Ndio ni kweli mna Matatizo mengi yamewasonga yakiwemo Ndoa zenu Watoto wenu,Biashara zenu,na Kadharika,Na mara nyingi nia yenu ni kufunguliwa kwenye hivyo vifungo vinavyowasumbua.Na shetani yuko karibu sana nanyi kwasababu anajua Nguvu iliyomo ndani yenu, ila wengi wenu hamjielewi.Ndio maana Mnafanyiwa vitu vingi sana kwa jina la kukombolewa na baadhi ya Watumishi kwa imani kwamba Mtapona.Na ndio maana kila huduma maombezi Mmejaa nyie na Ndio maana inakuwa rahisi sana kwenu kudhurumiwa mambo mengi kwa kujenga imani kubwa sana kwa watu kuliko BABA yenu.
Hebu tazama picha kama hii,Mumeo akikukuta unafanyiwa Maombi ya Staili hii "Atakuelewa kweli!?
Jifunzeni kumlilia MUNGU vyumbani mwenu na Mkumbusheni ahadi zake juu ya Maisha yenu na vizazi vyenu.
No comments:
Post a Comment