Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Saturday, January 17, 2015

MAMBO MAKUU YANAYOSABABISHA KUTENGANA KWA WAPENDANAO



MAMBO MAKUU YANAYOSABABISHA KUTENGANA KWA WAPENDANAO

  1. Kutofanya uchaguzi ulio sahii wa mke/mme au mchumba. Vijana wengi siku hizi hujilaumu sana 
  2.  juu ya chaguo la mwenza wake. Ukikosea mwanzo ujue utaoa na kuacha mke zaidi ya mmoja. 
  3. Pakifikia mahali unaanza kutamani wanawake/mwanaume wa nje na kumsahau wako wa ndani 
  4. ujue ni ishara kwamba hukufanya chaguo zuri ujana wako.
  5. Wazazi kutopendezwa na mke/mme. Hapa wazazi nawazungumzia wale wanaopenda kuingilia 
  6. mambo ya ndani ya watoto wao. Kuna watu wanaitwa mawifi, hawa ndio chokochoko kubwa 
  7. na mke na mme kutengana. Watatumia maneno ya uzushi na unafiki ili mradi mke au mme yule 
  8. waachane. Mwisho ndoa au uchumba unavunjika.
  9. Dini tofauti. Hili ni suala la mdahalo karibu dunia mzima. Inapotokea mme na mke wameanzisha 
  10. uchumba, na kila mtu ana dini yake, mwanzo wa penzi hakuna aneyekumbuka nini athali kwa 
  11. hapo baadaye. Muda unasonga, na kila mmoja anahitaji afunge ndoa au wazazi wafahamu, 
  12. hapa kila mmoja anaanza kukumbuka utofauti wao. Kutokana na imani kali au kutokuwa 
  13. na uelewa mwanzo, wanaamua kutengana ili kulinda maslahi ya dini au dhehebu la kila 
  14. mtu. Hii mara nyingi hutokea kama mmoja wao ni Mkristo au Muislam. Katika ndani 
  15. ya ukristo kuna misingi inayoongoza kanisa la SABATO. Hapa pia hawaruhusu muumini 
  16. kuoa au kuolewa nje ya dhehebu hili   vinginevyo anatengwa na kanisa.
  17. kutofikia kilele wakati wa tendo la ndoa. Hakuna ndoa inayoweza kudumu kama tendo 
  18. la ndoa halifanyiki. Au kama linafanyika ni kwa kulidhika mmoja na mwingine 
  19. asitosheke. Hii ni sahemu muhimu sana inayomfanya mke au mme aweze kuwa na 
  20. mahusino na mtu mwingine ili aweze kujitosheleza. Kila mmoja hupenda atosheke, 
  21. na inapotokea vinginevyo migogoro huanzia hapo na hatimae kuvunjika kwa penzi lao. 
  22. Zao la hili ni kutoroka kwa mke/mme au mchumba na kuanzisha uhusiano na mtu mwingine.
  23. Tabia ya uzinzi kupindukia. Hapa nazungumzia tabia ya umalaya ya mwanamke 
  24. au mwanaume nje ya mpenzi wake. Hawa ni watu ambao uzaliwa na genes za aina 
  25. hiyo na wamerithi kutooka kwa wazazi. Hivyo kwa mtu aliyorithi inakuwa ni rahisi 
  26. zaidi kutoka nje ya ndoa yake na kwenda kufuata wengine ili mradi atimize malengo 
  27. yake. NB. Tumetoa njia za kutatua hili katika kitabu hiki.
  28. Maneno au mawasiliano. Namna mke na mme wanavyozidisha mawasiliano, ndivyo 
  29. wanovyoongeza penzi lao. Kwa zamani barua zilikuwa ndio chombo cha mawasiliano kama 
  30. mmoja wao aliishi mbali. Lakini kwa sasa ni njia ya simu za mkononi. Inapotekea mawasiliano 
  31. yanapungua kati ya mme na mke kinachofuata ni kusauliana. Kila mmoja atapata wazo la 
  32. kuwa na mwingine na hatimaye kuanzisha mahusiano mapya na yule ambaye hakupenda 
  33. kuwa naye. Usipokuwa makini juu ya hili lazima mutatengana tu.
  34. Wivu. Hakuna penzi linaloweza kudumu kama hakuna wivu. Na wivu huo uwe wa kiasi 
  35. ambacho akiwezi kuathili penzi lao. Kuna watu wana wivu kupindikia. Hili ni tatizo 
  36. kubwa, na hakuna mtu anayependa afanyiwe wivu kiasi kwamba hadi mtu anakosa uhuru. 
  37. Pakifikia mahali hapa wapendanao huanza kutoa maneno ya siri kwa jirani na mwishowe 
  38. kutengana kwa 
  39. wependanao. Hapa pia inaambatana na hali ya kutokuwa na imani na mwenza wako.
  40. Kuwa na mahusiano ya hali ya juu na mtu wa jinsia tofauti pamoja na utani. Mtu 
  41. ukishaolewa, kuoa au kuwa mchumba ni bora zaidi upunguze mahusiaona ya kupindukia n
  42. a watu wa jinsia nyingine. Hali ya utani unaoambatana na kushikana, kubusiana pamoja 
  43. na kuelezana maneno ya kimapenzi kwa wale ambao si wapenzi wako husababisha 
  44. mgogoro na mwenza wako. Vinginevyo ndoa au uchumba ule utaelekea mahali pabaya 
  45. na mwisho kuvunjika kwa penzi.
  46. Kusikiliza maneno ya watu. Kuna watu hupenda kuchonganisha wanawake au wanaume
  47.  wa watu kwa maslai binafsi. Kwa kawaida watu hawa wapo kwa ajili ya kuona mnagombana. 
  48. Hivyo basi, kusikiliza kwa maneno ya hawa watu inapelekea kubadili kwa mwenendo wa 
  49. mweza na hatimaye kuwa mwisho wa penzi.
  50. Ugumba/tasa. Hii ni ile hali ya mmoja kati ya wapendanao kutokuwa na uwezo wa kuzaa. 
  51. Yaani kwa mwanaume kushindwa kutoa mbegu zinazoweza kusababisha kutungwa kwa 
  52. mamba, na kwa mwanamke kushindwa pia kutoa mayai yenye uwezo wa 
  53. kupokea mamba. Hali hii huwaathiri sana wanawake ambapo mke huonekana mzigo 
  54. mzito katika nyumba. Wangine wanafikia mahali wanawaambia wapenzi wao kuwa 
  55. wanajaza choo tu. Hii kauli lazima ipigwe vita sana. Madhara ya kauli zinazofanana 
  56. na hizo, yule mwenye kizazi huamua kumwacha yule asiye na kizazi na kwenda 
  57. kufungua kizazi kipya na mtu mwingine.

Hizo ni baadhi ya sababu za kimsingi zinazochangia uvunjifu wa ndoa au 
uchumba. Ukweli ni
 kwamba sababu zipo nyingi lakini zinazoumiza sana vichwa vya watu ni 
hizi.Hivyo kila mtu 
anapaswa kuwa makini juu ya mambo haya yaletayo mzozo katika penzi husika.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG