Mazishi ya aliyekuwa mnenguaji wa Twanga Pepeta, Aisha Madinda yaliyokuwa yafanyike Alhamis hii yameahirishwa hadi Ijumaa ili kufanyika uchunguzi wa kifo chake chenye utata.
Aisha alifariki jana na kwa mujibu wa mwanae wa kiume aitwaye Feisal, mama yake hakuwa mgonjwa.“Kimetokea tu ghafla, ni kifo ambacho sio cha kawaida ni cha utata. Serikali nayo imeamua kufanya mambo yake imeamua kuingilia kati ili tumzike tukiwa tunafahamu nini kimemfanya mpaka afariki,” Feisal ameiambia 255 ya XXL, Clouds FM.

Ameongeza kuwa mwanamke ambaye aliupeleka mwili wa Aisha hospitali anashikiliwa na polisi kwenye kituo cha Oyster Bay.(MM)
No comments:
Post a Comment