Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA
Showing posts with label somalia. Show all posts
Showing posts with label somalia. Show all posts

Wednesday, May 20, 2015

Somalia:Majeshi ya Burundi kuondolewa?

Jeshi la Burundi ni sehemu ya majeshi ya Amisom yanayopambana na Alshabaab nchini Somalia
Mjumbe wa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa nchini Somalia, Nicholas Kay amesema ikiwa hatua ya kuondoa majeshi ya Burundi itafanyika nchini Somalia itaathiri mapambano dhidi ya wanamgambo wa Al Shabab.
mwanzoni mwa juma hili Marekani ilitangaza kupunguza kiasi cha pesa inachotoa kwa majeshi ya Burundi baada ya shutuma kuwa jeshi hilo limejihusisha katika vitendo vya ukiukwaji wa haki za binaadam wakati wakizima vurugu zilizojitokeza wakati jaribio la mapinduzi dhidi ya Serikali ya Rais Pierre Nkurunziza liliposhindwa.
AU nayo imesita kupeleka kundi jingine la wanajeshi wa Burundi nchini Somalia.Lakini Kay ameiambia BBC kuwa majeshi ya Umoja wa Afrika yanahitaji msaada kuweza kupambana na Al Shabaab.pia ametahadharisha kuongezeka kwa mahitaji ya kibinaadam nchini Somalia na kutoa wito wa jumuia ya kimataifa kuendelea kupeleka misaada nchini humo.

Tuesday, April 7, 2015

Jeshi la Kenya lafanya shambulio Somalia


Ndege za kijeshi za Kenya zashambulia Somalia
Ndege za kijeshi za Kenya zimeshambulia maeneo ya wapiganaji wa kundi la Alshabaab katika taifa jirani la Somalia ,msemaji wa jeshi ameiambia BBC.
Ndege hizo zililenga maeneo mawili ya jimbo la Gedo,linalotumiwa na wapiganaji hao kuvuka na kuingia Kenya, msemaji huyo ameongeza.
Maeneo hayo mawili hutumiwa na wapiganaji hao kupanga mshambulizi nchini Kenya.
Wanajeshi wa AMISOM walitarajiwa kupeleka wanajeshi wao katika eneo hilo la Gedo lakini hadi sasa hawajafanya hivyo.
Hili ni shambulio la kwanza la Kenya kwa shambulizi la alshabaab ambalo lilisababisha mauaji ya watu 148 katika chuo kikuu cha Garissa wiki iliopita.
Amisom
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameapa kujibu shambulizi hilo kwa njia mbaya zaidi.
Msemaji wa jeshi la Kenya David Obonyo ameiambia BBC kwamba Jeshi la Kenya lilijibu vitisho kwa kutekeleza mashambulizi ya angani siku ya jumapili usiku katika eneo hilo.
Hakuna maelezo zaidi ya oparesheni hiyo yaliotolewa.

Thursday, January 22, 2015

Somalia Lugha za kigeni marufuku,ofisini

jamii ya wasomali
Rais wa Somalia amepiga marufuku ya matumizi ya lugha za kigeni katika ofisi za serikali na kusema kuwa lugha pekee ya mawasiliano katika ofisi hizo ni kisomali.
Raisi Hassan Shaykh Mahmud alikuwa akizungumza hayo katika sherehe za maadhimisho ya kutimiza miaka 42 tangu kuanza kutumika kwa lugha ya Kisomali nchini humo ,maadhimisho yaliyofanywa mjini Mogadishu kwa lengo la kutaka kuiimarisha lugha hiyo.Hata hivyo maadhimisho hayo yalihudhuriwa na mamabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini humo.
Matumizi ya lugha ya kisomali katika ofisi za serikali yametakiwa kuanza January mosi mwaka huu na kuendelea.Shughuli zote za kiserikali nchini humo zimetakiwa kuendeshwa katika lugha ya kisomali na si lugha ingine yoyote.Ruhusa ya matumizi ya lugha za kigeni imetolewa tu wakati wageni kutoka nje ya somalia watakapo kuwa wakihudumiwa .
Hata hivyo waziri wa habari wa taifa hilo,ametilia mkazo kauli hiyo na kudai kwamba January 21 ni siku muhimu sana kwa taifa hilo,na siku hiyo ni kumbu kumbu kwa gazeti la kisomali la kwanza kuchapishwa.naye spika wa bunge la Somalia,Muhammad Shaykh Usman Jawari,ambaye pia alitoa kauli yake kwenye maadhimisho hayo,na kusema kwamba ni jambo muhimu kwa jamii ya wasomali kuelewa umuhimu wa lugha yao na kuitaka jamii kuiimarisha lugha hiyo.
Rais Mahmud aliongeza kusema kwamba tarehe 21 January ni siku muhimu kwa wasomali na serikali yao.

Monday, September 29, 2014

Somalia:Wakazi wahisi kuwa salama


Licha ya matumaini mengi, wengi bafdo wana wasiwasi na kundi la wanamgambo la Al Shabaab
Wakazi katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, wanahisi kuwa salama na wenye matumaini zaidi kuliko hali ilivyo kuwa mwaka mmoja uliopita.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na taasisi ya masomo ya sera, ambayo ilitathmini data iliyokusanywa kutoka kwa zaidi ya watu 1,600.
Wengi wao walisema kuwa visa vya ghasia vimepungua.
Hata hivyo, wasiwasi mkubwa ungali kuhusu mashambulizi kutoka kwa kundi la wanamgambo wa Al Shabaab na wakazi kukosa imani na taasisi za usalama.
Somalia imekuwa ikikumbwa na ghasia kwa zaidi ya miongo miwili.
Licha ya hali hiyo maelfu ya wasomali waliokimbilia mataifa ya kigeni wamekuwa wakirejea nyumbani kujenga upya nchi yao kwani hali ya usalama angalau imeimarika katika miaka ya hivi karibuni.
Wapiganaji wa Al-Shabab, walifurushwa kutoka Mogadishu mwaka 2011 lakini mara kwa mara kundi hilo hufanya mashambulizi maeneo ya mjini na bado wanadhibiti maeneo mengi ya vijijini.
Mnamo mwezi Februari, wapiganaji wa kundi hilo, walishambulia jengo la Villa Somalia, ambalo lina makazi ya Rais na taasisi zengine za serikali na kuwaua watu 11.
Kulingana na utafiti huo, wakazi wengi walisema kuwa bado hawajashuhudia makabiliano ya kikabila katika mwaka mmoja uliopita.
Hata hivyo, watu wengi bado wanasema wana wasiwasi kuhusu mzozo kati ya jamii mbali mbali na mashambulizi yanayofanywa na Al Shabaab.
Pia walisema kuwa hawana imani na taasisi za usalama pamoja na idara ya mahakama.
Katika eneo moja, asilimia 66 ya wakazi waliohojiwa, walisema walionelea bora kuripoti utata wowote kwa viongozi wa kijamii huku asilimia 7 pekee wakitafuta msaada wa polisi.
TUPAMBANE BLOG