Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA
Showing posts with label MICHEZO. Show all posts
Showing posts with label MICHEZO. Show all posts

Monday, August 24, 2015

Kenya yashinda dhahabu mita 3,000 na 10,000

Vivian Cheruiyot
Mwanariadha wa Kenya Ezekiel Kemboi ameshinda medali ya nne mfululizo katika mashindano ya dunia mjini Bejjing baada ya kuwaongoza Wakenya wenzake kushinda nafasi za kwanza nne bora.
Awali mwanariadha wa Kenya Vivian Ceruiyot aliishindia Kenya medali nyingine ya dhahabu na baada ya kushinda mbio za mita 10,000 kwa upande wa wanawake.
Vivian alishinda medali za fedha mbio za mwaka 2003,2005,2007.
Mwanariadha wa Ethiopia Gelete Burka alichukua medali ya fedha baada ya kushindwa kumpita Cheruiyot.
Ezekiel Kemboi
Medali ya shaba ilimwendea Mmarekani Emily Infield ambaye alishinda medali hiyo baada ya kumpita Molly Huddle katika utepe.
Upande wa wanaume katika mbio za kuruka maji na viunzi mita 3000,Conseslus Kipruto alichukua fedha,Brimin Kipruto akachukua shaba huku Jairus Kipchoge Birech akichukua nafasi ya nne
Mpinzani wao raia wa marekani Evan Jagger aliona kivumbi wakati Wakenya hao walipotimka mbio.

Friday, August 7, 2015

MEMPHIS DEPAY AFANYA MAAMUZI MAGUMU NDANI YA OLD TRAFFORD


Mchezaji mpya wa Manchester United, Memphis Depay ameamua kuchukua maamuzi magumu ya kuvaa viatu vizito kwa kuomba kuvaa jezi namba 7 katika msimu huu wa ligi kuu ya Uingereza unaoanza Jumamosi hii.
Hiyo ni jezi ya heshima kwa Old Trafford ambapo iliwahi kuvaliwa na masupastaa waliochezea klabu hiyo wakiwemo George Best, Bryan Robson, Eric Cantona, David Beckham, Cristiano Ronaldo na Angel di Maria.
Hata hivyo kocha wa United, Louis van Gaal bado hajatoa namba katika kikosi chake.

Sunday, July 19, 2015

YANGA YANG’ANG’ANIWA NYUMBANI…YASHINDWA KUTAMBA MBELE YA WAKENYA


Mashabiki wa Yanga wakiwa hawana matumaini bada ya timu yao kufungwa goli la pili na timu ya Gor Mahia kwenye mchezo wa ufunguzi uwanja wa Taifa

