Showing posts with label marekiani. Show all posts
Showing posts with label marekiani. Show all posts
Tuesday, November 17, 2015
Tuesday, January 27, 2015
DHARUBA KUBWA YA THELUJI NA UPEPO MKALI YAPELEKEA KUSIMAMISHA HUDUMA ZA UMMA KASKAZINI MASHARIKI YA MAREKANI.
Lori maalumu la usafishaji likiondoa theluji iliondoka barabara ya South Church Street, katika mji wa Hazleton, Pennsylvania siku ya Jumatatu Jan 26, 2015. Photo via .dailymail.co.uk.
By Abou Shatry Washington DC
By Abou Shatry Washington DC
Zaidi ya watu 60 million wataadhithika kutokana na kimbunga kikubwa cha upepo unaoambatana na unyeshaji wa theleji katika eneo la kaskazini mashariki ya Marekani.
Kwa mujibu wa kitengo cha hali ya hewa nchini Marekani, imetaja maeneo ambayo yataathiriwa na tharuba hiyo, ya kihistoria ambayo itapelekea zaidi ya watu kadhaa kukosa huduma ya umeme, pamoja na huduma za usafiri wa anga na nchi kavu.
Imetaja baadhi ya majimbo ambayo yatakumbwa na kimbunga hicho kuwa ni New York, New Jersey, Massachusetts, Connecticut na Rhode Island, ambapo viongozi wakuu wamajimbo hayo kutangaza hali ya hatari kwa tukio hilo ambalo litatokea siku ya Jumatatu, Jumanne na Jumatano.
Imetabiriwa kiasi cha unyeshaji wa theluji hiyo 36inches katika jimbo la New York 16 hadi 26 inches katika jimbo la Boston, na kiwango chengine kama hicho katika baadhi ya majimbo mengine.
Zaidi ya safari za ndege 3,800 zimesimamishwa mapema leo Jumaatatu katia viwavya vya ndege vya JFK, LaGuardia na Newark airports, pia huduma za shule kufungwa siku ya jumanne na jumatano katika majimbo hayo.
Tuesday, November 25, 2014
Waziri wa Ulinzi wa Marekani ajiuzuru
Waziri wa ulinzi nchini Marekani, Chuck Hagel,amejiuzuru nafasi yake hiyo akiwa ametumia muda wa chini ya miaka miwili kazini.
Rais Barack Obama ameielezea hatua hiyo kuwa ni ya kawaida, na kumsifu Hagel kwa uamuzi aliouchukua lakini pia kwa ushauri alokuwa akimpatia na tabia yake ya ukweli na uwazi kwa kipindi chote alichokuwa waziri wa ulinzi.
Lakini wachunguzi wa mambo mjini Washington wanaielezea sababu halisi ya kujiuzuru kwa waziri huyo wa ulinzi ni kushindwa kuingilia misimamo ya raisi Obama juu ya sera ya uhamiaji.
Mwandishi wa BBC mjini humo amemuelezea waziri Hagel ambaye ni M Republican kuwa alichaguliwa kuvirejesha nyumbani vikosi vya kijeshi vya nchi hiyo vilivyoko Afghanistan na nje ya hapo lakini bajeti yake ikakatwa.
Lakini changamoto hiyo inayolikabili taifa hilo kutokana na kitisho cha kikundi cha dola ya kiislam Is,mgogoro wa Syria na Urusi na uchokozi wa Ukraine inadhaniwa kuwa ni toufauti za kitaaluma na bwana Hagel ametakiwa kusalia madarakani mpaka hapo mrithi wake atakapoteuliwa na baraza la Seneti.
Saturday, September 20, 2014
Marekani:Iran ina jukumu dhidi ya IS
Waziri wa
maswala ya kigeni nchini Marekani John Kerry amesema kuwa Iran ina
jukumu la kutekeleza katika juhudi za kimataifa dhidi ya wapiganaji wa
Islamic State nchini Iraq na Syria.
Bwana Kerry ameliambia baraza
la usalama la umoja wa mataifa kwamba muungano wa kuliangamiza kundi
hilo una majukumu mengine mbali na hatua za kijeshi na kwamba huenda
Iran ikashirikishwa.Wizara ya maswala ya kigeni nchini Marekani imebaini kwamba wawakilishi wa Iran na wale wa Marekani wamejadiliana kuhusu tishio linalosababishwa na wapiganaji hao kandokando ya vikao vya mkutano kuhusu mpango wa nuklia wa Iran.
Thursday, September 11, 2014
Marekani kupambana na Islamic State
- Written by Tupambane Blog
- Tuma Maoni
-
Share on facebook Share on google_plusone_share Share on twitter
Rais wa Marekani Barack Obama ametoa tamko kua hatasita kuchukua hatua stahiki dhidi ya kikundi cha wanamgambo wa dola ya kiislam huko Syria na Iraq.
Katika hotuba yake kwa taifa hilo ilooneshwa kupitia runinga ya taifa ameelezea mipango yake ya utekelezaji dhidi ya wanamgambo hao kua kikundi chochote cha kigaidi kitakachoitishia Marekani hakitakua salama milele.
Rais Obama pia amesema kwamba kikosi namba 475 watapelekwa Iraq ingawa hawatakua na jukumu lolote la kupambana na wanamgambo hao.
Inaelezwa kuwa kundi hilo la wanamgambo wa dola ya kiislam wanatwala eneo kubwa la Syria na Iraq,na wanamgambo hao wamegeuka kua hatari kwa matendo yao ya kuua watu kwa kuwakata vichwa waandishi wa habari kutoka ughaibuni huku ulimwengu ukishuhudi.
Marekani imesha fanya mashambulizi ya anga yapatayo
150 dhidi ya kikundi hicho cha Is na kugawanya silaha kwa wale wanakipinga kikundi hicho Iraqi vikundi vya ki Kurdi .
Katika hotuba yake hiyo ilodumu kwa muda wa dakika rais huyo amesema huu ni muda muafaka Marekani kuingilia kati na lazima Marekani itaongoza na kuwarejesha nyuma wanamgambo hao wa IS.
Akiizungumzia Iraq, amesema ataongeza nguvu za kulinda raia wa Marekani na kusambaza misaada ya kibinaadamu na tutaipiga Is .
Rais Obama amesema kwamba anakaribisha uungwaji mkono kutoka katika Bunge la Marekani lakini kwa mamlaka laonayo anayweza kuendelea na dhamira yake bila ruhusa ya bunge hilo.
Rais Obama alichaguliwa na chama chake cha Democrat kwasababu ya ari yake ya kupinga uvamizi katika nchi ya Iraq mnamo mwaka 2003 na kuongoza harakati za kuondoa wanajeshi wa Marekani nchini humo.
Wednesday, September 3, 2014
Obama kuongeza vikosi Iraq
3 Septemba, 2014 - Saa 04:52 GMT
- Google+
- Tuma kwa rafiki yako
- Chapisha na Tupambane
Rais Barack Obama
Rais Barack Obama wa Marekani
ameidhinisha kupelekwa vikosi vya wanajeshi wapatao 350 kwa lengo la
kuwalinda wanadiplomasia na wafanyakazi raia wa nchi hiyo waishio mji
mkuu wa Iraq Baghdad.
Ikulu ya Marekani imesema wanajeshi hao
watakaopelekwa baadhi yao ni wale wanaojihusisha na diplomasia ya ulinzi
ya iraq ambao ni zaidi ya mia nane.Hata hivyo Marekani inatarajia kuwatuma maofisa waandamizi akiwemo John kerry katibu mkuu wa marekani na Chuck Hagel katibu wa ulinzi ambao watakwenda mashariki ya kati katika harakati za kuimarisha ushirikiano.
Hatua hiyo inafuatia vitendo vya mashambulizi na mauaji yanayoendelea Iraq ikiwa ni matokeo ya utofauti kati ya Marekani na makundi ya wapiganaji ambao wamekuwa wakiwalenga raia wa Marekani waliopo nchini humo
Subscribe to:
Posts (Atom)
