Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA
Showing posts with label maajabu. Show all posts
Showing posts with label maajabu. Show all posts

Wednesday, February 18, 2015

HUZUNI:AUMWA NA NYOKA, ATOKWA MAGAMBA

  KWELI duniani hujafa hujaumbika! Mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la Kondo Athuman, mkazi wa Pugu Mnadani, Dar es Salaam amejikuta akiishi kwenye mazingira magumu kutokana na magamba kumtoka mwilini na kukatika vidole baada ya kumuua nyoka.  
Kondo Athuman akionyesha mguu unaotoka magamba.
CHANZO CHAKE
Akisimulia kwa huzuni, Kondo alisema mwaka 2006 alisafiri na mkewe kwenda mkoani Morogoro ambapo walipata shamba na kuendesha shughuli za kilimo cha mahindi na ufuta.
Alisema siku moja akiwa ametoka shambani alijipumzisha nyumbani kwake lakini ile anaingia ndani akamuona nyoka mkubwa na alijitahidi kumuua lakini kabla ya kumuua akakimbia, akashangaa kumuona wa pili akiingia na kufanikiwa kumuua.
ALIMUUA NYOKA, AKAMFUKIA, ASUBUHI AKAKUTA MTI
Akifafanua zaidi Kondo alisema baada ya kumuua nyoka wa  pili akiwa na mkewe waliendelea kumsaka yule wa kwanza ambaye aliingia chini ya kabati na kufanikiwa kumkata kichwa.
Baada ya kuwaua nyoka hao aliwatoa nje na kuchimba shimo kisha kuwafukia lakini cha ajabu alipoamka asubuhi na kwenda kuangalia alipowafukia, alikuta shimo likiwa wazi huku kukiwa kumepandwa mti.
KUISHIWA NGUVU NA KUTOKWA MAGAMBA
“Mara baada ya kuwaua wale nyoka nilianza kusikia baridi na kuishiwa nguvu  ambapo zilipita siku tatu nikaanza kutokwa magamba yanayofanana na wale nyoka huku nikitokwa na vidonda vikubwa mguuni na vidoleni kisha mikono ikawa inagoma kukunjuka. 

VIDOLE VIKAANZA KUKATIKA
“Niliendelea kuumwa mpaka vidole vingine vikakatika kutokana na vidonda. Kweli nateseka ambapo baada ya kuzidiwa tuliamua kurudi nyumbani Dar ambapo nilienda katika hospitali mbalimbali na kupimwa vipimo vyote ambapo nilionekana sina ugonjwa wa ukoma wala mwingine wowote.
“Nikaanza kutafuta dawa za kienyeji kwa waganga. Mganga mmoja alinieleza kwamba wale nyoka hawakuwa wa kawaida bali walitumwa na yote hayo yalitokana na wivu kwani wazee wa pale Morogoro walikasirika walipoona tunawapita kimaendeleo kwa kuwa nilikuwa na bidii ya kufanya kazi na kuvuma mavuno mengi,” alisema Kondo.

Wednesday, February 4, 2015

Mtoto wa wazazi watatu kuzaliwa Uingereza

Historia na maajabu ya mtoto wa wazazi watatu
Wabunge wa bunge la Uingereza wameunga mkono sheria inayoruhusu uzaaji wa wa watoto wenye vinasaba, DNA kutoka kwa wanawake wawili na mwaume mmoja, katika tukio la kihistoria.
Uingereza kwa sasa itakuwa nchi ya kwanza kuweka sheria zinazoruhusu watoto wenye vinasaba vya watu watatu tofauti.
Katika kura iliyopigwa katika bunge la Commons, wabunge 382 waliunga mkono muswada huo wa sheria na wabunge 128 walipinga mbinu inayozuia magonjwa ya kijenetiki kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Wakati wa mjadala huo, mawaziri wamesema mbinu hii ni "mwanga kwa safarindefu ya giza" kwa familia kupata watoto.
Upigaji kura zaidi unahitajika katika baraza la bunge la juu, maarufu kama House of Lords. Iwapo kila kitu kitakwenda sawa, basi mtoto wa kwanza wa teknolojia hii atazaliwa mwaka ujao.
Watetezi wa mpango huu wanasema uungwaji mkono wa sheria hii "ni habari njema kwa maendeleo ya tiba" lakini wakosoaji wanasema wataendelea kupinga mpango huu ambao una mashaka mengi kuhusu maadili na usalama katika uzazi huu.
Makisio yanasema watoto 150 wanaopatikana kutokana na vinasaba vya watu watatu watazaliwa kila mwaka.
Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron anasema: "Hatuzungumzii Mungu hapa, tunahakikika kuwa wazazi wawili ambao wanataka mtoto mwenye afya wanaweza kumpata."
Mpango huu ambao umebuniwa Newcastle, utasaidia wanawake kama Sharon Bernardi, kutoka Sunderland, ambaye alipoteza watoto wote saba kutokana na ugonjwa wa mitochondrial