Mashabiki wa Yanga wakiwa hawana matumaini bada ya timu yao kufungwa goli la pili na timu ya Gor Mahia kwenye mchezo wa ufunguzi uwanja wa Taifa
Yanga wameshindwa kutamba kwenye uwanja wa nyumbani baada ya kubanjuliwa na vigogo vya Kenya timu ya Gor Mahia kwenye mchezo wa ufunguzi wa michuano ya Kagame Cup uliopigwa leo jioni kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Yanga leo 4
Yanga walitangulia kupata goli dakika ya nne kipindi cha kwanza kupitia kwa mshambuliaji wao mpya Donald Ngoma walie msajili kutoka klabu ya FC Platinum ya Zimbabwe lakini bao hilo halikuweza kudumu kwani Haruna Shakava aliisawazishia Gor Mahia goli hilo dakika ya 16 ya kipindi cha kwanza na timu hizo kwenda mapumziko zikiwa sare ya kufungana goli 1-1.
Mashabiki wa Gor Mahia wakiwa wanaisapoti timu yao kwa nguvu zote
Mashabiki wa Gor Mahia wakiwa wanaisapoti timu yao kwa nguvu zote
Mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma alitolewa nje kwa kadi nyekundu kipindi cha kwanza baada ya kumpiga kwa makusudi mchezaji wa Gor Mahia.
Mwamuzi wa mchezo SsaliMashood wa Uganda akimwonyesha kadi nyekundu Donald Ngoma
Mwamuzi wa mchezo SsaliMashood wa Uganda akimwonyesha kadi nyekundu Donald Ngoma
Michael Olunga aliifungia Gor Mahia goli la pili dakika ya 45 katika kipindi cha pili na kuipa ushindi timu yake dhidi ya Yanga, mabingwa wa Tanzania bara (Yanga) walijitahidi kutafuta goli la kusawazisha lakini mambo yalikuwa magumu kwa upande wao.
Kma kawaida ya Yanga na Simba, mashabiki wa Simba wakiiunga mkono timu ya Gor Mahia
Kama kawaida ya Yanga na Simba, mashabiki wa Simba wakiiunga mkono timu ya Gor Mahia
Nadir Haroub ‘Cannavaro’ alikosa mkwaju wa penati baada ya mlinzi wa Gor Mahia kuunawa mpira kwenye eneo la hatari wakati akiwa kwenye harakati za kuokoa shambulizi lililofanywa na Yanga wakati wakilisakama lango la Gor Mahia wakitafuta goli la kusawazisha.
Msuva akichanja mbuga
Msuva akichanja mbuga
Mabadiliko yaliyofanywa na kocha wa Yanga Hans van der Pluijm kwa kuwaingiza wachezaji Kpah Sherman akichukua nafasi ya Simon Msuva, Deusi Kaseke akampisha Salumu Telela wakati Joseph Zutah akaingia kumpokea Juma Abdul lakini mabadiliko hayo hayakuzaa matunda.
Yanga leo 11

Manchester United yailaza Club America

manchester United
Morgan Schneiderlin aliifungia Manchester United bao moja dakika tano baada ya kuingia huku timu hiyo ikiishinda Klabu ya Mexico Club America 1-0 huko Seattle.
Wachezaji wapya wa Manchester United akiwemo Schneiderlin,Memphis Depay na Matteo Renzi walishiriki katika mechi hiyo.
Bastian Schweinsteiger alikuwa mmoja ya wachezaji 11walioingia katika kipindi cha pili.
Bao la Schneiderlin lilikuwa muhimu sana katika kuipatia ushindi Manchester United,baada ya kiungo huyo aliyesajiliwa kwa pauni milioni 25 kutoka Southampton kupata krosi safi ya Juan Mata.

Arsenal wakishangilia ushindi wa Barclays Asia Trophy 2015


Klabu ya Arsenal imefanikiwa kutwaa taji la Barclays Asia Trophy kwa kuifunga klabu ya Everton kwa jumla ya magoli 3-1.
Magoli ya Arsenal yamefungwa na Theo Walcott dakika 22, Santi Cazorla dakika 58 naMesut Ozil dakika 63 wakati goli pekee la Everton lilifungwa na Ross Barkley dakika ya 76.

Mashindano ya kombe Barclays Asia Trophy yamefanyika kuanzia 15-18 July katika Uwanja wa taifa wa Singapore kwa kushirikisha timu nne ambazo ni Arsenal, Everton, Stoke City na Singapore Selection XI.
Nimekusogezea picha mtu wangu jinsi Arsenal walivyoupokea ubingwa wao.
N

Thursday, July 2, 2015

SIMBA SPORT CLUB YAANDIKA HISTORIA, WAZINDUA KADI MPYA


Afisa MtendajiMkuuwa EAG Group Imani Kajula  Rais wa Simba Sport Club Evans Aveva Pamoja na Makamu wa Rais wa Club ya Simba Geofrey Nyange ‘Kaburu Wakiwa wameshika Mfano wa Kadi ya Club Hiyo waliyoizindua  Leo.
Klabu ya Simba leo hii imeandika historia kwa kuzindua Kadi Mpya za Wanachama ambazo zinamwezesha  kila Mwanachama wa  Simba  kupata  bima  ya maisha  hadi  Tsh 250,000 ikiwa atafiwa  na  mwenza au mtoto au yeye  mwenyewe  kupitia  bima  ya  maisha   iitwayo Simba Pamoja. Pia Simba  leo hii imezindua  Kadi za watoto yaani Simba Cubs. 

