Rais Jakaya Kikwete, ametupiwa lawama na makada wa CCM kwa kusababisha kushindwa CCM viti vingi katika uchaguzi wa Serikali za mitaa, kutokana kuchelewa kutoa maamuzi juu ya sakata la wizi wa Tsh 306 bilioni katika akaunti ya Tegeta Escrow.(MM)
Liyewahi kuwa mkuu wa wilaya mbalimbali nchini, Lapilali Ole Molloiment alisema kitendo cha Rais Kikwete kuchelewa kutoa maamuzi, katika sakata la Escrow kumechangia sana kuondoa imani ya wananchi kwa CCM."Kama Bunge letu, tayari lilitoa mapendekezo, kwanini Rais amechelewa kutoa maamuzi, hili ni tatizo ambalo limechangia CCM kushindwa,"alisema.
Alisema Watanzania wa sasa ni tofauti na zamani, wanajua vitu vingi hivyo, ni vigumu kuwaficha mambo ambayo yapo wazi na ambayo yanagusa maisha yao. "Mimi ninachoona washauri wa Rais ndio wanampotosha hili suala la Escrow, jambo hili lilitawala kampeni za Ukawa, hivyo ilipaswa kulifanyia maamuzi mapema na kuzima maneno kuwa CCM inawatetea waliohusika,"alisema. "Mimi ni Kada wa CCM, nasema tusipobadilika na kuwaondoa wachache wanaotuvuruga, tujiandae kuwa chama kikuu cha upinzani mwaka 2015,"alisema.
Kada Mwingine wa CCM, Joram Kaaya alisema, matokeo wa Uchaguzi wa Serikali za mtaa yana maana kubwa kwa uchaguzi ujao hivyo, ni muhimu kwa CCM kujipanga. "Lazima CCM tujipange haiwezekani watu wachache wavuruge chama alafu tubaki, mimi naungana na Katibu Mkuu wetu, Kinana wote waliohusika na haya mambo ya Escrow waondoke,” alisema Kaaya.
No comments:
Post a Comment