Tuesday, February 3, 2015

MADAKTARI NA WAUGUZI WAUZA VIUNGO VYA MIILI YA WATOTO WALIOKUFA HOSPITALI KWA WAGANGA WA JADI!!


Wakati serikali ikihaha kutafuta muarobaini wa mauaji ya watu wenye ulemavu Ngozo (Albino),katika mikoa ya kanda ya ziwa,huku ikidiriki kutangaza vita dhidi ya wapiga ramli wote, katika hali isiyokuwa ya kawaida imebainika kuwa watoto ambao huzaliwa wakiwa hawajafikisha umri na kufa au kupoteza maisha wakati wa kuzaliwa viungo vyao huuzwa kwa waganga wa kienyeji katika hospitali ya wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu.
Inaelezwa kuwa akina mama wanaojifungua watoto hao na kwa bahati mbaya kupoteza maisha, viungo vya watoto hao huwa havipelekwi kuzikwa kama ilivyo kawaida na taratibu za hospitali, badala yake wauguzi na wafanyakazi wengine huchukua viungo hivyo na kupeleka kwa waganga wa jadi.Tuhuma hizo zilitolewa juzi mbele ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Mwamvua Jilumbi katika kikao cha pamoja na wadau wa afya mkoa kilichofanyika katika ukumbi wa kanisa la KKKT mjini Bariadi wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa kukomesha vifo vya wajawazito
na watoto mkoani Simiyu ulioko chini ya AMREF Tanzania.
Wadau hao walibainisha kuwa hali hiyo imekuwa ikijitokeza kila mara katika hospitali ya Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, ambapo walieleza kuwa mtandao mzima wa kuuzwa kwa viungo hivyo ufanyika kati ya wauguzi pamoja na madaktari ambao ndiyo wahusika wakuu kuzalisha akina mama wajawazito.
Mbele ya Katibu huyo tawala wa Mkoa wadau hao waliendelea kueleza kuwa viungo hivyo vimekuwa vikiuzwa kuanzia shilingi 400,000 hadi 500,000 kiasi ambacho walieleza hutolewa na waganga wa hao wa jadi.
“..katika hospitali yetu ya Bariadi kuna jambo ambalo siyo zuri na jema leo ngoja tulitoboe mbele ya kikao hiki na tena mbele za waandishi wa habari na wewe Katibu tawala wa Mkoa..akina mama wanaojifungua watoto wao kwa bahati mbaya akafariki viungo vya watoto hao huuzwa kwa waganga wa jadi” Alisema Gasper Mathew na kuongeza kuwa..
“ viungo hivyo vinauzwa shilingi 400,000 hadi 500,000 huu ni ushirikina wa hali ya juu na ni hatari..wauguzi pamoja na madaktari ndiyo wanahusika sana..wamekuwa wakipewa kiasi hicho..kila mara wanafaya hivyo lakini tumekuwa kimya” Alisema
Walisema kuwa akinamama wengi hufika hospitalini hapo kwa lengo la kujifungua na mara wanapojifungua na kwa bahati mbaya mtoto au watoto kufariki kutokana na matatizo ya afya ya uzazi baadhi huamua kuwahifadhi katika chumba cha maiti lakini wengi hujikuta wakirejea nyumbani mikono mitupu baada ya miili ya watoto wao kuuzwa kwa waganga wa kienyeji.
Akizungumzia tuhuma hizo Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu,Mwamvua
Jilumbi katika kikao hicho alimtaka Mkurugenzi wa Halmshauri ya Mji wa Bariadi Erica Mssika kutoa maelezo juu ya tuhuma hizo.
Akitoa maelezo ya tuhuma hiyo Mkurugenzi huyo alisema kuwa hana taarifa yoyote juu ya kuwepo kwa vitendo hivyo katika hospitali yake, huku akieleza kuwa watafanya uchunguzi mara moja na watakao bainika kufanya hivyo watachukuliwa sheria mara moja.
“..hii ni hatari mimi hili nimelipata hapa na nimelisikia leo sina taarifa yeyote.. ila nawaomba wadau waliotoa tuhuma hizi tushirikiane tufanye uchunguzi haraka ili tuwabaini na watakaobainika tutawachulia sheria za kinidhamu” Alisema Mssika.
Katika kikao hicho Meneja Mradi wa Shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na masula ya afya AMREF Health Africa tawi la Tanzania,katika mkoa wa Simiyu, Godfrey Matumu, aliitaka jamii ya mkoa wa Simiyu kushiriki kikamilifu katika kuthibiti vifo vya akinamama wajawazito na watoto wachanga wenye umri chini ya miaka mitano
Alisema vifo hivyo vimekuwa vikisababishwa na kuchelewa kupata huduma katika vituo vya afya kwa wakati.wakati wa kuzindua Mpango Mkakati wa Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto katika mkoa wa Simiyu utakaotekelezwa kwa muda wa miaka 4 (2014-18),chini ya msaada wa watu wa Canada.

Friday, January 23, 2015

Ajuza miaka 90: anasoma darasa la nne


Gogo akiwa darasani na wanafunzi wenziwe.
Akiwa na umri wa miaka 90 mwanamke wa Kenya ambaye anahudhuria masomo akiwa na wajukuu zake wapatao sita inaaminika ndiye mwanafunzi mzee zaidi anayesoma shule ya msingi duniani.
Akiwa ameketi dawati la mbele kabisa darasani ,yuko darasa la tano na amevalia nguo za shule , Priscilla Gogo Sitienei anamsikiliza mwalimu anayefundisha kwa makini hukua akiandika majina ya wanyama kwa kiingereza kwenye daftari lake.
Prissilla alijiunga na shule hii ya Leaders Vision Preparatory School miaka mitano iliyopita lakini pia aliwahi kuwahudumia wakaazi wa kijiji chake cha Ndalat kilichoko kwenye bonde la ufa kama mkunga miaka sitini na mitano iliyopita.
Darasani Priscilla anawasaidia wengine wafanye vyema ambao wana umri kati ya miaka 10 hadi 14 na mar azote huwaambia ujumbe wake hasa mabinti kuwa elimu ndiyo urithi wao.
Priscilla anajulikana kama Gogo maana yake bibi katika lugha ya jamii ya wakalenjini,anasefurahia masomo akiwa na umri wa miaka 90 katika umri huo anajua kuandika na kusoma pia fursa aliyoikosa alipokuwa mdogo.
Lugha ambayo Priscilla anajiona yuko huru kuitumia ni lugha mama kwake ki Kalenjin kuliko kiingereza,pindi anapotakiwa kujieleza kwanini aliamua kujiunga na shule katika umri wake.
Sababu kubwa ambayo amekuwa akiitoa,ni ajue kusoma ili amudu kusoma bibilia,lakini pia kwa umri wake anataka awahamasishe watoto kupata elimu,kwani anawaona watoto wengi wakiwa hawako shuleni na watoto hao wana watoto.
Gogo apitapo mitaani haoni shida kukabiliana na watoto ambao hawako shuleni katika muda wa masomo na kuwauliza kwanini hawako shuleni.
Gogo anasema watoto hao humjibu kwamba hawaendi shule kwakuwa umri wao ni mkubwa,name huwaambia mimi ni mkubwa sana kwenu lakini niko shuleni hivyo nanyi jiungeni na shule.
Kikubwa kinachomuumiza Gogo ni kuwaona watoto wengi waliopoteza muelekeo,wengi wao hawana baba na wanazurura hovyo mitaani,bila msaada wowote.kutokana na hali hiyo nataka kuwahamsisha waende shulen

Wednesday, January 7, 2015

Ajifungua pacha wa kike walioungana kifua, tumbo


Musoma. Mwanamke mmoja mkazi wa Kata ya Buhare, Manispaa ya Musoma mkoani Mara, Helena Paulo (20), amejifungua watoto pacha wa kike walioungana eneo la kifuani hadi tumboni wakiwa na uzito wa kilo 4.6 kwa pamoja.
 Tukio hilo la ajabu katika Mji wa Musoma na mkoa kwa jumla, liliwavutia hisia za wananchi hali iliyosababisha msongamano katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa kwa madhumuni ya kutaka kushuhudia.
Akizungumza katika wodi ya wazazi hospitalini hapo, muuguzi wa zamu, Naabu Geraruma alisema mwanamke huyo alijifungua juzi saa saba usiku kwa njia ya upasuaji.
Geraruma alisema tukio hilo ni la kwanza katika hospitali hiyo na hali ya afya ya mzazi huyo na watoto inaendelea vizuri na muda wowote atahamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Mwanza.

