Baada ya kuingia hapa muhimbili kwenye wodi la mwaisela nimegundua kuwa nchi yetu bado tuna tatizo kubwa katika huduma ya afya.akina mama wanapata shida ya matibabu, vitanda havitoshi na baadhi ya vifaa vingine vya tiba. Nimejiuliza sana kama hawa viongozi wetu huwa wanapata muda wa kuja kutembelea sehemu kama hizi maana najua tatizo hili halipo hapa tu. Nimesikitika sana na kuona mafisadi wanaotafuna mali za serikali wakiendelea kukumbatiwa kama wafalme. Pesa hizo zingeweza kuondoa kabisa au kupunguza tatizo hilo hapa nchini. Viongozi timizeni wajibu wenu na msiwe watu wa kukaa ofisini na kusubiri ripoti zilozochakachuliwa na watendaji wenu wa chini. Msipofanya hivyo Mungu anasikia kilio cha hawa wanaopata taabu.
No comments:
Post a Comment