Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Sunday, January 18, 2015

ABIRIA WA BASI LA CHAMPION AFARIKI DUNIA AKIWA SAFARINI


MKAZI wa Dodoma, Ramadhan Zuber ambaye alikuwa abiria kwenye basi la Champion amefariki dunia akiwa safarini.
Akizungumza na paparazi mjini Kibaha, Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Ulrich Matei alisema kuwa Zuber (29) alikuwa akisafiri toka Dar es Salaam kwenda Dodoma.
Kamanda Matei alisema kuwa tukio hilo lilitokea Januari 16, saa 3:30 asubuhi katika kijiji cha chamakweza wilaya ya Bagamoyo ambapo alibainika kuwa ameshafariki dunia.
 
Alisema kuwa Zuber alikuwa amekaa kiti namba 3 kwenye basi hilo lenye namba za usajili T 909 BRA.
 
Chanzo cha kifo hicho bado hakijafahamika. Alisema kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye Hospitali ya Tumbi kwa ajili ya uchunguzi.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG