Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA
Showing posts with label mirad. Show all posts
Showing posts with label mirad. Show all posts

Wednesday, December 10, 2014

TATHIMINI YA RIPOTI MRADI WA GEWE YAZINDULIWA DAR

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka pamoja na meza kuu wakionesha ripoti ya GEWE mara baada ya uzinduzi wake leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka pamoja na meza kuu wakionesha ripoti ya GEWE mara baada ya uzinduzi wake leo jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Kituo cha Usuluhishi (CRC), Bi. Gladness Munuo (wa kwanza kushoto) akizungumza katika uzinduzi wa ripoti ya Kutokomeza Ukatili na vitendo vya Unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto (GEWE) leo jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ripoti ya Kutokomeza Ukatili na vitendo vya Unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto (GEWE) leo jijini Dar es Salaam.

TAMWA Yazinduwa Tathmini ya Ripoti Mradi wa GEWE
Mratibu wa Mradi wa GEWE kutoka TGNP Mtandao, Matha Samwel akizungumza na vyombo vya habari katika uzinduzi wa ripoti ya Kutokomeza Ukatili na vitendo vya Unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto (GEWE) leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka akionesha ripoti ya GEWE mara baada ya uzinduzi wake leo jijini Dar es Salaam.
kurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka akionesha ripoti ya GEWE mara baada ya uzinduzi wake leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka akizungumza na viongozi wa vituo vya taarifa na maarifa waliokuwa katika hafla ya uzinduzi wa ripoti ya GEWE jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka akizungumza na viongozi wa vituo vya taarifa na maarifa waliokuwa katika hafla ya uzinduzi wa ripoti ya GEWE jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ripoti ya Kutokomeza Ukatili na vitendo vya Unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto (GEWE) leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ripoti ya Kutokomeza Ukatili na vitendo vya Unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto (GEWE) leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanahabari na viongozi wa vituo vya taarifa na maarifa wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa ripoti ya GEWE jijini Dar es Salaam Makao Makuu ya Ofisi za TAMWA Sinza Mori Dar es Salaam.
Baadhi ya wanahabari na viongozi wa vituo vya taarifa na maarifa wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa ripoti ya GEWE jijini Dar es Salaam Makao Makuu ya Ofisi za TAMWA Sinza Mori Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka pamoja na meza kuu wakionesha ripoti ya GEWE mara baada ya uzinduzi wake leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka pamoja na meza kuu wakionesha ripoti ya GEWE mara baada ya uzinduzi wake leo jijini Dar es Salaam.
CHAMA cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kwa kushirikiana na taasisi anuai za kijamii kimezinduwa tathmini ya ripoti juu ya utekelezaji wa mradi wa Kutokomeza Ukatili na vitendo vya Unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto (GEWE).
Akizinduwa ripoti hiyo leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka alisema mradi huo umekuwa na mafanikio makubwa kwa jamii katika kujitambua na kuibua vitendo vya Ukatili wa kijinsia ikiwa ni pamoja na vyombo vya habari kuibua vitendo hivyo zaidi ya hapo awali.
Alisema idadi kubwa ya habari, makala na vipindi vya redio na televisheni juu ya masuala ya ukatili vimefanywa maeneo mbalimbali nchini, jambo ambalo limeonesha mafanikio ikiwa ni pamoja na jamii kuelewa zaidi masuala ya ukatili na unyanyasaji na wengine kuanza kuyapiga vita kwa ushirikiano.
Aidha Mkurugenzi huyo Mtendaji wa TAMWA alisema mradi huo ulitekelezwa kwa pamoja kwa ushirikiano wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA), Chama cha Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) na Kituo cha Usuluhishi cha TAMWA (CRC), kinatekeleza mpango wa kutokomeza ukatili na unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto (GEWE II) katika wilaya 10 za Tanzania bara na Zanzibar.
Kwa upande wake Matha Samwel Mratibu wa Mradi wa GEWE kutoka TGNP Mtandao, akizungumza alisema mradi huo umekuwa na mafanikio makubwa kiasi cha kuibua changamoto ambazo zinaitaji utatuzi kwa ushirikiano na wadau wengine mbalimbali.
“…Katika kipindi cha utekelezaji wa mradi wa GEWE kumekuwa na mafanikio makubwa, moja wapo kubwa ni kuanzishwa kwa vituo vya taarifa na maarifa katika wilaya zote 10 za mradi, ambapo vituo hivyo vimekuwa vikitumika kama sehemu ya kutolea taarifa kwa jamii…sehemu ambayo wanajamii wanawake na wanaume wanakutana na kubadilishana taarifa na kuangalia namna ya kutatua matatizo yao yanayotoka katika jamii kama kubakwa, vipigo au kulawitiwa na mengineyo,” alisema Bi. Samwel.
Hata hivyo aliongeza kuwa vituo vya taarifa na maarifa vimekuwa na msaada mkubwa katika maeneo hayo kwani jamii zimeweza kuvitumia pia kwa kujadili namna ya kukuza uchumi kwenye familia zao kwa kuanzisha vikundi vya kijasiriamali vinavyochangia pia kupunguza umasikini kwenye jamii suala ambalo linachangia vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye jamii.
Anasema vituo vya taarifa na maarifa vimekuwa vikiunganisha nguvu na serikali na vyombo vingine vya dola kuhakikisha wanapambana na vitendo vya ukatili kwa kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake kwa watu wanaohusika ama kutuhumiwa na vitendo vya ukatili. Alitolea mfano katika eneo la Mwananyamala Kituo cha Taarifa na Maarifa kilishirikiana na Serikali kwa kuibua taarifa ya kuteswa kwa binti wa kazi za ndani na mwajiri wake jambo ambalo liliwezesha bosi huyo kufikishwa mahakamani.
“…Hivyo waweza kuona matokeo makubwa katika mradi wa GEWE ni kuanzishwa vituo vya taarifa na maarifa sehemu ambayo imekuwa ni kimbilio la wengi, na pili ni nguvu ya pamoja ya jamii katika uwajibikaji. Lakini changamoto iliyopo sasa ni namna ya kuwasaidia kwa kuwaifadhi waathiriwa wa vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii,” alisema Mratibu huyo.
Aidha aliitaka Serikali na wadau wengine kujitokeza na kushirikiana katika kujenga kituo kikubwa cha kuwasaidi wananchi ambao wamekumbana na ukatili wa kijinsia wakati wakipatiwa huduma kabla ya kurejea katika jamii yao. “…Mfano kumekuwa kuna mabinti hata hapa Dar es Salaam wamekuwa wakikimbia kukeketwa na familia zao lakini hakuna sehemu ya kuwaifadhi, hivyo tunaiomba Serikali na wadau wengine wajitokeze ili kuunganisha nguvu tujenge kituo hiki,” alisema.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com

Tuesday, November 18, 2014

MWANRI: ZUIENI UBADHIRIFU WA MIUNDOMBINU YA MAJI

SONY DSCKiongozi wa timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Mwenye koti jekundu) akihoji masuala mbalimbali kuhusu utekelezaji wa miradi ya maji kwenye manispaa ya Songea.SONY DSCTimu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikishuka kutoka kwenye tanki la kuhifadhia maji ya Mradi wa Maji wa Ruhuiko Kanisani utakaohudumia zaidi ya wakazi 3000 wa kitongoji ya Kijiji cha Ruhuiko Kanisani na maeneo ya jirani.SONY DSCKiongozi wa timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) akizungumza mara baada ya timu yake kukagua Mradi wa Maji wa Ruhuiko Kanisani. Wanaomsikiliza kutoka kulia ni Naibu Katibu Mtendaji (Uchumi Jumla), Prof. Longinus Rutasitara, anayemfuatia ni Msanifu wa Mradi huo Bw. Elezear Ndunguru na Mratibu wa ukaguzi huo Bw. Senya Tuni (Wapili kulia).
…………………………………………………………………
Na Saidi  Mkabakuli
Serikali imetoa wito kwa taasisi za umma kusimamia kwa umakini miundombinu ya miradi ya maji pindi inapokamilika ili kuweza kuwapatia wananchi huduma ya maji ya uhakika mara miradi hiyo inapokabidhiwa kwa kamati za usimamizi wa maji.
Wito huo umetolewa na kiongozi wa timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri wakati timu hiyo ilipokuwa ikifanya ukaguzi wa ujenzi wa miundombinu ya maji ya utekelezaji wa program ya maji na usafi wa mazingira katika vijiji 10 vya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Bibi Mwanri ambaye pia ni Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango anayeshughulikia Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu, alisema kuwa kwa miaka mingi kumekuwepo na ubadhirifu wa miundombinu ya miradi mingi ya maji hali inayorudisha nyuma juhudi za serikali za kuhakikisha kuwa wananchi wanafikiwa na maji safi na salama kote nchini.
“Kumekuwa na tabia mbaya ya ubadhirifu wa miundombinu hii, msikubali waiharibu ama kuiba vifaa vya ujenzi wa miradi yote 10 maana kama munavyoona serikali na wafadhili wamejitolea ili kuhakikisha munafikiwa na huduma hii muhimu,” alisema.
Akizungumza wakati timu hiyo ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ilipotembelea na kukagua Mradi wa Maji wa Ruhuiko Kanisani utakaohudumia zaidi ya wakazi 3000 wa kitongoji ya Kijiji cha Ruhuiko Kanisani na maeneo ya jirani, Msanifu wa mradi huo, Bw. Elezear Ndunguru alisema kuwa mpaka sasa utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 55.
“Kasi ya utekelezaji wa mradi huu ni ya kuridhisha kwani mpaka sasa tumeweza kujenga vituo 12 vya kuchotea maji kati ya 15, kinachongojwa kwa sasa ni kukamilika kwa tanki la kuhifadhia maji,” alisema.
Msanifu huyo ameongeza kuwa hadi kukamilikwa miradi yote 10 jumla ya shilingi bilioni 2.77 zitatumika na kuweza kuwahudumia zaidi ya wakazi 9000 wa vijiji vitakavyopitiwa na miradi hiyo.
Kwa mujibu wa Mpango wa Kwanza wa Maendeleo, lengo kuu kwa upande wa maji ni kuongezeka kwa upatikanaji wa maji safi na salama ni mojawapo ya maeneo yanayotiliwa mkazo ili kuweza kuongeza kasi ya maendeleo na kupunguza umaskini miongoni mwa Watanzania.

Monday, November 17, 2014

WANAWAKE WA INDIA WATEMBELEA VIKUNDI VYA WANAWAKE WAJASIRIAMALI MKURANGA

Mwakilishi wa Wanachama wa Ushirika wa Wanawake waliojiairi wenyewe kutoka India (SEWA), Labhu Thakkar akizungumza katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kuranga wakati walipotembelea vikundi vya wajasiriamali vilivyopo wilayani hapo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Mercy Sila na mlezi wa Kikundi cha Kiwalani Women Group ambaye pia ni mke wa mbunge wa Mkuranga, Naima Malima.
 Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Mercy Sila akizungumza na Wanachama wa Ushirika wa Wanawake waliojiairi wenyewe kutoka India (SEWA) walipotembelea vikundi vya wajasiriamali vilivyopo Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani, pamoja na kutembelea Zahanati ya kijiji cha Msufini Kidete. Kushoto ni mlezi wa Kikundi cha Kiwalani Women Group ambaye pia ni mke wa mbunge wa Mkuranga, Naima Malima.
 Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Mercy Sila akipokea zawadi kutoka kwa Mwakilishi wa Wanachama wa Ushirika wa Wanawake waliojiairi wenyewe kutoka India (SEWA), Labhu Thakkar walipotembelea vikundi vya wajasiriamali vilivyopo Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani, pamoja na kutembelea Zahanati ya kijiji cha Msufini Kidete. 
 Mkutano ukiendelea kabla ya wageni kutoka Ushirika wa Wanawake waliojiairi wenyewe kutoka India (SEWA) kutembelea Zahanati ya Kijiji cha Msufini Kidete iliyopo Mkuranga Mkoa wa Pwan
TUPAMBANE BLOG