Mbunifu wa mavazi Kiki Zimba ametunukiwa tuzo ya kuwa mbunifu bora wa mavazi kwa mwaka huu iliyotolewa katika onesho la mavazi la Swahili Fashion 2014.
Pia Mwanamitindo wa kimataifa mtanzania aishie Marekani Millen Magese alishinda tuzo ya mtu mwenye mvuto zaidi nchini ijulikanayo kama Mercedes – Benz Style Icon of the Year iliyotolewa kwenye tuzo za Swahii Fashion 2014.
Katika kipengele hicho alikuwa akishindanishwa na akina Nasib Abdul, Diamond Platinum, Mohamed Dewji na Wema Sepetu.
Millen pia alitunukiwa tuzo ya kutambua mchango wake kama mwanadada mwenye mchango mkubwa katika kusaidia jamii yake.
Tuzo hizo zilizoandaliwa na kampuni ya 361 degree ambayo pia imeandaa onesho hilo, kulikuwa na utoaji wa tuzo nyingine mbalimbali zilizotolewa kwa wadau wa mitindo nchini kwa lengo la kutambua mchango wao katika kuendeleza fani hiyo.
Mbunifu wa mavazi Martin Kadinda alichaguliwa kuwa mbunifu bora wa mavazi ya kiume huku Jamila Nyangassa akichaguliwa kuwa mwanamke wa mwaka.
Gazeti tando (blog) ya Missie Populaar ilichaguliwa kuwa blog bora ya mwaka huku mbunifu wa mavazi Husna Tandika akitajwa kuwa ndio mbunifu bora anaechipukia.
Pia mwandishi wa habari wa kituo cha Eatv Deogratius Kithama alichaguliwa kuwa mwandishi bora wa mavazi ya kiume, na Albert Manifester alichaguliwa kuwa mpiga picha bora wa masuala ya Mitindo.
Wengine walioshinda tuzo ni pamoja na Rehema Samo alietajwa kuwa mrembaji bora wa mwaka na Irfan Rizwanali kuwa mtaalamu bora wa kuwapendezesha watu mbalimbali.
Akizungumzia ushindi wa kuwa mbunifu bora wa mavazi kwa mwaka huu, Kiki Zimba alisema kuwa ushindi huo unatokana na nia ya dhati katika tasnia hiyo hasa kwa kujituma kwa hali na mali katika kutengeneza nguo bora zaidi.
“Mwakande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Leah Kihimbi alisema kuwa serikali itaendelea kusaidia tasnia ya Mitindo nchini huku akiipongeza kampuni ya 361 degree kwa kutimiza miaka saba katika kuandaa onesho hilo la Swahili Fashion Week.
Swahili Fashion Week na Tuzo za mwaka 2014 zinaandaliwa na 361 Degrees kwa usaidizi wa Hotel Sea Cliff, Sea Cliff Court, chini ya udhamini wa EATV, East Africa Radio, Basata, Baileys, Mercedes-Benz, 2M Media, Tanzania Printers LTD and Syscorp Media. huu nimefanya kazi kubwa zaidi kwa kuwabunia watu mbalimbali hadi nimeweza kushinda tuzo hii ninaomba na watu wengine wajitokeze zaidi katika kutuunga mkono wabunifu wa ndani kwa kushona nguo kwetu”alisema Kiki.
Kwa upa
No comments:
Post a Comment