Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA
Showing posts with label MSAADA. Show all posts
Showing posts with label MSAADA. Show all posts

Tuesday, January 27, 2015

DKT.MENGI AUNGANA NA WATU WENYE ULEMAVU KWENYE CHAKULA CHA MCHANA ALICHOWAANDALIA


Watoto wenye Albinism, wakipata "msosi", wakati wa hafla ya chakula cha mchana kila mwaka inayoandaliwa na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dkt. Reginald Mengi, kwa watu wenye ulemavu. Hafla ya mwaka huu ilifanyika pale ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, siku ya Jumapili Januari 25, 2015. Kwa uchache watu 4,000 walihudhuria hafla hiyo.
MWENYEKITI Mtendaji wa IPP, Dkt. Reginald Mengi, Jumapili Januari 26, 2015, kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, aliwaalika watu wenye ulemavu kiasi cha 4,000 kwenye hafla ya kila mwaka ya chakula cha mchana.
Dkt. Mengi alishiki kula nao chakula cha mchana ikiwa ni pamoja na kuwahudumia kwa kuwagawia vyakula baadhi yao.

Kama ilivyo ada, wageni wake hao walikula, walikunywa na kucheza muziki, ambapo wasanii mbalimbali mashuhuri hapa nchini wa muziki wa kizazi kipya yaani BONGO Flava, walitumbuiza.

Jambo jipya lililojitokeza kwenye hafla ya mwka huu, Dkt. Mengi aliwatangazia “Bingo” watu wenye ulemavu kote nchini, kuwa ataanzisha shindano la wazo bora la shughulki ya kibiashara itakayomkomboa mtu mwenye ulemavu, ambapo atatenga shilingi milioni 10 kila mwezi kwa washindi kumi kujinyakulia shilingi milioni 1 kama mtaji wa kunzia shughuli iliyopendekezwa kama wazo.

Hali kadhalika, hafla ya mwaka huu imekuja na neema kwa watu wenye ulemavu wa viungo, ambapo kampuni ya Kamal Steels imeahidi kutoa miguu bandia 200 kila mwaka kuwasaidia watu wenye ulemavu wa viungo kote nchini, na kwa kuanzia kwenye hafla hiyo palitolewa miguu hiyo bandia 200.
Picha kwa hisani ya K-VIS Blog

Sunday, December 28, 2014

JOKATE MWEGELLO ATOA MSAADA KITUO CHA YATIMA CHA EXTREM CHA TANDALE

2
Miss Tanzania namba mbili 2006, mwanamitindo na mcheza filamu, Jokate Mwegello, akicheza na mmoja wa watoto wanaolelewa katika Kituo cha Yatima cha Extrem cha Tandale kwa Bi Mwamvua Jumanne, alipotembelea kuwapa zawadi ya Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya. Zawadi alizotoa ni mchele, unga wa sembe, sabuni na ndala zenye nembo za Kidoti. Picha na Jumanne Juma
7
Miss Tanzania namba mbili 2006, mwanamitindo na mcheza filamu, Jokate Mwegello, akimpa zawadi ya ndala mmoja wa watoto wanaolelewa katika Kituo cha Yatima cha Extrem cha Tandale kwa Bi Mwamvua Jumanne, alipotembelea kuwapa zawadi ya Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya. Zawadi alizotoa ni mchele, unga wa sembe, sabuni na ndala zenye nembo za Kidoti. Picha na Jumanne Juma
IMG_2647
Miss Tanzania namba mbili 2006, mwanamitindo na mcheza filamu, Jokate Mwegello, akiwa katika picha ya pamoja na watoto wanaolelewa katika Kituo cha Yatima cha Extrem cha Tandale kwa Bi Mwamvua Jumanne, alipotembelea kuwapa zawadi ya Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya. Zawadi alizotoa ni mchele, unga wa sembe, sabuni na ndala zenye nembo za Kidoti. Picha na Jumanne Juma
.....................................................................................
MISS Tanzania namba mbili 2006, mbunifu mavazi na muigizaji wa filamu za kibongo, Jokate Mwegelo 'Kidoti', jana ilitoa msaada wa vitu mbalimbali katika Kituo cha Kulea Yatima cha Extrem kilichopo Tandare kwa Bi Mtumwa, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Mrembo huyo ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya Kidoti inayojihusisha na masuala ya urembo, alitoa msaada huo kama zawadi yake ya Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya kwa watoto hao kama sehemu ya kuwafariji ili nao kujiona wako sawa na wengineo wanaioshi nawazazi wao.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo, Jokate alisema kuwa ameguswa na kituo hicho ambacho huwa hakikumbukwi na wahisani kutokana na mazingira ya eneo hilo.
"Nimefika hapa kutoa msaada kama sehemu ya kuonyesha ninavyoguswa na jamii ya watoto kama hawa, lakini pia nikiwa na lengo la kuwafariji ili nao kujiona ni sehemu ya jamii ya Watanzania," alisema.
Kidoti alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa watu wenye uwezo, kampuni na taasisi mbalimbali kuona umuhimu wa kusaidia makundi hayo maalumu katika jamii kwani nao wana haki ya kuishi na kufurahia maisha kama wengine.
Msaada aliokabidhi kwa ushirikiano na kampuni ya Raibow Shell, ni mchele, unga wa sembe, sabuni, jozi za viatu vyenye nembo za Kidoti.
Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, mlezi wa watoto hao, Mwamvua Jumanne, alitoa pongezi kwa Kidoti na kuwasihi wengine kuiga mfano wa mrembo huyo kusaidia makundi maalum.
Akielezea changamoto zilizopo katika kituo hicho, Mwamvua alisema ni kukosa uwezo wa kifedha kuwalipia ada watoto wanaosoma elimu ya msingi na sekondari, gharama za matibabu pamoja na kukosa watu wa kuwatembelea ili kuwafariji