Kwa upande wake, Mganga wa Idara ya Magonjwa ya Wanawake, Dk Simon Kamuli alisema baada ya jitihada za kuhakikisha mwanamke huyo anajifungua salama kukamilika, kinachofuatia ni kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa uangalizi zaidi.

Alisema kuwa hospitali ya mkoa haina uwezo wa kuwafanya chochote watoto hao, ikiwamo kuwatenganisha na taratibu zingine kabla ya uchunguzi wa kina.-MWA

Tuesday, December 16, 2014

WATUMIA NYETI ZA MWANAUME KAMA KEKI YA BIRTHDAY

Katika hali inayozidi kuonesha kuporomoka kwa maadili na heshima miongoni mwa wanawake, wasanii fulani nchini Nigeria wamefanya kali ya mwaka pale walipotengeza keki ya Birthday ya rafiki yao ambayo ilipambwa na taswira ya NYETI za kiume ambapo rafiki huyo alikuwa akiilamba kila wakati kama anavyoonekana pichani hapo juu.

Saturday, December 13, 2014

MAAJABU: MTOTO WA MWAKA MMOJA ASHIKA MIMBA NA KUJIFUNGUA....SOMA ZAIDI

PICHA YA MZAZI MTOTO AKIWA KTK CHUMBA CHA KUJIFUNGULIA WAKINA MAMA
ni kweli imetokea nchini china mtoto amzaa mtotot mwenzake,ni katika hali ya kushangaza wengi ila mchina 

amegeuza mambo mengi sana kwani tecknology anaijua vilivyo na ndio mana mambo kama haya aoni shida kujalibu na kuweka history katika dunia. kunausemi unasea unapopata tumia unapokosa jutia hii inamana

mchini ni wakati wake wa kutumia maarifa yake aliyo nayo kwa sasa kwani itafika kipindi kuna nchi zineingine zitakuja kasi na kutaka kumshinda kwa kila kitu.

BAD NEWS: MTU MWENYE UNENE MKUBWA KULIKO WOTE DUNIANI AFARIKI DUNIA...ALIKUWA NA KILO 444!


Rekodi mbalimbali zimekuwa zikivunjwa kila siku Duniani, siku chache zilizopita tuliisikia ile ya watu wawili waliovunja rekodi mbili kubwa ile ya mtu mfupi kuliko wote na mtu mrefu kuliko wote Duniani kukutana kwa mara ya kwanza.
Leo kuna taarifa kuhusu mtu aliyekuwa akishikilia rekodi ya mtu mnene kuliko wote duniani kwa kuwa na uzito wa Kilo 444, Keith Martin ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 44.
Wakati wa uhai wake aliwahi kufanywa upasuaji na  robo tatu ya nyama za kwenye tumbo lake ilikuwa imeondolewa na kufanikiwa kumpunguza nusu ya uzito wa mwili wake, ambapo kifo chake kimetokea miezi nane toka afanyiwe upasuaji huo kwa kuugua ugonjwa wa Pneumonia.
Kabla ya upasuaji Martin alikuwa anakula Calories 20,000 kiasi ambacho ni mara kumi ya kiasi ambacho kinapendekezwa kuliwa na mtu mzima.
Moja ya vitu alivyopendelea kula wakati wa kifungua kinywa ni Pizza na Mayai na kutokana na tatizo la uzito mkubwa Martin aliwahi kukaa ndani ya nyumba yake huko Uingereza kwa miaka 10 bila kutoka nje kutokana na kuelemewa na uzito mkubwa.
Moja ya dada zake amesema wana majonzi kumpoteza ndugu yao na bado wanaendelea kuomboleza msiba huo.
fattest-man-2-600x395
fattest-man-3-600x325
Fattest-Man-in-World-600x376

Thursday, September 11, 2014

AJALI YA MUSOMA YAZUA MAPYA


  • Written by  Tupambane Blog
  • Email
  • Tuma Maoni
  • Share on facebook Share on google_plusone_share Share on twitter

Marehemu wa ajali ya Musoma aliyezikwa juzi huko Musoma , leo ndugu zake wamekuta kafukuliwa na kaburin hakuna kitu, Musoma nzima yashangaa
TUPAMBANE BLOG