- Written by Tupambane Blog
-
Share on facebook Share on gmail Share on twitter
Stori: Victor Bariety, Sengerema
WAJUKUU wa marehemu Sabina Ngalu (77) wameibua kutuko makaburini kufuatia kuzama ndani ya kaburi la marehemu huyo na kugoma kutoka wakidai kwamba mpaka walipwe shilingi laki moja (100,000), Uwazi lina mkanda mzima.
WAJUKUU wa marehemu Sabina Ngalu (77) wameibua kutuko makaburini kufuatia kuzama ndani ya kaburi la marehemu huyo na kugoma kutoka wakidai kwamba mpaka walipwe shilingi laki moja (100,000), Uwazi lina mkanda mzima.
Wajukuu wa bibi huyo wakiwa kaburini.
Tukio
hilo la aina yake lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita katika Kitongoji
cha Nyamwanza Kata ya Sima wilayani Sengerema mkoani Mwanza muda mfupi
baada ya mwili wa marehemu kuwasili eneo la mazishi kwenye shamba lake
ukitokea Kanisa la Roman Katoliki Parokia ya Yesu Kristo Mfalme la mjini
Sengerema.(T.K)
Sababu za
wajukuu hao kung’ang’ania ndani ya kaburi hilo walitaka wapewe ng’ombe
mmoja au pesa hizo taslimu kwa mjibu wa mila na desturi za kabila la
Kisukuma jambo ambalo lilipingwa na baadhi ya wanandugu waliodai mila
hizo zilipitwa na wakati.
Kufuatia
wajukuu hao kuendelea kugomea ndani ya kaburi, kaka wa marehemu, Enosi
Ngalu alikwenda kukata fimbo na kuwashukia kisha kuwacharaza viboko
wote huku nao wakisisitiza hawatoki mpamka ‘kieleweke’.
Padri na wananchi wakiwa makaburini.
Baadhi ya
wajukuu walioonja joto la jiwe ya kuchapwa viboko ni Andrea Mabula,
Sabina Bukuru, Johari Bukuru, Asha Bukuru, Faida Bukuru, Yuves Petro,
Semeni na kiongozi wao, Enos Ntilaga.
Kitendo
cha wajukuu hao kuendelea kugoma kutoka kaburini kilimchefua Padri
Nicodemus Mayalla ambaye pia ni Paroko wa Parokia ya Yesu Kristo Mfalme,
Sengerema ambaye aliamua kuondoka eneo la maziko huku akiwataarifu
polisi kuhusiana na vurugu hizo.
Kufuatia
hali hiyo, mmoja wa waombolezaji alizama mfukoni na kutoa kiasi hicho
cha pesa na kuwapa ndipo walipokubali kutoka dani ya kaburi hilo ili
mazishi yaendelee.
Ili
kuonesha alikerwa na kitendo hicho, Padri Mayalla ambaye kwa wakati huo
alikuwa amewekwa chini na baadhi ya ndugu wakimsihi kutosusia mazishi
hayo, aligoma kurejea kaburini kuongoza ibada ya mazishi.
Jeneza lenye mwili wa bibi huyo likishushwa kaburini.
Baada ya
vuta nikuvute, hatimaye Padri Mayalla alikubali kuendelea na ibada
lakini aliwataka wajukuu hao kurudisha pesa waliyochukua na kuwaomba
radhi wana mtaa huo na ndipo yeye aweze kurudi kaburini.
Wajukuu
hao waliitwa mbele ya padri huyo na mbele ya wana mtaa, wakaomba
samahani ikiwa ni pamoja na kurudisha kitita hicho cha pesa paroko huyo
naye akarejea kaburini na kuongoza ibada ya mazishi.
Hata
hivyo, wakati ibada ikiendelea polisi zaidi ya wanne kutoka Kituo cha
Polisi Sengerema wakiwa na bunduki aina ya Sub Machine Gun (SMG) na
mabomu ya machozi walifika eneo la tukio ili kuhakikisha amani na
utulivu vinatawala.
Polisi akiwa eneo la tukio.
Cha
kushangaza, saa baada ya kutoka makaburini, wajukuu hao waliwahi
nyumbani kwa marehemu, Mtaa wa Mlimani, Kata ya Nyatukala wilayani
Sengerema na kuanzisha timbwili jingine kwa kuficha chakula na vyombo
vya kupakulia wakidai warudishiwe pesa yao waliyoirejesha makaburini kwa
shinikizo la baba paroko.
Baada ya
timbwili hilo kukolea, mmoja wa wafiwa alizama mfukoni na kutoa shilingi
laki moja na kuwakabidhi wajukuu hao ambao walirudisha chakula jikoni
na taratibu za waombolezaji kupata chakula ziliendelea.
No comments:
Post a Comment