Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA
Showing posts with label serikali. Show all posts
Showing posts with label serikali. Show all posts

Friday, April 10, 2015

MGOMO WA MADEREVA : SERIKALI YAKUBALI KUFUTA AGIZO LA KUWATAKA MADEREVA KWENDA KUSOMA


Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Gaudencia Kabaka amefanikiwa kumaliza mgomo wa madereva baada ya kutangaza kufuta agizo lililokuwa likiwataka madereva wa mabasi na malori kwenda kusoma tena katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT)Kuhusu suala la Madereva kusoma, Serikali na Madereva wamekubaliana kukutana mwezi huu tarehe 18 kuzungumza njia mbadala ya kutumika.
Miongoni mwa malalamiko ya madereva ilikuwa ni kukerwa na tochi za barabarani, hivyo jeshi la Polisi wamekubali kuziondoa.
Pia serikali imeagiza Madereva wote wapewe mikataba ya ajira za uhakika na waajiri wao na Trafiki wameagizwa kulifatilia hilo.

Thursday, November 6, 2014

VIONGOZI TANZANIA SAFI ICC-MEMBE

  • Share on facebookShare on google_plusone_shareShare on twitterShare on linkedin
UMOJA wa Afrika (AU) unatarajia kukutana hivi karibuni kujadili hatua za kuchukua kutokana na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta kupandishwa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) hivi karibuni.(MM)
Hatua hiyo inatokana na kupuuzwa kwa ombi la AU la kutaka Marais wa Afrika kutofikishwa ICC.
Katika hatua nyingine, imeelezwa kwamba viongozi wa Tanzania hawatafikishwa katika mahakama hiyo, kujibu mashitaka yoyote, kutokana na kufanya kazi nzuri na kwa kuzingatia misingi ya utawala bora na haki za binadamu.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, alisema bungeni mjini hapa jana kuwa viongozi wa nchi za Afrika, watajadili hatua za kuchukua dhidi ya ICC katika kikao chao kitakachofanyika Addis Ababa, Ethiopia Januari mwakani.
Rais Kenyatta alipandishwa katika Mahakama hiyo iliyopo The Hague, Uholanzi, Oktoba 8, mwaka huu, pamoja na Azimio la Umoja wa Afrika, kutaka viongozi wa Afrika wasifikishwe katika mahakama hiyo wanapokuwa madarakani.
Viongozi hao wa nchi za Afrika, walifikia Azimio hilo katika mkutano wao uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia, Oktoba 2013.
Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Chwaka, Yahya Kassim Issa (CCM) aliyehoji hatua zitakazochukuliwa na AU kwa Rais Kenyatta kupandishwa kizimbani na ICC, Membe alisema nchi 34 za Afrika wanachama wa ICC watatoa uamuzi wao kwa kitendo hicho.
Alisema pia kuwa si rahisi kwa viongozi wa Tanzania kufikishwa katika mahakama hiyo, kwa vile wanaendesha nchi vizuri na kwa kuzingatia misingi ya utawala bora.
“Naomba nilihakikishie Bunge kwamba hakuna kiongozi wa Tanzania atakayefikishwa ICC maana wanaendesha nchi vizuri sana,” alisema Membe.
Awali akijibu swali la mbunge huyo, Waziri Membe alisema ni kweli kwamba katika miaka ya hivi karibuni imejitokeza hali ya baadhi ya viongozi wa nchi za Afrika kushitakiwa ICC, lakini kushitakiwa huko hakumaanishi kuwa nchi za Afrika hazina umoja.
“Kimsingi nchi za Afrika zina umoja ulio imara. Hii inathibitishwa na namna nchi za Afrika zilivyoonesha umoja na mshikamano wa kiwango cha juu katika kukabiliana na changamoto hii. “Kupitia AU nchi za Afrika zimefanya vikao na kupitisha maazimio na maamuzi ya pamoja kwa ajili ya kupinga kushitakiwa kwa viongozi wa nchi za Afrika walio madarakani katika Mahakama hiyo ya ICC na kuliomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lenye mamlaka ya kusitisha kesi hizo kufanya hivyo,” alisem

Tuesday, November 4, 2014

ZITO KABWE AWATIA RUMANDE VIGOGO WA TPDC

01
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPDC, Michael Mwanda (mbele) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, James Andilile (nyuma yake), wakiongozwa na Polisi kuingia kwenye gari kwa ajili ya kupelekwa rumande baada ya kamati hiyo, kuwakuta na hatia ya kuidharau na kuinyima taarifa muhimu, wakati ilipokaa kama Mahakama katika kikao chake hicho.
02Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe, akifafanua jambo wakati akiwahoji Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Michael Mwanda na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, James Andilile wakati kamati hiyo, ilipokaa kama Mahakama katika kikao chake kilichofanyika jana, Ofisi za Bunge, Dar es Salaam. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Deo Filkunjombe.
03Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, James Andilile (kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya TPDC, Michael Mwanda
04Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPDC, Michael Mwanda (mbele) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, James Andilile (nyuma yake), wakiongozwa na Polisi kwenda kuingia kwenye gari kwa ajili ya kupelekwa rumande baada ya kamati hiyo, kuwakuta na hatia ya kuidharau na kuinyima taarifa muhimu, wakati ilipokaa kama Mahakama katika kikao chake hicho

