloyafanya nyuma
Sina mbele wala nyuma
Kitandani naishia
Ninatubu kwa Mungu
Na kwako mke wangu
Ndugu na watoto wangu
Goti ninawapigia
Mama Njiku alizidi
kulia huku akiwa ameushika mkono wa mume wake ambaye sasa hakuweza kufanya
lolote, Mama Njiku aliyahisi maneno hayo kutoka kwenye macho ya mumewe,
aliuhisi msamaha wa nguvu na maneno mazito yaliyougusa moyo wake. Alipiga
magoti sakafuni na kumtazama mumewe aliye kufani kwa ukaribu zaidi, kinywa
chake kilifunguka akasema
Laazizi mume wangu
U mweupe moyo wangu
Hakuna kinyongo kwangu
Mimi nimekusamehe
Dunia yetu mapito
Mambo mpwitompwito
Hilo nalo ni pito
Mimi nimekusamehe
Marefu pa si na ncha
Hamna kutwa kwa kucha
Maadam kumekucha
Mimi nimekusamehe
Najua unaumia
Kwa yote yalotukia
Ni njia ya kupitia
Mimi nimekusamehe
Siku zote nilijua
Kuwa kwangu utarudia
Mimi ni mke wandoa
Wengine viruka njia
Mateso nilipitia
Gerezani kuingia
Maisha kunichachia
Kila kitu kupoteza
Yote tumuachie Mungu
Muumba nchi na mbingu
Toka kwako na kwangu
Maombi tumtolee
Nakupenda mume wangu
Kuliko wazazi wangu
Narudisha moyo wangu
Kwako laaziz wangu.
Mama Njiku aliuinua
mkono wa mumewe na kuubusu kisha kuukumbatia na kulia kwa machozi ya upendo.
Masikini, mzee Njiku, muda wake ulikuwa umefika tamati, macho yake yalishindana
na kiza kinene lakini nuru ilizidi kufifia kwa haraka, alihisi mabadiliko ya
maisha yakiivamia roho yake, mara tu, roho yake ikaacha mwili, macho yakafumba
akapumzika kwa amani.
Mama Njiku
alibubujikwa na machozi, alilia kwa uchungu, alitamani mumewe arudi wamalizie
maisha lakini haikuwa hivyo, mauti yalikwishamfika.
€ € € €
Kautipe alitulia
kimya katika chumba cha mahabusu pale mahakama ya mwanzo ya Chang’ombe. Alijua
wazi kuwa mwisho wake umefika kwa kosa lisilomhusu, atafungwa pasipo kutarajia.
Jalada lake
lilifika, kizimbani akasimama pamoja na Rasta, mahakama ikaendelea hakukuwa na
utetezi, hakimu alipoitisha dhamana kama ipo, Kautipe hakuamini macho yake. Zai
alijitokeza na kumuwekea dhamana Kautipe. Mambo yote ya kimahakama
yalipomalizika Kautipe na Zai walitoka mahakamani na kuketi kwenye grosary
moja iliyopo katika eneo hilo, waliagiza vinywaji na kunywa taratibu.
“Pole mdogo wangu!”
Zai alianzisha mazungumzo
“Asante da Zai, mi
nimekamatwa bure tu” Kautipe aliongea huku analia
“Basi yataisha tu
maadamu upo nje, tutafanya kinachowezekana” Zai alimfaraiji mwenzake.
“Nitashukuru, mi
naogopa” Kautipe aliendelea kulia
“Usiogope we tulia
tu”.
Punde si punde gari
moja nyeusi salon ilisimama eneo hilo, kioo cha mbele upande wa kulia
kiliteremka taratibu, hakuwa mwingine bali Mr Damdam. Zai alijiinua na Kautipe
wote wakaingia garini.
Msichana mmoja
alievalia baibui alikuwa akifuatilia nyendo zote za Zai na Kautipe kila hatua
mapka walipoingia garini humo, mara tu walipoondoka na ye alichuku tax
kuwafuata.
“Fuata hiyo gari
mpaka itapoishia” alimuamuru dereva, na dereva alitii amri ya mteja wake.
No comments:
Post a Comment