Rais wa Simba Sport Club Evans Aveva Akimkabidhi Mtoto  Iqram Ally Kadi ya Simba Cubs waliyoizindua leo wanaoshuhudia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa EAG Group Imani Kajula (kulia) Pamoja na Makamu wa Rais wa Club ya Simba Geofrey Nyange
Akizungumza wakati wa uzinduzi Rais wa Simba Evans Aveva alisema ‘’Simba inaendeleza falsafa yetu ya utendajii  kifanya kazi ‘’maneno machache vitendo vingi’’, baada ya kuboresha upatikanaji wa taarifa kupitia mtandao kwa kuzindua tovuti yenye taarifa na huduma mbalimbali ndani yake, leo tumewaita  hapa  kuandika historia mpya kwa wana Simba na hususani wale wanaota ka kuwa wanachama wa Simba’’.
Aliongeza  kusema ‘’ Simba inapenda kuwajulisha kuwa sasa mpenzi wa Simba anayetaka kuwa mwanachama anaweza kuomba kupata kadi ya wanachama kupitia tovuti ya Simba yaani www.Simbasports.co.tz . Napenda mtambue hii ni historia katika  ukanda huu kuweza kutumia  teknojia kufikia wanachama, Sisi  ni wakisa  sana  tunaona  mbele!.
AfisaMtendajiMkuuwa EAG Group Imani Kajula (Kulia) Akielezea Jambo  Akiwa Ameambatana na Rais wa Simba Sport Club Evans Aveva (katikati) Wakati wa Uzinduzi wa Kadi Hiyo ya Simba Sport  Club Pamoja na Makamu wa Rais wa Club ya Simba Geofrey Nyange ‘Kaburu
Kwa  upande wake Afisa Mtendaji  Mkuu  wa EAG Group ambao ni washauri watekelezaji wa mikakati  ya masoko na  biashara Imani  Kajula  alisema
‘’ Uanzishwaji  wa  Kadi  ya  Simba Cubs itawawezesha watoto sio tukutambuliwa  kuwamemba  wa  Simba, bali  pia  kupata  punguzo   kubwa au kuingia  bure  kwenye  matukio  yanayo  andaliwa  na  Simba Sports Club. Pia  maduka  mbalimbali  yatatoa  punguzo  kwa  watoto  wenye  Simba Cub Card.
Wote  mna  jua fika  kuwa  mapenzi   hujengwa, Simb  aina lenga kujenga msingi  imara  wa kuendeleza  wanachama  na  wapenzi wake’’.

Friday, June 12, 2015

Camara awa kivutio Yanga

Lansana Camara(asiye na jezi-wa pili kulia) akiwa mazoezini
Kiungo Lansana Camara kutoka Sierra Leone amesema anafurahia mazoezi katika klabu ya Yanga na ana imani mabingwa hao wa Tanzania Bara watamsajili kwa ajili ya msimu ujao.
Lansana, ambaye alikuwa akiitumia klabu ya Umea FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Sweden, alikutana na kocha mkuu wa Yanga, Hans Pluijm na kufanya naye mazungumzo kuelekea ndoto yake ya kutua katika klabu hiyo.
“ Nina furahia mazoezi yangu na mashabiki wengi wanakuja kutuangalia, hii inatia moyo”, amesema Camara, amambaye anafanya mazoezi na timu hiyo kwa sasa.
Yanga imeanza mazoezi Jumatatu wiki hii katika viwanja vya kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi kuu Tanzania Bara.
Mashabiki wengi na makocha wa Yanga, Mdachi Hans Pluijm na msaidizi wake, Charles Boniface Mkwasa wanaonekana kuvutiwa na mchezaji huyo mwenye umbo la kuvutia kisoka na wana imani ataisaidia timu hiyo endapo ataonekana anafaa.

