KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA MBUZI NA KONDOO
1.. Utangulizi
Mbuzi na kondoo wanaweza kufugwa kwa gharama nafuu nakuishi katika mazingira magumu kama ya maradhi na ukame ikilinganishwa na ng’ombe. Kutokana na umbile lao dogowanaweza kufugwa katika eneo dogo na pia wanaweza kuhudumiwa na familia yenye nguvukazi na kipato kidogo. Uzaowa muda mfupi unamwezesha mfugaji kupata mbuzi/kondoo wengikwa kipindi kifupi. Wanyama hao hufugwa kwa ajili ya nyama, maziwa, ngozi, sufu na mazao mengine kwa matumizi ya familia nakuongeza kipato. Ufugaji bora wa mbuzi na kondoo uzingatie kanuni zifuatazo:-
i) Wafugwe kwenye banda au zizi bora,
ii) Wachaguliwe kutokana na sifa za koo/aina na lengo la uzalishaji
(nyama, maziwa au sufu),
iii) Wapatiwe lishe sahihi kulingana na umri na mahitaji ya mwili,
iv) Kuzingatia mbinu za kudhibiti magonjwa kama inavyoshauriwa na mtaalam wa mifugo,
v) Kuweka na kutunza kumbukumbu sahihi za uzalishaji; na
vi) Kuzalisha nyama, maziwa au sufu yenye ubora unaokidhi mahitaji ya soko
2. Zizi au Banda la Mbuzi/Kondoo
Mbuzi/kondoo wanaweza kufugwa katika mifumo ya huria, shadidi na kwa kutumia njia zote mbili. Zizi hutumikakatika mfumo huria ambapo mbuzi/kondoo

• Lililo imara linaloweza kumkinga mbuzi/kondoo dhidi ya wanyama hatari na wezi,
• Lililojengwa mahali pa mwinuko pasiporuhusu maji kutuama,
• Ukubwa wa zizi uzingatie idadi na umri wa mifugo. Ni vema mbuzi/kondoo watengwe kulingana na umriwao; na
• Liruhusu usafi kufanyika kwa urahisi.
Pale ambapo mbuzi/kondoo wanafugwa kwa mfumo wa shadidi hufugwa katika banda wakati wote. Bandabora la mbuzi/kondoo linatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:-
• Imara, lenye uwezo wa kuwahifadhi kiafya na pia dhidi ya hali ya hewa hatarishi kwa mfano jua kali,upepo, baridi na mvua pamoja na wanyama hatari,
• Lenye mwanga, hewa na nafasi ya kutosha inayoruhusu usafi kufanyika kwa urahisi,
• Lijengwe sehemu isiyoruhusu maji kutuama na liwe mbali kidogo na nyumba ya kuishi watu. Pia ujenziuzingatie mwelekeo wa upepo ili hewa kutoka bandani isiende kwenye makazi,
• Liwe na sakafu ya kichanja chenye urefu wa mita 1 kutoka ardhini (Kwa banda la mbuzi),
• Liwe na sehemu ya kuwekea chakula, maji na mahali pa kuweka jiwe la chumvichumvi; na
• Liwe na vyumba tofauti kwa ajili ya majike na vitoto, mbuzi/kondoo wanaokua, wanaonenepeshwana wanaougua.
3. Vifaa vya Kujengea na Vipimo vya Banda
Inashauriwa banda la mbuzi/kondoo lijengwe kwa kutumia vifaa vinavyopatikana kwa urahisi katika eneo husika. Ukubwa wa banda utategemea idadi ya

Jedwali Na 1: Eneo la mbuzi/kondoo linalotakiwa
Kundi la Mbuzi/Kondoo Eneo kwa Mnyama Mmoja
(Mita2)
Vitoto 0.3
Wasio na mimba 1.5
Wenye mimba 1.9
Dume 2.8
• Paa lijengwe kwa kutumia vifaa kama miti, mbao, na kuezekwa kwa nyasi, makuti, majani ya migomba, mabati au hata vigae kwa kutegemea uwezo wa mfugaji,
• Kuta zijengwe kwa kutumia mabanzi, mbao, nguzo, wavu wa waya, fito na matofali. Kuta ziwe imarazinazoruhusu hewa na mwanga wa kutosha. Mlango uwe na ukubwa wa sentimita 60 x 150,
• Sakafu inaweza kuwa ya udongo au zege. Sakafu ya kichanja inaweza kujengwa kwa kutumia miti,fito, mianzi, mbao au mabanzi na iweze kuruhusu kinyesi na mkojo kupita. Chumba cha majike navitoto kiwe na nafasi ya sentimita 1.25 kati ya papi na papi, fito na fito au mti hadi mti. Chumba chambuzi/kondoo wakubwa iwe sentimita 1.9 kati ya mbao na mbao.
4. Uchaguzi wa Mbuzi/Kondoo wa Kufuga
Madhumuni ya kuchagua mbuzi au kondoo wa kufuga ni kuboresha uzalishaji na kuendeleza kizazi bora. Kunaaina nyingi za mbuzi/kondoo wanaoweza kufugwa kulingana na mazingira na mahitaji ya mfugaji. Uchaguzihufanyika kwa kuangalia umbile, uzalishaji na kumbukumbu za wazazi kama vile umbo kubwa, ukuaji waharaka, uwezo wa kutunza vitoto na kutoa maziwa mengi.
Mbuzi wanaofaa kwa ajili ya maziwa ni aina ya Saanen, Norwegian na Toggenburg pamoja na chotara wao.

Aidha, kondoo aina ya Black Head Perrsian (BHP), Masai na Red Suffalk Hampshire wanafaa kufugwa kwa ajili yanyama. Merino na Lincoln hufugwa kwa ajili ya sufu, wakati Corriedale na Romney hufugwa kwa ajili ya nyama nasufu. Hapa Tanzania kondoo wanaopatikana kwa wingi ni Black Headed Persian, Masai Red Dopper na kondoowengine wa asili.
Mbuzi/kondoo jike wanaofaa kwa ajili ya kuzalisha maziwa na nyama wawe na sifa zifuatazo:-
• Historia ya kukua upesi, kuzaa (ikiwezekana mapacha) na kutunza vitoto vizuri,
• Umbo la mstatili linaloashiria utoaji wa nyama nyingi; na
• Asiwe na ulemavu wa aina yoyote
Sifa za Ziada kwa Mbuzi wa Maziwa
• Awe na miguu ya nyuma iliyo imara na iliyonyooka na yenye nafasi kwa ajili ya kiwele; na
• Awe na kiwele kikubwa na chuchu ndefu zilizokaa vizuri
Sifa za Dume
Dume bora awe na sifa zifuatazo:-
• Miguu iliyonyooka, imara na yenye nguvu,
• Asiwe na ulemavu wa aina yoyote,
• Mwenye uwezo na nguvu ya kupanda; na
• Mwenye kokwa mbili zilizo kaa vizuri na zinazolingana
Angalizo: Dume lichaguliwe kwa makini kwa sababu “dume ni nusu ya kundi”.

5. Utunzaji wa Vitoto vya Mbuzi/Kondoo
Utunzaji huanza mara tu baada ya kuzaliwa. Mfugaji ahakikishe:-
• Kitoto cha mbuzi/kondoo kinapata maziwa ya mwanzo (dang’a) ndani ya masaa 24 tangu kuzaliwa nakwa muda wa siku 3,
• Kama kinanyweshwa maziwa, kipewe lita 0.7- 0.9 kwa siku. Maziwa haya, ni muhimu kwani yana viinilishena kinga dhidi ya magonjwa,
• Iwapo mama hatoi maziwa au amekufa, inashauriwa kutengeneza dang’a mbadala au kama kunambuzi/kondoo mwingine aliyezaa anaweza kusaidia kukinyonyesha kitoto hicho,
• Kitoto cha mbuzi/kondoo kiendelee kunyonya kwa wiki 12 - 16. Wiki 2 baada ya kuzaliwa, pamoja namaziwa, kianze kupewa vyakula vingine kama nyasi laini na chakula cha ziada ili kusaidia kukua kwatumbo. Aidha, kipewe maji wakati wote,
• Vyombo vinavyotumika kulishia vinakuwa safi muda wote,
• Kitoto cha mbuzi/kondoo kiachishwe kunyonya kikiwa na umri wa miezi 3 hadi
4 kutegemea afya yake; na
• Vitoto vipatiwe kinga na tiba ya magonjwa kulingana na ushauri wa mtaalam wa mifugo.
6. Matunzo Mengine
Utambuzi
Mbuzi huwekewa alama ili atambulike kwa urahisi na kuwezesha utunzaji wa kumbukumbu zake. Shughuli hiihufanyika kwa mbuzi/kondoo akiwa na umri wa siku 3 - 14. Njia zitumikazo ni pamoja na:
• Kuweka alama sikioni kwa kukata sehemu ndogo ya sikio,
• Kumpa jina kwa wafugaji wenye mbuzi wachache,
• Kumvisha hereni ya chuma au plastiki yenye namba kwenye sikio,
• Kumvalisha mkanda wenye namba shingoni; na