Monday, December 22, 2014

KITUO CHA RADIO 5 WAFANYA KAMPENI YA USHINDI KWA WATOTO YATIMA

SAM_0388
Wafanyakazi wa kituo cha redio 5 Arusha wakikabidhi misaada mbalimbali katika kampeni ya “USHINDI”inayoendeshwa na kituo hicho,misaada hiyo ilitolewa na wahisani mbalimbali kwaajili ya watoto wanaoishi katika vituo vya watoto yatima Mkoani Arusha,katika Meneja  ubunifu wa Redio 5 Vicky Mwakoyo kushoto ni Sarah Keiya wakiwakabidhi watoto wa kituo cha kiwohede ndoo ya mafuta ya kupikia kwaajili ya sikukuya Krismass na mwaka mpya jijini hapa jana katika hotel ya world Garden
SAM_0393
Wafanyakazi wa kituo cha redio 5 wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wa kituo cha kiwohede na huruma katika hotel ya world Garden iliyopo moshono jijini Arusha katika tam
SAM_0390
Mkuu wa vipindi wa kituo hicho Mathew Philip akikabidhi moja ya msaada kwa shcha watoto huruma
SAM_0363
Watoto wanaoishi katika vituo vya watoto yatima wakishindana kucheza muziki
SAM_0376
Grace Joseph(12)wa kituo cha Kiwohede akionyesha ujuzi wake wa kucheza katika shindano
SAM_0400
Mtoto anayeishi katika mazingira magumu akiwa jukwaani akiimba wimbo wa “NISEME”wimbo wa Ya moto band
SAM_0358
Mashindano yakiwa yanaendelea
SAM_0361
Wafanyakazi wa Redio 5 wakiwa mzigoni
SAM_0385
Meneja  ubunifu wa Redio 5 Vicky Mwakoyo akiwa anamkabidhi zawadi ya kikombe mshindi namba moja katika shindano la kucheza muziki
SAM_0384
Meneja  ubunifu wa Redio 5 Vicky Mwakoyo akiwa anamkabidhi zawadi ya kikombe mshindi namba mbili baada ya kushinda katika shindano la kucheza muziki
SAM_0364
SAM_0346
Wafanyakazi wa redio5 wakiwa wanaanda sausage kwaajili ya watoto yatima
SAM_0352
Muonekano wa watoto wakiwa katika eneo la kuchezea michezo mbalimbali
SAM_0350
Meneja  ubunifu wa Redio 5 Bi.Vicky Mwakoyo akiwa na  Meneja masoko wa Redio 5Bi.Sarah Keiya
SAM_0366
Mtangazaji wa kituo hicho Akiba Kilango ambaye alikuwa MC wa shughuli hiyo akiwa anaongea na watoto jukwaani kabla ya mashindano ya kucheza kuanza
SAM_0371
Mtoto mwenye ulemavu wa ngozi akiwa anafatilia tamasha hilo
Kampuni Tan Communication Media  inayo miliki kituo cha  Radio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha  imeeanda tamasha kwa watoto yatima wanaoishi katika vituo lenye jina “Kampeni ya USHINDI”linalowashirikisha wadau mbalimbali wa mkoa wa Arusha
Mkurugenzi wa kituo hicho  Robert Francis anachukua jukumu la kuwasihi jamii kwa ujumla kuwa na tabia ya kuwakumbuka mayatima hasa kipindi hichi cha sikukuu ili nao wasijione kutengwa
Meneja  ubunifu wa Redio 5 Vicky Mwakoyo alisema kuwa kila mtoto anastahili kuwa na furaha na baadhi yao ni wale wenye uwezo mdogo ni vyema kuwakumbuka na tusiwatenge na tukifanya hivi watajiskia vizuri
Meneja masoko wa Redio 5 Sarah Keiya ametoa shukrani kwa wadau wote walioshirikiana na kituo hicho kwa kuwezesha kampeni hiyo kufanikiwa,wadau wakubwa walioshiriki ni Redio 5,Pepsi,Fifis bakery,Arusha meat,Skytel,Monaban,Vibration duo,Brundful company,World garden

