Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
(kulia)akizungumza na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Sudan ya Kusini
Mhe. Stephen Dhieu Dau Ayik aliyeleta ujumbe maalum wa Rais wa nchi hiyo
Salva Kiir kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe
Magufuli na kupokelewa na Makamu wa Rais ,Ikulu jijini Dar es Salaam
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
(kulia)akizungumza na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Sudan ya Kusini
Mhe. Stephen Dhieu Dau Ayik pamoja na ujumbe wake walioleta ujumbe
maalum wa Rais wa nchi hiyo Salva Kiir kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli na kupokelewa na Makamu wa Rais
,Ikulu jijini Dar es Salaam
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Sudan
ya Kusini Mhe. Stephen Dhieu Dau Ayik pamoja na ujumbe wake ambao
walileta ujumbe maalum wa Rais wa nchi hiyo Salva Kiir kwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli na kupokelewa
na Makamu wa Rais ,Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Sudan Kusini Salva Kiir amemtumia ujumbe maalum Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishukuru kwa jitihada za
serikali ya Tanzania za kusaidia kupatikana kwa amani katika nchi hiyo.
Ujumbe
huo wa Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir umewasilishwa nchini na Waziri
wa Biashara na Viwanda wa nchi hiyo Stephen Dhieu Dau Ayik kwa Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa niaba
ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli ikulu
jijini Dar es Salaam Tarehe 27-Jul-16.
Waziri
huyo wa Serikali ya Sudan Kusini Stephen Ayik amesema hali ya usalama
kwa sasa imeendelea kuimarika kufuatia kusitishwa kwa mapigano kati ya
wanajeshi watiifu wa Rais Salva Kiir na wanajeshi wa watiifu wa
Aliyekuwa Makamu wa Rais Riek Machar.
Akipokea
ujumbe maalum wa Serikali ya Sudan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya Rais Dkt. John
Pombe Magufuli amesema serikali ya Tanzania itaendelea kuwa mstari wa
mbele katika kuhakikisha amani inapatikana katika Taifa hilo changa
barani Afrika ambayo itawezesha wananchi wa taifa hilo kufanya kazi za
maendeleo kwa amani na utulivu.
Makamu
wa Rais Samia Suluhu Hassan pia amezitaka pande hizo MBILI
zinazohasimiana kuzingatia na kuheshimu mkataba wa amani waliosaini
jijini Arusha mwaka 2015 uliolenga kusitisha vita vya wenyewe kwa
wenyewe na kurejesha amani katika Taifa hilo.
Makamu
wa Rais amesisitiza umuhimu wa kufanyika kwa mazungumzo ya amani ya
kutafuta suluhu ya kudumu ya mgogoro huo ili kukomesha vita ambavyo
vimekuwa vikigharimu mali na maisha ya mamia ya wananchi wa Sudan
Kusini.
No comments:
Post a Comment