Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA
Showing posts with label sherehe za wasanii. Show all posts
Showing posts with label sherehe za wasanii. Show all posts

Friday, August 7, 2015

WASANII WAMUAGA RAIS KIKWETE


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Jakaya Kikwete akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali (hawapo pichani),waliofika ndani ya ukumbi wa Mlimani City  katika hafla ya kuagwa kwake ilioandaliwa na Muungano wa Wasanii kwa ajili ya kumshukuru kwa namna alivyowasaidia tangu alivyoingia madarakani kwa miaka 10 na pia kumtambulisha Mgombea wa Urais wa chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli,Dkt Jakaya Kikwete alizungumza mambo mbalimbali zikiwemo haki na hatimiliki za wasanii wa muziki pamoja na Bongomovie na pia alikubali kuwa mlezi wa tasnia hizo na kuhakikisha mambo yanakwenda sawa ndani ya tasnia hizo mbili adhimu kwa sasa hapa nchini.Picha na Ahmad Michuzi
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Jakaya Kikwete katikati pichani akiserebuka na wadau wa muziki na huku akipiga nao picha,ndani ya ukumbi wa Mlimani City  katika hafla ya kuagwa kwake ilioandaliwa na Muungano wa Wasanii kwa ajili ya kumshukuru kwa namna alivyowasaidia tangu alivyoingia madarakani kwa miaka 10 na pia kumtambulisha Mgombea wa Urais wa chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akipiga ngoma huku akishirikiana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipiga gitaa ndani ya ukumbi wa mlimani City jijini Dar.
Mwanadada Wema Sepetu akimtunza midola Dkt John Magufuli alipokuwa akipiga ngoma jukwaani kwa ustadi mkubwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Jakaya Kikwete akiwa ameambatana na Mgombea Urais wa chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,Katibu wa NEC Itikadi na Uuenezi Nape Nnauye na pamoja na Januari Makamba wakifurahia jambo kwa pamoja na wageni waalikwa mbalimbali waliofika ndani ya ukumbi wa Mlimani City kushiriki hafla ya kuagwa kwake ilioandaliwa na Muungano wa Wasanii kwa ajili ya kumshukuru kwa namna alivyowasaidia tangu alivyoingia madarakani kwa miaka 10.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Jakaya Kikwete akiwa ameambatana na Mgombea Urais wa chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli pamojoa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  (mwisho kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh.Paul Makonda wakiwasili ndani ya ukumbi wa Mlimani City kushiriki hafla ya kuagwa kwake ilioandaliwa na Muungano wa Wasanii kwa ajili ya kumshukuru kwa namna alivyowasaidia tangu alivyoingia madarakani kwa miaka 10.
Rais Dr. Jakaya Kikwete akifurahia jambo  na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kupitia CCM wakati alipowasili Mlimani City jijini Dar es salaam kwa ajili ya kushiriki hafla ya chakula cha jioni kilichondaliwa na Muungano wa wasanii Kumshukuru Mh. Dr. Jakaya Kikwete kwa jinsi alivyowasaidia katika uongozi wake wa miaka 10 kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kumkaribisha Mgombea wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dr. John Pombe Magufuli, Kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana pia akishiriki tukio hilo.Hafla hiyo imehudhuriwa na wasanii mbalimbali  wakiwemo waigizaji wa filamu, wachezaji na wanamuziki wakishiriki kwa pamoja kumshukuru Dk.Jakaya Kikwete.
 Baadhi ya Wadau wa muziki wakifurahia jambo wakati Rais Dkt Jakaya Kikwete alipokuwa akiwasili ndani ya ukumbi wa Mlimani City.
 Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na baadhi ya wadau wa muziki nchini ndani ya ukumbi wa mlimani City usiku huu.
 Dkt Jakaya Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya Vodacom,Kelvin Twisa
 Dkt Kikwte akisalimiana na baadhi ya Wasanii wa muziki wa bongofleva
 Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam,Mh Said Meck Sadick ndani ya ukumbi wa mlimani city usiku huu.
 Mmoja wa wasanii akiimba jukwaani kwa hisia.
Baadhi ya Wanamuziki wakongwe walihudhuria hafla hiyo iliyofana kwa kiasi kikubwa.









Wanauziki wakongwe pia walikuwepo kumshukuru Rais Kikwete kwa mambo mengi aliyoyafanya katika uongozi wake wa miaka kumi ndani ya tasnia ya muziki








 Mmoja wa wasanii akitumbuiza jukwaani usiku huu

Saturday, April 4, 2015

MENGI NA MKEWE KYLN WALIVYO FUNGA NDOA YA KIHISTORIA



Mr and Mrs Mengi wakiwa na furaha siku ya Ndoa yao 



Mimi Dr. Reginald Mengi naahidi kumpenda Jacqueline Ntuyabaliwe katika shida na raha hadi kifo kitutenganishe
Ilikuwa ni furaha, upendo wa dhati na shangwe pomoni.
Baada ya miaka kadhaa ya uhusiano thabiti na uliokuwa umetawaliwa na upendo usio kifani, Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Limited, Dr. Reginald Mengi na Miss Tanzania, 2000, Jacqueline Ntuyabaliwe wamefunga ndoaWawili hao wamebahatika kupata watoto wawili mapacha pamoja. Watoto hao wa kiume nao waliungana na wazazi wao kushuhudia wazazi wao wakibadilisha viapo vya ndoa

Sunday, December 21, 2014

KWAYA MAALUM MBEYA YATINGA KAMBINI KUIBEBA KRISMASI

images
Na Mwandishi Wetu
KWAYA maalum jijini Mbeya wiki iliyopita iliingia kambini kwa siku moja kujiandaa na uzinduzi wa albamu yao ya Mubhopeghe Pa Finganilo (Kimbilieni kwenye ahadi) yenye nyimbo nane.
Kwa mujibu wa Mchungaji wa Kanisa wa EAGT, Zacharia Mwakasaka kambi hiyo inashirikisha waimbaji ambao ni Maaskofu, Wachungaji na viongozi mbalimbali wa dini waliomo kwenye Kwaya hiyo.
Mwakasaka alisema uzinduzi huo unashirikisha waimbaji, maaskofu na wachungaji waliopita kwenye mikono ya mzee Amulike Mwakiteka (84).
Mwakasaka alisema kupitia uzinduzi huo waumini mbalimbali watajionea viongozi hao ambao wanaongoza makanisa mbalimbali hapa nchini.
Mwakasaka alizitaja nyimbo zilizoko kwenye albamu hiyo ni pamoja na Mubhopeghe Pa Finganilo, Lazaro, Ilisubha ‘Jua Linachomoza’, Yesu alipokwenda, Jesu Bho Ikufyuka ‘Yesu alipopaa’, Matendo, Gwe Kyala Mwikemo ‘Mungu Mtakatifu’ na Nasobhile ‘Nilikuwa nimepotea Msituni’

Wednesday, November 26, 2014

SEND OFF PARTY YA NOREEN MHINA YAFANA KATIKA UKUMBI WA DELUXE SINZA.

 
 Bibi Harusi Mtarajiwa Noreen Mhina  akiwa katika nyuso ya Furaha, jana tarehe 25.11.2014
  
 Bibi Harusi Mtarajiwa Noreen akiwa amempata Mume wake mtarajiwa Leonard  Baada ya kumsaka ukumbi Mzima kwa ajili ya kumtambulisha kwa wageni waalikwa .
 Bibi harusi Mtarajiwa Noreen akimvisha Mume wake mtarajiwa Leonard  zawadi ya Saa Mara baada ya kutambulishwa Rasmi wa wageni waliofika katika Sherehe ya kumuaga
Mc wa Sherehe hiyo ya Kumuaga Noreen Akiendelea na yake
 
 Bwana Harusi Mtarajiwa Leonard  akionesha zawadi yake ya saa aliyonunuliwa na Mke wake mtarajiwa Noreen ikiwa ni moja ya zawadi ya kufika kwake katika sherehe hiyo
 
 Mume Mtarajiwa Leonard  wa Noreen akiwa anamlisha  Chakula Mkewe Mtarajiwa ishara ya Upendo
Msemaji wa upande wa Bwana harusi mtarajiwa akiwakaribisha Rasmi katika harusi upande wa wazazi wa Noreen, Ndugu jamaa na marafiki na kutoa nasaha chache. Jana Tarehe 25.11.2014
Meza
ya wazazi wa upande wa Bibi harusi mtarajiwa wakiwa wanasikiliza Nasaha
kutoka kwa msemaji wa upande wa Bwana Harusi mtarajiwa.
Wadada wa Mujini nao walimwagia pesa za kutosha Noreen..
Baadhi ya Marafiki wakubwa wa Noreen aliosoma nao katika chuo cha CBE Dodoma
Palikuwa hapatoshi hapa ambapo Noreen na Bwana Harusi Mtarajiwa Leonard  pamoja na wageni wengine waalikwa walicheza kwaito ya nguvu..
Burudani ya Nguvu inaendelea hapa..
Kama kawaida wale mapaparazi wa kujitegemea hawakosi kupata ukodaki wa nguvu kwa ajili ya Facebook, Twitter, Instagram, Whatsapp na kwengine kwingi kuifanya sherehe kuwa inanoga zaidi
Baadhi ya Wageni waalikwa wakifuatilia Sherehe na kufurahi.
Bibi Harusi Mtarajiwa akiwa anapunga mikono kuaga wageni waalikwa ishara ya kuondoka ukumbini kwenda kupumzika na kujiandaa na harusi huku akisindikizwa na wapambe wa kutosha
TUPAMBANE BLOG