Thursday, October 23, 2014

Mahakama ya Tanzania imedhamiria kutekeleza dira yake ya haki sawa kwa wote

  • Written by  Mjengwa Blog
  • Share on facebook Share on gomail Share on twitter 

Kaimu Mkurugenzi, Kurugenzi ya Usimamizi na Uendeshaji wa Mashauri kutoka Mahakama ya Tanzania Bw. John Kahyoza akiwaeleza waandishi wa (hawapo pichani) mikakati iliyoweka iliyowekwa na Mahakama ya Tanzania ili kutekeleza dira yake ya haki sawa kwa wote na kwa wakati kwa vitendo, kwa kuhakikisha inapunguza muda wa mashauri kukaa mahakamani, wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Habari wa Mahakama ya Tanzania Bi. Mary Gwera. Picha na Hassan silayo-maelezo
Na Georgina Misama-MAELEZO.
Mahakama ya Tanzania imedhamiria kutekeleza dira yake ya haki sawa kwa wote ili kuhakikisha inapunguza muda wa mashauri na rufaa kukaa Mahakamani kwa muda mrefu.
Hayo yamesemwa na Afisa Habari wa Mahakama ya Tanzania Bi Mary Gwera wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.(T.K)
Akizitaja hatua zilizochukuliwa na Mahakama Bi Mary alisema, kuboresha bajeti ya kushughulikia mashauri kupitia mfuko wa mahakama toka bilioni 57 kwa mwaka 2012/13 mpaka bilioni 88 mwaka 2014/15, Idadi ya vikao vya Mahakama ya Rufani vimeongezeka kutoka 26 mwaka 2012 hadi 34 mwaka 2013/14.
Aidha, Bi Mary alisema kuwa hatua nyingine ni pamoja na kuanzisha kitengo cha Mahakama Kuu Dar es Salaam kitakachoshughulikia masuala ya utatuzi wa mashauri kwa njia ya suluhu muafaka, pia uundwaji wa kamati ya kanuni za Mahakama itakayosaidia kutunga au kurekebisha kanuni ili kuhakikisha kuwa kanuni zinazotumika Mahakamani si chanzo cha kuchelewa mashauri Mahakamami
Naye, Kaimu Mkurugenzi, Kurugenzi ya Usimamizi na Uendeshaji wa Mashauri kutoka Mahakama ya Tanzania Bw. John Kahyoza alisema kuwa Mahakama imeanza kuchukua hatua za kuimarisha ukaguzi wa shughuli za Mahakama na maadili ya watumishi kwa kuanzisha kurugenzi ya ukaguzi na maadili.
Aidha, Bw Kahyoza alivitaja viwango ambavyo kila hakimu au Jaji anatakiwa kuvitimiza kwa mwaka na muda ambao mashauri yanatakiwa kuwa Mahakamani kuwa ni Mh. Jaji wa Mahakama Kuu analenga kumaliza kesi 220, Mahakimu wa Mahakama za Wilaya na Hakimu Mkazi kesi 250 na Mahakimu wa Mahakama za mwanzo kesi 260
Mahakama Kuu inatoa rai kwa Watanzania kufika Mahakamani kwa Tarehe zinazopangwa ili kuisaidia Mahakama kuhakikisha inapunguza muda wa mashauri kukaa Mahakamani.

Saturday, October 11, 2014

TAARIFA FUPI YA MAFANIKIO YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA SERIKALI..

  • Written by  Tupambane Blog
  • Share on facebook Share on gmail Share on twitter Share on linkedin
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Parseko Vicent Kone
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Parseko Vicent Kone.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Bw. Liana Hassan.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Bw. Liana Hassan.
Jengo la OPD katika Hospitali Mpya ya rufaa ya Mkoa wa Singida.
Jengo la OPD katika Hospitali Mpya ya rufaa ya Mkoa wa Singida.(Thommy kundy)
Jengo la utambuzi wa Magonjwa katika Hospitali Mpya ya rufaa ya Mkoa wa Singida.
Jengo la utambuzi wa Magonjwa katika Hospitali Mpya ya rufaa ya Mkoa wa Singida.
TAARIFA FUPI YA MAFANIKIO YA UTEKELEZAJI WA.doc by moblog

Wednesday, September 10, 2014

TANCIS KUPUNGUZA MUDA NA KUIONGEZEA MAPATO SERIKALI

  • Written by  Tupambane Blog
  • Email
  • Tuma Maoni
  • Share on facebook Share on google_plusone_share Share on twitter 
DSC_0002
Mkurugenzi Mkazi wa ASASI isiyo ya kiserikali ya kupiga vita umaskini Actionaid Tanzania (AATZ), Yaekob Metena akifungua kongamano la siku tatu kwa asasi zisizo za kiserikali, wawakilishi kutoka makundi ya vijana na waandishi wa habari juu ya masuala ya haki kwenye kodi linaloendelea kwenye hoteli ya Seascape jijini Dar.(Picha na Zainul Mzige wa MOblog)
Na Mwandishi wetu
MAMLAKA mbalimbali ambazo zinawajibika kwa namna moja au nyingine katika kuwezesha mizigo mbalimbali inayoingia nchini kutolewa bandarini zitaunganishwa na mfumo mpya wa kisasa wa kutumia mtandao wa kompyuta wa Tanzania Customer Integrated System (TANCIS) kwa lengo la kuharakisha uondoaji wa mizigo hiyo. (FS)

Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa elimu kwa walipa kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Diana Masalla wakati akitoa mada katika kongamano lililoandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali inayoendeshwa bila faida ikiwa na lengo la kupiga vita umaskini Actionaid Tanzania (AATZ) ikishirikiana na Kikundi cha haki kwenye kodi (Tanzania Tax justice Group).
Kongamano hilo ambalo linahusu haki kwenye kodi ni sehemu ya mpango wa asasi ya Action Aid Tanzania kuleta uelewa na weledi katika masuala ya kodi miongoni mwa watanzania na walipa kodi ili kufanikisha ukusanyaji wa raslimali zinazowezesha serikali kutoa huduma za msingi na pia kutengeneza fursa za wananchi kujiendesha kiuchumi.
Masalla alisema mfumo huo mpya ambao utamfanya mwenye mzigo kutoa maelezo ya mzigo wake kidigitali na maofisa forodha nao kushughulika na mzigo wake bila kukutana naye ana kwa ana, umeonesha ufanisi mkubwa hasa wa ufuatiliaji wa hatua kwa hatua tangu mzigo umeingia nchini hadi unamfikia mhusika.
Aidha mfumo huo umebana uchepushaji wa mizigo hiyo kutokana na ufuatiliaji wa kidigitali unaofanywa na mfumo huo.
DSC_0008
Meneja uratibu na mahusiano wa Action Aid Tanzania Bibi Jovina Nawenzake akielezea historia fupi ya ActionAid Tanzania na kazi wanazozifanya.
Alisema ingawa kumekuwepo na kilio kikubwa cha ucheleweshaji wa mizigo na kusukumiwa lawama hizo TRA, lakini kiukweli kuna mambo ambayo yanaingiliana na mamlaka zingine na mzigo hauwezi kutolewa mpaka mamlaka hizo ziseme na kwa mfumo wa zamani ilikuwa inachukua muda kuhangaika ofisi moja hadi nyingine.
Alisema mathalani kwa bidhaa za pembejeo , dawa na mazao mengine yenye sheria za kimataifa, mizigo yake haiwezi kuingia mpaka TBS au TFDA au wizara husika iidhinishe.
Alisema kuundwa kwa mamlaka na taasisi hizo katika mfumo mpya kutasaidia kila kitu kwenda kigitali na hivyo kuharakisha kasi ya uondoaji mizigo bandarini kutokana na kuongezeka kwa kasi ya utoaji wa vibali na ulipaji wa kodi.
Akiwasilisha mada ya uelewa wa misingi ya kodi na uchambuzi wa misingi ya sera ya kodi nchini Tanzania, Masalla alisema kwamba mfumo huo pamoja na kunung’unikiwa Julai mwaka huu baada ya kuzinduliwa Oktoba mwaka jana, maboresho makubwa yamefanyika ili kuufanya ujibu mahitaji ya wananchi na walipa kodi.
Miongoni mwa maboresho hayo ni kuweka kompyuta takribani 20 katika chama cha mawakala wa utoaji mizigo nchini TAFFA ambapo zinatumiwa na watumishi wa TRA kuingiza takwimu na kusaidia kujibu hoja za watumishi wa TRA kwa njia za mfumo wa kompyuta.
DSC_0116
Meneja wa elimu kwa walipa kodi kutoka mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), Diana Masalla, akiwasilisha mada ya uelewa wa misingi ya kodi na uchambuzi wa misingi ya sera ya kodi nchini wakati wa kongamano hilo.