Kuondoa vishina vya pembe
Mbuzi/kondoo aondolewe vishina vya pembe akiwa na umri kati ya siku 3 hadi 14. Visipoondelewa hukua nakusababisha kuumizana na kuhitaji nafasi kubwa
kwenye banda. Kazi hii ifanywe na mtaalam wa mifugo.
Kuhasi
Vitoto vya mbuzi/kondoo ambavyo havitatumika kwa ajili ya kuendeleza kizazi vihasiwe kabla ya kufikia umri wamiezi 3. Kazi hii ifanywe na mtaalam wa mifugo.
7. Utunzaji wa Mbuzi/Kondoo wa Miezi 4 - 8
Mbuzi wa miezi 4 mpaka 8 ni wale ambao wameacha kunyonya mpaka umri wa kupandishwa kwa mara yakwanza. Mbuzi wa umri huu wana uwezo wa kula aina mbalimbali za malisho kama nyasi, mikunde, miti malishona mabaki ya mazao wakati kondoo hupendelea zaidi nyasi fupi. Wakati wa kiangazi huhitaji kupatiwa chakulacha ziada au kupewa pumba za nafaka mbalimbali, mashudu ya alizeti, pamba na dengu, majani ya mikunde yaliyokaushwa, madini na vitamini.
Katika ufugaji huria ni vema kuzingatia idadi ya mbuzi/kondoo inayoweza kuchungwa katika eneo, ainana hali ya malisho.
Ili mbuzi/kondoo aweze kukua na kufikia uzito wa kuchinjwa/kupevuka mapema, mfugaji anapaswa kufuatakanuni za ufugaji bora zifuatazo:-
• Kumpatia vyakula vya ziada kwa muda wa miezi 2 mfululizo kiasi cha kilo 0.2 –0.7 kwa siku kuanziaanapoachishwa kunyonya,
• Kumpatia dawa ya kuzuia minyoo kila baada ya miezi 3 na kutoa kinga za magonjwa mengine kamaitakavyoshauriwa na mtaalam wa mifugo,

• Kukata kwato mara zinapokuwa ndefu; na
• Kuhasi madume yasiyotumika kuzalisha.
8. Umri wa Kupandisha Mbuzi/Kondoo
Mbuzi/kondoo wakitunzwa vizuri wanaweza kupandishwa wakiwa na umri wa
miezi 8 hadi 12 kwa mbuzi/kondoo walioboreshwa na miezi 18 hadi 24 kwa mbuzi wa asili kutegemea afya yake.Hata hivyo, inashauriwa wapandishwe wanapofikia uzito wa kilo 12 au zaidi na wasipandishwe mbuzi/kondoo waukoo mmoja.
Dalili za joto
Mfugaji anashauriwa asimpandishe jike kabla hajafikisha umri wa kupandwa wa miezi 8 hadi 12 kwambuzi/kondoo walioboreshwa na miezi 18 hadi 24 kwa mbuzi wa asili hata kama ataonyesha dalili ya kuhitajidume. Mbuzi/kondoo aliyezaa anaweza kupandishwa siku 30-60 baada ya kuzaa. Mbuzi/kondoo aliyeko kwenyejoto huonyesha dalili zifuatazo:-
• Hutingisha/huchezesha mkia,
• Hupanda na kukubali kupandwa na wengine,
• Hutoa ute mweupe ukeni,
• Huhangaika mara kwa mara na kupiga kelele,
• Hufuata madume,
• Hamu ya kula hupungua,
• Hukojoa mara kwa mara,
• Uke huvimba na huwa mwekundu kuliko ilivyo kawaida; na
• Kwa mbuzi anayekamuliwa hupunguza kiwango cha maziwa
Mbuzi/kondoo apelekwe kwa dume mara tu dalili za joto zinapoonekana kwani joto hudumu kwa wastani wasiku 2 (saa 48). Chunguza tena dalili za joto baada ya siku 19 hadi 21 na kama dalili hazitaonekana tena kunauwezekano mkubwa