Interpol yakata ushirikiano na FIFA

Polisi wa kimataifa wavunja uhusiano wao na FIFA
Shirika la polisi wa kimataifa Interpol limesema linasimamisha uhusiano wake na FIFA uliokuwa na lengo la kuchunguza na kukabiliana na visa vya upangwaji wa matokeo ya mechi za kandanda, kutokana na kashfa ya rushwa inayolizonga shirikisho hilo la soka duniani.
Miaka minne iliyopita FIFA iliipa interpol dolla millioni 22 kufadhili mradi ulio na lengo la kuendeleza maadili katika secta ya michezo.
Interpol inasema washirika wake wote ni sharti wadumishe na kuendeleze maadili na taratibu zinazotumiwa na interpol katika utendaji kazi wake.
FIFA imesema imesikitishwa na uamuzi huo wa Interpol na kuongeza kuwa mradi huo wa mikakati ya kuzua udandanyifu katika soka hauhusiani kwa vyovyote vile na kashfa ya madai ya rushwa dhidi ya FIFA.

Ombi la kumnunua Sterling lakataliwa

Raheem Sterling
Liverpool imekataa ombi la kitita cha pauni milioni 25 na nyongeza ya pauni milioni 5 kutoka kwa Manchester City ili kumnunua Raheem Sterling.
Pia inaaminika kwamba Liverpool inamthamini mchezaji huyo wa miaka 20 kuwa na thamani ya pauni milioni 50 na kwamba haina mpango wa kumuuza .
mancity
Mchezaji huyo amehusishwa na mzozo katika uwanja wa Anfield na hivi majuzi alisema kuwa hatoweka sahihi ya mkataba mwengine katika klabu hiyo.
Hatahivyo ajenti wa Sterling Aidy Ward amedaiwa kusema kwamba hatokubali kandarasi nyengine katika klabu ya Liverpool hata akipewa kandarasi ya pauni laki tisa kwa wiki.

Friday, June 5, 2015

BARCELONA NA JUVENTUS WATUA BERLIN SALAMA

BARCELONA NA JUVENTUS WATUA BERLIN SALAMA

Ligi ya Mabingwa barani Ulaya msimu wa 2014/2015 inafikia tamati Jumamosi hii kwa pambano la fainali baina ya Barcelona ambao ni mabingwa wa Spain watakaomenyanana Juventus ambao ni mabingwa wa Italia pambano litakalopigwa katika dimba Olmpico jijini Berlin Ujerumani.
Timu zote mbili hizi zinatafuta ubingwa wa tatu msimu huu kukamilisha makombe matatu (treble) katika msimu mmoja.
Katika picha hapa chini Wachezaji wa timu hizo wakiwasili Ujerumani
Kikosi cha Barcelona wakiongozwa na Messi
Neymar akiondoka uwanja wa ndege 

Kipa wa Juventus Buffon akiwapungia mashabiki hotelini
Carlos Tevez wa Juventus
Massimiliano Allegri kocha wa Juventus akiwasili
Mabus yakasubiri wachezaji wa Barca na Juve uwanja wa ndege wa Berlin



Artudo Vidal na Pirlo wakiwasili hotelini
Kiungo wa Barcelona Rakitic na kipa Marc-Andre Stegen
Neymar na Danny Alves


Estadio Olimpico mahali ambapo pambano hilo litapigwa

Saturday, May 30, 2015

Andy Murray asonga mbele French Open

Andy Murray asonga mbele mashindano ya French Open
Muingereza Andy Murray amezidi kusonga mbele katika mashindano ya French Open baada ya kutinga mzunguko wa tatu kwenye mashindano hayo pale alipomshinda Joao Sousa raia wa Ureno, kwa jumla ya set 6-2 4-6 6-4 6-1. Murry alianza mpambano huo akiwa vizuri na alibaki hivyo hadi mwisho, japo alionesha kupatwa na mshangao kutokana na ushindani mkali aliokutana nao kutoka kwa mpinzani wake huyo. Sasa Murray anataraji kuvaana na Nick Kyrgios kutoka Australia. "nilifurahi sana namna nilivyobadili mchezo na kuweza kufanya marekebisho pale uwanjani, ambapo upepo mzuri ukahamia kwangu" alisema Murray. Naye Muingereza mwingine Heather Watson, amegaragazwa na Mmarekani Sloane Stephens kwa set 6-2 6-4, huku Rafael Nadal na Novak Djokovic wakifanikiwa kusonga mbele kwenye hatua hiyo ya tatu.