Masalla alisema kwamba mfumo mpya unaleta makampuni na mamlaka zote husika katika mwavuli mmoja na hivyo kurahisisha utoaji huduma na kudhibiti upotevu wa mapato ya serikali.
Akifungua kongamano hilo Mkurugenzi mkazi wa Action Aid Yaekob Metena alisema kwamba ni lengo lao kuhakikisha kwamba kila mtanzania anajua misingi ya kodi na kwamba bila kodi serikali haiwezi kufanya majukumu yake ya msingi kama ukusanyaji wa rasilimali kwa ajili ya kuzitumia katika kazi nyingine.
Alisema kutokana na kukosekana kwa haki katika kodi kumefanya serikali kupoteza fedha nyingi ambazo zingeliweza kutumika kwa ajili ya kufungua fursa za ajira na pia kuhudumia shughuli za afya.
Mkurugenzi huyo alisema lengo kuu la kongamano hilo kutambua misingi ya kodi na sababu zake na pia kuelewa kwamba kuna haki ya kodi ambayo inamtaka kila mwananchi na mfanyakazi iwe wa umma au watu binafsi kutambua ushiriki wake katika kuiwezesha serikali kuwa na makusanyo makubwa ya kodi kwa maendeleo ya taifa.
Metena alisema: kama hakuna uelewa wa haki ya kodi na wahusika nao wakasababisha kodi isikatwe serikali itakuwa inapoteza fedha nyingi.
“Kama hakuna haki katika kodi, serikali haitaweza kukusanya mahitaji yake ambayo yanasubiriwa na watu wake”
DSC_0004
Pichani juu na chini ni baadhi ya washiriki wanaohudhuria kongamano la haki kwenye kodi lililoandaliwa na shirika la Actionaid Tanzania.
Amesema mfumo wa kodi unaposhindwa kuwafanya watu wote kushiriki katika kuitendea haki serikali kwa kulipa kodi ambayo ndiyo msingi wa mapato yanayochangia maendeleo na ustawi wa jamii.
Kongamano hilo la Actionaid Tanzania linafanyika katika hoteli ya Seascape iliyopo jijini Dare s salaam, lengo kuu likiwa kuhamasisha watu kutambua misingi ya kodi, sababu na serikali yenye makusanyo mazuri ya kodi inavyoweza kutengeneza fursa nyingi za kiuchumi ili wananchi wake waweze kuzitumia.
Lengo la kongamano hilo ikiwa kutanua uelewa na weledi wa washiriki ambao wengi wao ni kutoka asasi zisizo za kiserikali na waandishi wa habari wanaotakiwa kujua masuala ya kodi, baada ya mada mbalimbali, ofisa wa TRA aliulizwa kuhusu misamaha ya kodi.
DSC_0128
Katika kongamano hilo pia waandishi wa walijifunza utendaji wa serikali na pamoja na kuitaka serikali kuhakikisha kwamba wadau wenye fedha wanaotoa michango yao kwa ajili ya bajeti ya taifa na kuboresha huduma za msingi kwa wakati kwa Tanzania.
Aidha washiriki wengi katika kongamano hilo walihoji kisa cha serikali kung’ang’ania Pay as you earn (PAYE) kwa wafanyakazi na kuacha vyanzo vingine huku misamaha ya kodi ikiendelea kuitafuna.
Wakati huo huo katika mazungumzo na waandishi wa habari Masalla amewataka waandishi wa habari/jamii kufichua wakwepa kodi.
Aidha alisema kwamba sheria mpya ya VAT itaondoa misamaha mingi na hivyo kuisaidia serikali.
Pia amesisitiza wateja wanapofanya manunuzi kudai risiti.
DSC_0135
Mkufunzi wa kongamano la siku tatu la haki kwenye kodi, Bwana Mosses Kulaba kutoka kituo cha uendeshaji uchumi na sera za biashara, akiwasilisha mada inayohusu mfumo wa kodi nchini Tanzania na changamoto zake katika ukusanyaji kodi.
DSC_0099
Mmoja wa washiriki katika semina hiyo aliyeibua hoja ya kuwepo kwa jitihada za makusudi kwa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), kujikita katika kutafuta vyanzo vipya vya mapato kuliko kujikita katika kodi zilizozoeleka kama PAYE inayolenga kukusanya kodi zaidi kutoka kwa wafanyakazi na wafanyabiashara wadogo wadogo.
DSC_0088
Ndugu Anwar Mkama mwakilishi kutoka vyombo vya habari akiuliza swali kwa meneja elimu kwa walipa kodi juu ya changamoto za mfumo wa kodi nchini ni namna gani wanazishughulikia ili kuboresha ukusanyaji wa mapato na kupunguza urasimu.
TUPAMBANE BLOG