Sikukuu ya IDD: Ulinzi Waimarishwa jijini Dar.....FFU, Polisi Wanamaji, Askari wa Mbwa na Farasi, Helkopta ya Polisi na Magari ya Washawasha yatatumika kulinda Amani
1.
Limepanga kushirikiana na vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama ikiwa
ni pamoja na Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji, Kampuni binafsi za ulinzi,
Vikosi vya uokoaji wakati wa majanga, na vikundi vya Ulinzi Shirikishi
ili kuhakikisha kuna udhibiti wa matukio ya uhalifu au fujo zinazoweza
kujitokeza.
2.
Tumejipanga kutumia Kikosi cha FFU kikijumuisha askari na magari ya
washawasha, Askari wa Mbwa na Farasi. Kikosi cha Polisi Wanamaji nacho
kitakuwepo. Pia Vikosi vya Kuzuia Dawa za Kulevya, askari wa kawaida
(GD), askari wa Usalama Barabarani, na askari Makachero. Wote hawa
wamepewa maagizo maalum ya kuchukua hatua kabla matukio ya uhalifu
hayajajitokeza na sio kungoja tukio lifanyike. Kwa mantiki hiyo, dalili
zozote za uvunjifu wa amani litashughulikiwa pasi na ajizi.
3. Zitakuwepo doria za Miguu, doria za pikipiki na doria za miguu katika barabara zote muhimu.
4.
Wananchi wanashauriwa kusherehekiea siku ya Idd El Haji katika ngazi ya
familia au kukusanyika katika mitaa kwa amani wakisherehekea.
5.
Aidha kutokana na sababu za kiusalama na matishio mbalimbali katika
ukanda wa Afrika ya Mashariki, Jeshi la Polisi limepiga marufuku disko
toto katika kumbi mbalimbali kutokana na sifa za kumbi hizo kutokidhi
viwango vya kiusalama.
6.
Wananchi wanapoona dalili zozote au maandalizi ya uvunjifu wa amani
watoe taarifa mapema iwezekanavyo katika vituo vya Polisi vya karibu ili
hatua zichukuliwe kwa haraka.
7.
Madereva wanatakiwa kuzingatia sheria za usalama barabarani ikiwa ni
pamoja na kutoendesha vyombo vya moto kwa mwendo kasi, wasiwe walevi,
magari au pikipiki zenye sauti kali/zenye kuleta mshtuko nazo ni
marufuku.
8.
Aidha, Kikosi cha Polisi Wanamaji (Marine Police) kitafanya doria
kwenye fukwe za Bahari na maeneo yote ya Bahari jijini Dar es Salaam.
Patakuwepo Helkopta ya Jeshi la Polisi ikifanya doria kuzunguka jiji la
Dar es Salaam na askari wa Kikosi cha Mbwa na Farasi nao watahusika na
doria.
9.
Polisi watatoa ulinzi katika fukwe za bahari, kwa kuweka vituo vya
Polisi vya muda vinavyohamishika (Mobile Police Station) ili kutoa
msaada wa haraka pindi unapohitajika. Pia askari wa kutosha watakuwepo
kuhakikisha wananchi wanasherehekea kwa amani.
10. Aidha, kwa urahisi wa mawasiliano wananchi wasisite kutoa taarifa za uhalifu kwa namba muhimu za simu zifuatazo:
1. RPC ILALA: Mary Nzuki – SACP 0754 009 980 / 0754 339 558
2. RPC TEMEKE: Kihenya wa Kihenya – SACP 0715 009 979/ 0754 397 454
3. RPC K’NDONI: Camillius Wambura – ACP 0715 009 976 / 0684 111 111
“NAWATAKIA NYOTE HERI YA IDD EL FITR 2014”.
S.H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM


No comments:
Post a Comment