Saturday, December 6, 2014

KITUO CHA KULELEA WATOTO YATIMA CHA AMANI ORPHANAGE CENTER CHA POKEA ZAWADI NA MSAADA KWA AJILI MAANDALIZI YA KRISMASI KUTOKA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF

Kushoto ni Meneja wa Pwani wa PSPF Msafiri
S. Mugaka  akiwa na Afisa Mahusiano wa PSPF Coleta Mnyamani
wakiwakabidhi zawadi ya Mbuzi  kwa ajilli ya Krismasi watoto wa kituo cha
kulelea yatima cha Amani Orphanage Centre tarehe 5.12.2014
 Afisa Mahusiano wa PSPF Coleta Mnyamani akimkabidhi zawadi ya vinywaji mmoja wa watoto katika kituo hicho
 Meneja wa Pwani wa PSPF Msafiri S. Mugaka akimkabidhi mmoja wa watoto msaada wa mafuta ya kupikia kwa niaba ya watoto wenzake walipo watembelea katika kituo chao huko  Zinga Bagamoyo
 Kati kati ni Mwanzilishi wa Kituo hicho cha watoto yatima na Mkurugenzi mkuu wa Kituo hicho Bi. Magreth Mwegalawa akikabidhiwa zawadi ya unga kwa ajili ya kituo cha watoto hao yatima na Mfuko wa Pensheni wa PSPF
Watoto , Walezi, pamoja na ma Afisa wa PSPF wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhi zawadi kwa watoto kwa ajili ya Sikukuu ya Krismas
Kutoka Kulia  ni Afisa wa PSPF Mhina, Afisa Ustawi wa Jamii Bagamoyo Flora Walioba ,Afisa Mahusiano wa PSPF Coleta Mnyamani, Meneja wa Mfuko wa PSPF Pwani Msafiri S. Mugaka na Afisa Ustawi wa Jamii wa Bagamoyo Rajabu Mturuya 
Watoto wa Kituo cha Amani Orphanage Centre Wakiimba wimbo wa Taifa wakati wanawakaribisha wageni kutoka Mfuko wa Pensheni wa Pspf 
Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Mkoa wa Pwani Msafiri Mugaka akizungumza na watoto katika kituo cha Kulelea watoto yatima cha Amani Orphanage Centre kilichopo Zinga Bagamoyo, Alisema kuwa Mfuko wa Pemsheni wa PSPF umeguswa sana na vituo mbalimbali vya kuwalea watoto yatima kikiwemo na cha Amani Orphanage Centre ambapo pamoja na kuwapelekea zawadi za Sikukuu ya Krismas , lakini kutokana na Kituo hicho watoto kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu watasoma watakuwa wakubwa na wakianza kazi nao watajiunga na PSPF kwa kuwa hata mtu binafsi kama anakipato tuu anaweza kujiunga na Mfuko huo. 
Afisa Mahusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Coleta Mnyamani akiongea na watoto pamoja na walezi wa Kituo cha Amani Orphanage Centre ambapo alisisitiza kuwa watoto wasijisikie vibaya kwa kuwa wengine hawana wazazi au wamekuja katika kituo hicho kwa matatizo mbalimbali na kwamba PSPF wameguswa na ndio maana wamewatembelea kuwaona pia kuwaletea msaada na zawadi mbalimbali ili nao waone kuwa wapo katika jamii moja kuwa hakuna tofauti kati ya watoto yatima na wenye wazazi.
Afisa Ustawi wa Jamii wa Bagamoyo Rajabu Mturuya   akiwakaribisha ma Afisa wa PSPF katika kituo hicho cha kulelea watoto yatima 
 Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea watoto yatima Cha Amani Orphanage Centre  Magreth Mwegalawa akisoma hotuba kwa wageni ambapo aliwashukuru kwa kuja kuwaona pia alisema kituo hicho kimesajiliwa kwa namba 000NGO/3288 na kimeanzishwa mwaka 2008 ambapo kuna jumla ya watoto 50 wakiume 19 na wakike 31.
Mlezi wa watoto wa Kituo cha Amani Orphanage Centre Bibi Titi 
Mtoto Haji Akitoa neno la Shukurani kwa Mfuko wa Penshemi wa PSPF kwa zawadi walizopewa na mfuko huo.
Watoto wakiwasikiliza kwa makini ma Afisa wa PSPF ambao hawapo pichani
Afisa Mahusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Coleta Mnyamani  akiwa anatoa zawadi kwa watoto
Julia Richard akiwa na Mtoto Getruda Shabani aliyechukuliwa na Kituo hicho akiwa na umri wa siku nne na mpaka sasa anasiku 40 mtoto huyu hana wazazi.
 Watoto wakipata Burudani 
 
