Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndugu Vuai Ali Vuai mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Kikobweni jimbo la Chaani mkoa wa Unguja Kaskazini akiwa katika ziara ya kukagua na kuhimiza utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 inayotekelezwa na serikali ikiwa ni pamoja kuhimiza uhai wa Chama Cha Mapinduzi mahali ambapo kimelegalega na kuongeza nguvu mahali ambapo kinatekeleza vizuri ilani ya uchaguzi, Katika ziara hiyo Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-UNGUJA KASKAZINI).Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akielekea kwenye ukubi wa Mkorea mahali ambapo mkutano wa Halmashauri kuu ya Wilaya ya Unguja Kaskazini umefanyika.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki shughuli za kupanda migomba wakati alipokitembelea kikundi cha akina mama cha Tuko Imara kinachojishughulisha na shughuli za kilimo cha Migomba, Mbogambona na Mananasi katika kijiji cha Banda Maji.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndugu Vuai Ali Vuai naye akishiriki kupanda migomba wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokitembelea kikundi hicho na kujionea shughuli zao za uzalishaji wa mazao ya kilimo.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya kilimo cha mananasi kutoka kwa Bi Mayasa Abdallah Juma Mwenyekiti wa kikundi cha Tuko Imara wakati alipokitembelea kikundi hicho.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika shughuli za kusafisha visiki katika mradi uliobuniwa na wananchi wakisaidiwa na TASAF kwa ajili ya utengenezaji wa barabara inayounganisha kijiji cha Kijini kwa Shauri Pili kwenda katika kijiji cha Kirwa.Baadhi ya wananchi wakiondoka mara baada ya kufanya kazi ya kusafisha barabara hiyo kwa pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akishiriki ujenzi wa nyumba ya madaktari katika kijiji cha Kijini Hospitali jimbo la Matemwe.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifurahia mchezo wa sarakasi uliochezwa na vijana wa Kijini Hospitali wakati alipotembelea ujenzi wa nyumba wa madaktari katika kijiji hichoBaadhi ya viongozi wa timu mbalimbali za jimbo la Nungwi wakiwa na jezi na mipira yao mara baada ya kukabidhiwa kwenye uwanja wa Tazari ambapo pia Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alishiriki katika ujenzi wa ukuta wa uwanja huo.Mwandishi wa habari kutoka kituo cha televisheni cha Star TV ambaye yuko katika ziara hiyo akishiriki kupiga Dufu katika kijiji cha Banda Maji. Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akiwahutubia wananchi wa jimbo la Nungwi katika uwanja wa Skuli mjini Nungwi.Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika mkutano huo.Baadhi ya wanahabari ambao wako katika ziara ya Katibu Mkuu huyo wakiwa kazini.Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndugu Vuai Ali Vuai akitema cheche zake mjini Nungwi.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi kwenye uwanja wa Skuli mjini Nungwi.Baadhi ya wanachama wapya wa CCM wakila kiapo mara baada ya kukabidhiwa kadi zao za uanachama wa chama hicho.Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akiwaaapisha wanachama wapya wa CCM kwenye uwanja wa Skuli mjini Nungwi.
No comments:
Post a Comment