
MENEJA wa
Kiwanda cha Kimea - Moshi, Vitus Mhus akiwaonyesha hatua ya kwanza ya
zao la Shayiri linalotumika kutengenezea kimea mahali linapopokelewa
kabla ya kuanza kuingizwa kiwandani. Wakulima hao kutoka Vyama Nane vya
Ushirika vya wilaya ya Karatu na Monduli mkoani Arusha walitembelea
kiwandani hapo hapo juzi ili kujifunza na kujionea zao wanalolima
linaandaliwa vipi hadi kutengeneza Kimea

wakulima
wa zao la Shayiri kutoka Vyama Nane vya Ushirka vya wilaya ya Karatu na
Monduli mkoani Arusha wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya
kusikiliza maelezo namna ya kulima Shayiri yenye ubora kutoka kwa
Meneja Mradi Kilimo cha Shayiri Dk. Basson Bennie. Wakulima hao
walifurahia ziara iliyofanywa kwenye Kiwanda cha kuzalisha Kimea
kilichopo mjini Moshi ambapo waliahidi kulima Shayiri yenye ubora zaidi
katika msimu ujao.

Meneja
Uhusiano wa Kampuni ya Bia nchini (TBL), Edith Mushi akiwapa
maendelekezo wakulima wa zao la Shayiri waliotembelea Kiwanda cha
kuzalisha Kimea mjini Moshi namna ya kutembelea ndani ya kiwanda ili
wajionee namna Shayiri inavyozalishwa na kuwa Kimea.Wakulima hao
wanatoka kwenye vyama Nane vya Ushirika vilivypo wilaya ya Karatu na
Monduli mkjoani Arusha. (P.T)

Meneja wa
Kiwanda cha Kimea- Moshi Vitus Mhusi akiwaonyesha wakulima wa Shayiri
waliofanya ziara ya kutembelea kiwanda hicho namna uchafu
unavyochambuliwa kutoka kwenye Shayiri wanayolima mashambani, ambapo
aliwaomba kujitahidi kuhakikisha inakuwa safi wakati wa mavuno.

Pichani
ni Meneja wa Kiwanda cha Kimea kilichopo mjini Moshi akiwaonesha
wakulika kutoka Vyama vya Ushirika Nane vya Wilaya ya Karatu na Monduli
wanaolima Shayiri namna ambavyo uzalishaji wa kimea unavyofanyika,
wakati wa ziara yao.

Meneja wa
Kiwanda cha Kimea kilichopo Moshi, Vitus Mhusi akiwaonyesha wakulima wa
Shayiri namna Kimea kinavyozalishwa wakati wa ziara yao kiwandani hapo.
Vingozi hao wa Vyama vya Ushirika Nane kutoka wiayani Monduli na Karatu
mkoani Arusha walitembelea kiwandani hapo kwa leng la kujifunza zaidi
namna ya kulima zao la Shayiri lenye ubora zaidi na hata kufikia
mahitaji ya kiwanda ya Tani 12,000
No comments:
Post a Comment