Johnson Thompson apania kushinda

Mashabiki wa riadha nchini China
Mwanadada raia wa Uingereza Katarina Johnson-Thompson, amesema atajisikia vibaya kama hata nyakua medali yake ya kwanza ya dunia.
Thompson anashiriki a mashindano yanayotaraji kufanyika Beijing China mwaka huu. Nyota ya Muingereza ilianza kung'aa zaidi mwezi March mwaka huu pale aliponyakua medali ya dhahabu katika mashindano ya ndani ya Ulaya.
Lakini kwa sasa anasema kiu yake ni kushinda mashindano hayo hali anayosema itakuwa imetimiza ndoto yake.

Blatter azungumzia kashfa ya rushwa,Fifa

Askari wakiwakamata baadhi ya viongozi wa Fifa wanaotuhumiwa kwa rushwa
Rais wa FIFA Sepp Blatter ameibuka na kuzungumzia kashafa ya rushwa ndani ya shirikisho hilo kwa kusema wale wao watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo hawana tena ndani ya shirikisho hilo la Soka Duniani.
Maoni yake yamekuja,huku idara ya sheria ya Marekani ikisema kuwa kushikiliwa kwa baadhi ya viongozi hao wa Fifa kunafuatia matokeo ya uchunguzi wa miaka 20 ya mienendo ya rushwa ndani ya shirikisho hilo..
Hata hivyo kwa mjibu wa uchunguzi wa vitendo hivyo vya rushwa ndani ya Fifa umebainisha kuwa viongozi hao wanatuhumiwa kuhusishwa na rushwa ya kiasi cha dola million 150 ndani ya kipindi cha miaka 20.
Awali idara ya sheria ilieleza kuwa viongozi hao wa Fifa wanaotuhumiwa ni 14 wakiwemo tisa ambao wanaendelea na uongozi na wengine ni wale waliomaliza muda wao ndani ya shirikisho hilo la Fifa.
Watu wengi wamekuwa wakijiuliza ni kwa vipi Blatter amekuwa Kiongozi wa Fifa kwa muda mrefu namnahiyo , pamoja na kuwepo kwa ripoti nyingi za vitendo vya rushwa lakini ameendelea kushikilia wadhifa huo.
Wizara ya sheria ya Uswiss imesema katika tamko lake siku ya jumatano kuwa maafisa wa serikali ya Marekani waliwashuku maafisa hao kupokea rushwa ya dola milioni 100, tangu mwanzoni mwa miaka ya 1990 kwa ajili ya michuano ya Amerika ya kati.
Serikali ya Uswiss imesema itaidhinisha haraka kusafirishwa kwao.
Mwanzoni mwa mwezi huu, Blatter alisema anafahamu baadhi ya wafanyakazi wenzake wa zamani walikuwa wakichunguzwa lakini amekanusha kuwa uchunguzi huo ulimhusu pia.

Wednesday, May 20, 2015

Ramsey sasa ndio mkufunzi mkuu wa QPR

Chris Ramsey
Kilabu ya QPR imemuajiri Chris Ramsey kama mkufunzi mkuu kwa kandarasi ya miaka mitatu.
Ramsey mwenye umri wa miaka 53 alipewa kazi hiyo hadi mwisho wa mwezi Februari baada ya Harry Redknapp kujiuzulu lakini alishindwa kuizuia kilabu hiyo kusalia katika ligi kuu ya Uingereza.
''Chris alipochukua ukufunzi wa timu hii tayari tulikuwa katika matatizo makubwa'', alisema mwenyekiti wa kilabu hiyo Tony Fernandes.
wachezaji wa klabu ya QPR
Licha ya kushushwa daraja,sisi kama bodi tumefurahishwa na kazi ya Ramsey aliyofanya.
QPR imeshinda mechi tatu kati ya 14 zilizosimamiwa na Ramsey huku wakitarajiwa kucheza mechi ya mwisho dhidi ya Leicester.
TUPAMBANE BLOG