Wakati Mwezi wa Kumi na Mbili Ukiwa Unaendelea Kuyoyoma Nayo Maandalizi ya Kusherehekea Sikukuu ya Kuzaliwa Kwa Mokozi yakiwa Yamepamba Moto Mfuko wa Pensheni Wa PSPF Kwakushirikiana na Ustawi wa Jamii wa Bagamoyo Wame Kabidhi Msaada wa Vitu mbalimbali Katika Kituo Cha Kulelea Watoto Yatima Cha AMANI kilichopo katika Mkoa Wa Pwani Wilaya Ya Bagamoyo Eneo la Zinga Baadhi Ya Zawadi na Msaada Ulio Tolewa ni pamoja na Mbuzi,Mchele,Unga wa sembe,Vinywaji na Mafuta ya Kula.
 
PSPF wameweza Kushiriki katika kutoa msaada Huo Ilikuweza kujenga mazingira mazuri kwa Watoto hao wanao lelewa katika vituo Mbalimbali na Kuwaweka karibu na Jamii Ili wasiweze kujihisi Katika hari ya Upweke Bali kuwa  Katika Hari Ya Furaha Hususani Katika Kipindi Hiki Cha Kusherehekea sikukuu ya Krismasi na Kuukaribisha Mwaka 
 
Akizungumza Wakati Wa Ugawaji Wa Zawadi na Msaada HuoMeneja wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Mkoa wa Pwani Msafiri Mugaka amesema Mfuko wa PSPF ni mfuko Wa Jamii Unao Ungana na Jamii Mbalimbali Bila Kubagua Matabaka Yoyote Kwani Wao Wapo Kwaajiri ya Kusaidia Jamii Hivyo Kwa Kipindi Hiki wameamua Waanze na Kituo Cha Bagamoyo lakini Sio hapo tu Bali Wataendelea na Moyo Huo Ili kuhakikisha Watoto wanapata Mahitaji Machache Japo Havita watosha ila Vitawasaidia kwa kiasi kikubwa,Vilevile Aliwaasa watoto Wa Kituo Hicho Kwa Kuwaambia Siku Zote waendelee Kumtegemea Mwenyezi Mungu Kwani Ndiye anaye wawezesha kwa Yote atawakuza na Kuweza kufanya Kazi katika Mfuko Wa Pensheni Wa PSPF
 
Naye afisa Mahusiano wa Mfuko Wa Pensheni wa PSPF Coleta Mnyamani Alikuwa na Machache Ya Kuzungumza Wakati Wa Shughuli Ya Ugawaji Wa Zawadi na Msaada Ikiendelea “Kwaniaba Ya Makao Makuu ya PSPF Tunapenda Kushiriki Kuwasaidia Watoto Mbalimbali Wanaoishi Katika Mazingira Magumu Hata Wale wasio na Wazazi Hivyo Tunatoa Zawadi na msaada Huu Ili Kuweza Kuwakuza Watoto Ki Fikra na Kuto Dhani Kuwa Wao ni wapweke” Alimaliza Kwa Kusema Tunawapenda Watotop
 Wote Na Nijukumu La kila mmoja Kuwalea Ili Waweze Kuja Kuwa tegemezi kwa Baadae  
 
Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea watoto yatima Cha Amani Orphanage Centre  Magreth Mwegalawa Ametoa Shurani zake Za Dhati Kwa Niaba Ya Kituo Kwa Mfuko Wa PSPF Nimfuko nUnao Jali Jamii Kwani Ni Watu na Mashirika Machache Yenye moyo Kama Huu Tunapenda Kusema Asanteni na Muendelee Na Moyo Huo Huo Kwani Hawa Watoto ni Jukum letu kuwatimizia Ndoto Zao Mungu Awabariki Katika kazi zote muendeleazo kuzifanya .
TUPAMBANE BLOG