Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Wednesday, December 31, 2014

Azimio kuhusu Palestina lakataliwa

Kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa limekataa azimio lililoandaliwa na Palestina ambalo limewasilishwa na Jordan linalopendekeza kusitishwa kwa mpango wa Israel wa kuyakalia maeneo ya Palestina kwa miaka miaka mitatu.
Jordan iliwasilisha azimio hilo baada ya kukubaliwa na nchi 22 za kiarabu ikiwemo mamlaka ya Palestina.
Kura tisa zilihitajika ili kupitisha azimio hilo lakini azimio hilo lilipigiwa kura nane pekee.
Nchi mbili zilipiga kura ya hapana kupinga azimio hilo ambazo ni Australia na Marekani zilizokataa mpango huo wa mwisho na kusema hautasaidia katika masuala ya usalama wa Israel.
Nchi tano hazikupiga kura ambazo ni Uingereza, Lithuania, Nigeria, Jamuhuri ya Korea na Rwanda, huku Urusi, China, Ufaransa, Argentina, Chad, Chile, Jordan na Luxembourg zikilipigia kura ya ndio azimio hilo

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG