Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA
Showing posts with label bank ya crdb. Show all posts
Showing posts with label bank ya crdb. Show all posts

Wednesday, December 10, 2014

CRDB YAIBUKA KIDEDEA KATIKA TUZO ZA NBAA UPANDE WA MABENKI

Naibu waziri wa fedha Adam Malima akimkabidhi meneja wa fedha
wa benki ya CRDB Sosteness Biseko
tuzo  ya NBAA ya ushindi  katika
uandaaji wa taarifa bora za fedha mwaka 2013-2014,jumla ya benki tisa
zilishiriki ambapo Benki ya CRDB iliibuka mshindi wa kwanza katika kundi la
mabenki, hafla hiyo ilifanyika juzi katika hotel ya Mount Meru jijini Arusha
*********
Mashirika binafsi ,taasisi
na idara mbalimbali za serikali zimehimizwa   kushiriki katika mashindano ya tuzo
zinazotolewa na bodi ya wahasibu  
na wakaguzi wa hesabu nchini NBAA katika
uandaaji bora wa taarifa za fedha za mwaka ili kuboresha hesabu za mashiriki
hayo na kuongeza uwazi katika shughuli za biashara za ndani ya nchi na
kimataifa 
Mwenyekiti
wa bodi ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu nchini NBAA Profesa Issaya Jairo ametoa kauli hiyo jijini Arusha wakati wa kufunga  mkutano mkuu wa mwaka wa bodi hiyo ulio enda
sambamba na utoaji wa tuzo na vyeti kwa washindi  katika uaandaaji  bora wa taarifa za fedha za mwaka ambapo kwa
mwaka 2014 jumla ya washiriki 40 walishiriki ambao waligawanywa katika makundi
11 kulingana na huduma wanayo itoa
Katika kundi
la mabenki, benki ya crdb ilibuka mshindi  wa kwanza kwa mwaka2013-2014 na kupata tuzo
maalumu ya uandaaji  wa taarifa bora  za fedha za mwaka iliyokabidhiwa na naibu
waziri wa fehda Adam Malima  kwa meneja
wa fedha wa benki hiyo Sosthenes Biseko ambaye akizungumzia ushindi huo amesema
ni njia mojawapo ya kuudhihirishia umma wa watanzania kuendelea kuwa na Imani nabenki.

Wafanyakazi mbalimbali wa benki ya CRDB wakiwa katika picha wakati wa makabidhiano hayo.

Saturday, November 15, 2014

BENKI YA CRDB YASHIRIKI KONGAMANO LA VIJANA LA BIASHARA LILILOANDALIWA NA TAASISI YA AIESEC JIJINI ARUSHA


Jumla yaVijana 150
kutoka ndani na nje ya nchi wameudhuria Kongamano la Biashara kwa Vijana
lililofanyika jijini Arusha ambapo Benki ya CRDB wakiwa ni miongoni mwa
wadhamini wa  kongamani hilo.
Kongamano hilo lilihudhuriwa na Vijana kutoka katika Vyuo Vikuu vya nchi za
Afrika Mashariki na kuandaliwa na Taasisi ya AIESEC ambalo hujihusisha na
ubunifu wa vipaji vya uongozi miongoni mwa vijana lililofanyika jijini
Arusha hivi karibuni katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Hall CDTI- TENGERU,
Arusha ambalo lilihudhuriwa na wanafunzi 150 kutoka nchi tofauti za kimataifa
na 150 kutoka vyuo vya elimu ya juu ndani ya Tanzania.
 
Benki ya CRDB kama
miongoni mwa makampuni yaliyodhamini kongamano hilo, ilialikwa kuweza kutoa
elimu juu ya “Teknolojia na Ubunifu” ambapo  Mkurugenzi wa mikakati na
ubunifu wa Benki ya CRDB, Bw. Goodluck Nkini
 aliweza kutoa elimu hiyo kwa wanafunzi
walengwa.
 
 Katika kongamano hilo washiriki walipata nafasi ya
kuelemishwa kuhusu huduma za kibenki kwa njia ya kieletroniki zilizotolewa na
Mangire Kibanda (Meneja huduma za kibenki kwa njia ya kielektroniki) ambaye
alitoa elimu kuhusu huduma za kibenki kwa njia ya simu (SimBanking), kwa njia
ya Internet (Internet Banking), mashine za mauzo (Pos), Wakala wa Benki
(FahariHuduma).
Mkurugenzi wa Mikakati na Ubunifu wa Benki ya CRDB, Bw. Goodluck Nkini akitoa mada kuhusu teknolojia  na ubunifu.
Mkurugenzi wa Mikakati na Ubunifu wa Benki ya CRDB, Bw. Goodluck Nkini akitoa mada.
Mkurugenzi wa Mikakati na Ubunifu wa Benki ya CRDB, Bw. Goodluck Nkini akijibu maswali ya wanafunzi.
Ofisa Masoko wa Benki ya CRDB, Alma Ally (kushoto) akifafanua jambo kuhusu akaunti ya Scholar ambayo ni maalumu kwa wanafunzi.
Baadhi ya wanafunzi wakipata elimu kuhusu huduma za kibenki.
Meneja wa Huduma za Kibenki za Kieletroniki, Bw. Mangire Kibanda (kulia) akitoa elimu kuhusu huduma za kibenki za kielectroniki kwa njia ya simu
(SimBanking), kwa njia ya Internet (Internet Banking), mashine za mauzo (Pos),
Wakala wa Benki (FahariHuduma) 
kwa wanafunzi waliohudhuria kongamano hilo.
Baadhi ya wanafunzi wakipata elimu kuhusu huduma za kibenki zitolewazo na Benki ya CRDB.
Wanafunzi kutoka vyuo vya nchi za Afrika Mashariki na Kati wakisikiliza mada kutoka kwa Mkurugenzi wa Mikakati na Ubunifu wa Benki ya CRDB, Bw. Goodluck Nkini (hayupo pichani).
Ofisa Rasilimali Watu wa Benki ya CRDB, Bw. Petro Kasindya (kulia), akitoa ufafanua kwa walengwa kuhusu mfumo wa Rasilimali Watu wa Benki ya CRDB. 
TUPAMBANE BLOG