Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA
Showing posts with label jeshi. Show all posts
Showing posts with label jeshi. Show all posts

Friday, March 20, 2015

NAIBU INSPEKTA JENERALI WA POLISI AFUNGA MAFUNZO YA WAKAGUZIWASAIDIZI WA JESHI LA POLISI CCP-MOSHI

Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi,DIGP, Abdulrahmani Kaniki akikagua gwaride la wakaguzi wasaidizi wa polisi wakati wa sherehe ya kufunga mafunzo ya maofisa hao katika chuo cha polisi Moshi.
Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi,DIGP, Abdulrahmani Kaniki akimvisha cheo wp 2704 ssgt Batuli kuwa mkaguzi msaidizi wa jeshila polisi wakati wa sherehe ya kufunga mafunzo ya maofisa hao katika chuo cha polisi Moshi.
Wahitimu wa kozi ya mkwaguzi msaidizi wa jeshi la polisi wakipita kutoa heshima kwa mgeni rasmi wakati wa sherehe ya kufunga mafunzo ya maofisa hao katika chuo cha polisi Moshi.
Wahitimu wa kozi ya mkwaguzi msaidizi wa jeshi la polisi wakiimba kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa sherehe ya kufunga mafunzo ya maofisa hao katika chuo cha polisi Moshi. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.

Tuesday, March 3, 2015

Majeshi ya Iraq mbioni kuikomboa Tikrit

   

Tikrit ilikuwa mji wa pili baada ya Mosul uliotekwa na Islamic State
Serikali ya Iraq inasema kuwa wanajeshi wake wameanza kampeini ya kuwafurusha wapiganaji wa Islamic State kutoka mji wa Tikrit .
Mji huo mkuu wa jimbo la kaskazini la Salahuddin ulidhibitiwa na wanamgambo wa Islamic state Juni mwaka uliopita.
Serikai inasema kuwa wanajeshi 30,000 wakiwemo wapiganaji 200 wakujitolea wa kisuni pamoja na wakurdi wanaelekea mji wa Tikrit wakisadiwa na ndege za kivita .
Mwandishi wa BBC mjini Baghadad anasema kuwa ikiwa mji wa Tikrit utatekwa na serikali itawezesha wanamgambo wa Islamic State kusukumwa kwenda maeneo ya mbali ya kaskazini hadi mji wa Mosul ambao ndio mji mkubwa
zaidi ulio mikononi mwa wanamgambo hao.
Mji wa Tikrit uko kilomita 150kmKaskazini mwa mji wa mkuu wa Baghdad.
Tikrit ilikuwa mji wa pili baada ya Mosul uliotekwa na Islamic State
Runinga ya kitaifa ya Al-Iraqiya imetangaza ripoti iliyodai kuwa wapiganaji hao wa IS walikuwa wamebumburushwa kutoka viunga vya mji wa Salahuddin nje ya Tikrit lakini habari hizo hazijathibitishwa.
Waziri mkuu Haider al-Abadi alifanya mazungumzo na koo za waSalahuddin kabla ya kutangazwa kwa operesheni hii kubwa zaidi kuwahi kufanyika.
Hata hivyo hii si mara ya kwanza kwa jaribio kama hili kutokea mwaka uliopita operesheni ya kujaribu kuwang'oa IS ilitumbukia nyo'ngo huku mamia ya wapiganaji waliokuwa wakiunga serikali mkono wakiangamia mikononi mwa wapiganaji wa Islamic State.

Friday, February 27, 2015

Jeshi la China laingia Sudan Kusini

Wanajeshi wa Uchina waingia Sudan kusini kuweka amani
Uchina imesema kuwa kikosi chake kwa kwanza maalum cha kijeshi kilichojumuishwa wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa mataifa kimeanza shughuli zake nchini Sudan kusini.
Katika kipindi cha majuma machache yajayo, jumla ya wachina mia saba watawasili nchini humo .
Watakuwa na ndege zisizokua na rubani, vifaru na makombora.
Uchina haijawahi kuwatuma maelfu ya walinda amani , lakini imekuwa zaidi ikitoa misaada kwa ajili ya amani. .

Thursday, November 6, 2014

WANAJESHI WA LIBYA WAFUKUZWA UINGEREZA


Wanajeshi kutoka nchini Libya wamerejeshwa nchini kwao kutokana na kukosa uadilifu wakiwa mafunzoni Uingereza huku wengine wakituhumiwa kufanya vitendo vya ukatili wa kimapenzi.
Wanajeshi hao waliokuwa mafunzoni nchini Uingereza, 300 kati yao wamesharejeshwa Libya kutokana na tuhuma kuhusiana na unyanyasaji wa kimapenzi.
Waziri wa Ulinzi wa Libya amethibitisha kurejeshwa kwa askari hao na kuongeza kuwa wengine watarejeshwa siku chache zijazo.
wanajeshi wawili wa Libya wamekiri kufanya vitendo vya unyanyasaji wa kingono dhidi ya wanawake huko Cambridge, ambapo wawili wameshafikishwa mahakamani wakikabiliwa na mashitaka ya ubakaji.
Baadhi ya wakazi wa eneo jirani na kambi ya jeshi walipo wanajeshi hao wa Libya,wamesema kuwa wamekuwa wakiwaona wanatoka nje ya ngome za jeshi kwaajili ya kununua pombe, na tayari waziri wa ulinzi amekiri kupokea mashtaka hayo na kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya wanajeshi hao wa kigeni.
Waziri Libya amesema wanajeshi hao wanaruhusiwa kutoka nje ya kambi kwa saa tatu wiki kwani ameongeza kuwa madhara ya askari hao kuzagaa mitaani ni makubwa na wengine hujitumbukiza katika matumizi dawa za kulevya na ulevu wa kupindukia.BBC (VICTOR SIMON

Saturday, November 1, 2014

JESHI LAGAWANYIKA KUHUSU UONGOZI BURKINA FASO


  • Written by  Tupambane Blog
  • Email
  • Tuma Maoni
  • Share on facebook Share on gmail Share on twitter 

Jenerali, Honore Traore, mkuu wa majeshi ya Burkina Faso akitangaza kuchukua madaraka ya nchi.
Mgawanyiko umeripotiwa ndani ya jeshi la Burkina Faso kuhusu ni nani anayefaa kuliongoza taifa hilo kufuatia kujiuzulu kwa rais Blaise Campaore baada ya miaka 27 uongozini.
Kituo kimoja cha radio kilitangaza taarifa kutoka kwa naibu mkuu wa kikosi cha kumlinda rais kanali Isaac Zida iliyosema kuwa amechukua jukumu la kuliongoza taifa hilo.

Mkuu wa majeshi ya Burkina Faso Jenerali Honore Traore, (katikati),akitangaza kuchukua madaraka kwa waandishi wa habari. 
Mkuu wa majeshi ya Burkina Faso Jenerali Honore Traore, (kati kati),akizungumza kwenyemkutano na waandishi habari kutangaza kwamba anachukua madaraka ya nchi akiwa katika makao makuu ya jeshi mjini Ouagadougou, mji mkuu wa Burkina Faso, Oct. 31, 2014.
Mapema mkuu wa majeshi Honore Traore alitangaza kuwa alikuwa amechukua usukaniBlaise Compaore alijiuzulu baada ya kushuhudia maandamano yenye ghasia baada ya jitihada zake za kutaka kuliongoza taifa hilo kwa awamu nyengine kupitia bunge kugonga mwamba.

Aliyekuwa rais wa Burkina Faso Blaise Campaore.
Akizungumza hapo jana kanali Zida amesema kuwa Jenerali Traore hawezi kuliongoza taifa hilo.''Nimechukua jukumu la kuliongoza taifa hili na serikali ya mpito ili kuliendeleza na kuhakikisha kuwa kuna mabadiliko ya kidemokrasia kwa njia ya amani'' alisema kanali Zida katika hotuba yake katika runinga.
Chanzo: BBC
TUPAMBANE BLOG