9. Utunzaji wa Mbuzi/Kondoo Mwenye Mimba
Kwa kawaida mbuzi/kondoo hubeba mimba kwa muda wa miezi 5. Utunzaji wa mbuzi/kondoo mwenye mimbani muhimu kwani ndiyo chanzo cha kupata vitoto vyenye afya bora. Mfugaji anashauriwa kufuata kanunizifuatazo:
• Apatiwe vyakula vya ziada kilo 0.2 – 0.7 kwa siku ili kutosheleza mahitaji yake na kitoto kinachokuatumboni,
• Apatiwe nyasi, miti malisho na mikunde mchanganyiko kilo 1.8 – 2.5 kwa siku.
Dalili za Mbuzi/Kondoo Anayekaribia Kuzaa
• Huhangaika kwa kulala na kuamka mara kwa mara,
• Sehemu ya nje ya uke hulegea,
• Hujitenga na kundi na hutafuta sehemu kavu na yenye kivuli,
• Hupiga kelele; na
• Hutokwa na ute mzito ukeni.
Mfugaji akiona dalili hizi anashauriwa asimruhusu mbuzi/kondoo kwenda machungani, bali amtenge kwenyechumba maalum, ampatie maji ya kutosha na kumuandalia sehemu ya kuzalia.
10. Utunzaji wa Mbuzi/Kondoo Anayenyonyesha
Mbuzi/kondoo anayenyonyesha huhitaji chakula kingi zaidi ili kukidhi mahitaji ya mwili na kuzalisha maziwa kwaajili ya kitoto/vitoto. Pamoja na nyasi, mikunde na majani ya miti malisho kilo 1.8 – 2.5 kwa siku ni muhimuapewe chakula cha nyongeza kilo 0.3 – 0.8 kwa kila lita ya maziwa inayoongezeka baada ya lita 2 na maji safi,salama na ya kutosha wakati wote.
Taratibu za Kuzingatia Katika Ukamuaji wa Mbuzi wa Maziwa

• Sehemu ya kukamulia iwe safi na yenye utulivu,
• Mbuzi/kondoo awe na afya nzuri, msafi, na kiwele kioshwe kwa maji safi ya uvuguvugu,
• Mkamuaji asibadilishwe badilishwe awe msafi, mwenye kucha fupi na asiwe na magonjwa ya kuambukiza,
• Vyombo vya kukamulia viwe safi; na
• Maziwa ya mwanzo kutoka kila chuchu yakamuliwe kwenye chombo maalum (strip cup) ilikuchunguza ugonjwa wa kiwele.
11. Utunzaji wa Dume Bora la Mbegu
Dume bora la mbegu ni muhimu litunzwe ili liwe na uwezo wa kutoa mbegu bora, kupanda na kuzalisha. Dumebora huanza kupanda akiwa na umri kati ya miezi.8 -
10 kwa mbuzi walioboreshwa. Katika msimu wa kupandisha dume moja liruhusiwe kupanda majike 40 hadi 50.Aidha, inashauriwa madume wenye umri wa miezi 8 –
9 waruhusiwe kupanda majike ambao ndio mara ya kwanza kupandwa.
Dume apatiwe:-
• Malisho ya kutosha na vyakula vya ziada kiasi kisichopungua kilo 0.2 – 0.7 kwa siku na maji ya kutosha,
• Majani ya miti malisho, mikunde na nyasi mchanganyiko na mabaki ya mazao; na
• Kilo 0.45 hadi 0.9 za chakula cha ziada za nyongeza kwa siku kulingana na uzito wake na wingi wamajike anayopanda.wiki 2 kabla na baada ya kuanza kupanda.
12. Matunzo Mengine
Kukata Mkia

Kumnyoa Kondoo wa Sufu
Sufu hunyolewa wakati kondoo akiwa hai au amechinjwa. Kwa kawaida hunyolewa miezi 6 hadi mwaka 1ambapo sufu huwa imefikia urefu wa sentimita
15 – 20. Vifaa vinavyotumika ni pamoja na mikasi au visu maalum. Uangalifu unahitajika wakati wa kunyoa ilingozi ya kondoo isiharibike. Unyoaji ufanyike wakati wa kiangazi na siyo wakati wa mvua, kondoo akiwa namimba au kipindi cha majani kutoa mbegu.
13. Udhibiti wa Magonjwa ya Mbuzi na Kondoo
Magonjwa husababishwa na vimelea jamii ya virusi, bakteria, protozoa na riketsia. Magonjwa menginehusababishwa na upungufu wa viinilishe, vitamini na protini. Dalili za mbuzi/kondoo mgonjwa ni pamoja na:-
Manyoya husimama,
Kuzubaa, kusinzia, kukohoa na kupiga chafya,
Kukosa hamu ya kula na kunywa maji,
Kujitenga na kundi,
Kuvimba taya la chini,
Kupumua kwa shida,
Kutokwa na machozi na makamasi,
Kuwa na upele au uvimbe kwenye sehemu ya mwili; na
Kutupa mimba.
• Hatua za haraka za kumuona mtaalamu wa mifugo zichukuliwe iwapo baadhi ya dalili hizizitaonekana,

Ugonjwa huu ni hatari sana na huenea kwa njia ya hewa na unaweza kusababisha vifo kati yaasilimia 60-100,
• Kila baada ya miezi 6 mifugo ipatiwe kinga dhidi ya ugonjwa wa miguu na midomo na magonjwa mengine kama Kimeta, bonde la ufa, kutupa mimba na chambavu (BQ) zitolewe kulingana na ushauri wa mtalaam wa mifugo,
• Kama kuna wanyama walioathirika watengwe kwenye kundi, wasisafirishwe au kuuzwa,
• Mbuzi/kondoo wapatiwe dawa ya minyoo. Vitoto vya mbuzi/kondoo vipatiwe dawa ya minyoo vinapofikiaumri wa mwezi 1. Viendelee kupatiwa dawa ya minyoo kila mwezi hadi vinapofikia miezi 5 na baada yahapo vipatiwe dawa ya minyoo kila baada ya miezi 3 - 4; na
• Zingatia usafi wa banda ili kuwakinga na ugonjwa wa kuharisha na kuharisha damu na magonjwambalimbali.
14. Utunzaji wa Kumbukumbu za Mifugo
Kuweka kumbukumbu za mifugo ni muhimu katika uzalishaji kwa ajili ya kutambua kosaafu, gharama za utunzajina faida. Pia, humsadia mfugaji kufanya maamuzi katika uendelezaji wa ufugaji wake. Mtalaamu wa mifugo piaanaweza kutumia kumbukumbu hizi ili kumsaidia mfugaji kuboresha ufugaji wake.
Kumbukumbu muhimu zinazohitajika kutunzwa ni:-
• Kumbukumbu za idadi na ukuaji wa wanyama waliopo, jinsi zao, uzito wa mbuzi/kondoo kwa kila mwezi ili kufuatilia ukuaji wake, tarehe ya kuachishwa kunyonya na idadi ya waliouzwa,
• Kumbukumbu ya uzazi zinazoonyesha tarehe ya kuzaliwa, namba yake, jinsi yake, aina (breed), namba yadume/jike, na uzito wa kuzaliwa,
• Kumbukumbu za upandishaji zinazoonyesha namba ya mbuzi/kondoo anayepandwa, tarehe ya joto naya kupandwa, namba ya dume lililotumika kupanda, tarehe ya joto la pili kama atarudia na tarehe ya kuzaa,

• Kumbukumbu za maziwa zinazoonyesha namba ya mbuzi/kondoo, tarehe ya kuzaa, kiasi cha maziwa kwasiku, na kiasi cha maziwa kwa kipindi chote cha kukamuliwa, tarehe ya kuacha kukamua na idadi ya sikualizokamuliwa,
• Kumbukumbu za mapato na matumizi zinazoonyesha mapato na matumizi, vitu vilivyouzwa au kununuliwakwa siku, kiasi cha fedha unachokuwa nacho kila wakati, kiasi cha fedha unachodai na kudaiwa.
No comments:
Post a Comment