Bunge lakodi vipaza sauti kwa Sh8.9 milioni kila siku
NaThommy kuny Mwananchi
Posted Jumatatu,Agosti11 2014 saa 8:22 AM
Posted Jumatatu,Agosti11 2014 saa 8:22 AM
Kwa ufupi
Kwa maana hiyo Bunge, hilo linatumia Dola 5,400 sawa
na Sh8.91 milioni kwa siku kugharimia vipaza sauti katika vyumba 12
vinavyotumiwa na kamati hizo na kwa siku 16 ambazo kamati zitakutana,
gharama hizo zitafikia Sh142.56.
Dodoma. Wakati kukiwa na
malalamiko kwamba Bunge la Maalumu la Katiba linagharimu fedha nyingi za
walipakodi, uongozi wa taasisi hiyo umetumia Sh142.56 milioni kukodi
vipaza sauti kutoka Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).
Katibu wa Bunge Maalumu, Yahya Khamis Hamad
alithibitisha kukodiwa kwa vipaza sauti hivyo kwa ajili kamati zote 12
na kwamba kila gharama ya chumba kimoja kwa siku ni Dola 450 za Marekani
(Dola moja ni wastani wa Sh1,650).
Kwa maana hiyo Bunge, hilo linatumia Dola 5,400
sawa na Sh8.91 milioni kwa siku kugharimia vipaza sauti katika vyumba 12
vinavyotumiwa na kamati hizo na kwa siku 16 ambazo kamati zitakutana,
gharama hizo zitafikia Sh142.56.
“Vifaa vya sauti tulivyokuwa navyo vinalalamikiwa,
vilikuwa siyo standard (viwango) hasa vya mazungumzo, tumekodi kutoka
Ukumbi wa Mikutano wa AICC na tumekuwa nao usiku mzima kuvifunga,”
alisema.
Alisema tangu wavifunge, hawajawahi kupata
malalamiko tena kutoka katika kamati kuhusu ubora na kwamba gharama za
kukodisha vifaa hivyo itatoka katika fungu la dharura la Bunge Maalumu.
“Mara ya kwanza walituambia gharama zao ni Dola
500 kwa siku lakini tukajadiliana nao, hivyo tukafikia kiwango hicho cha
Dola 450,” alisema.
Hamad alisema vifaa vya awali ambavyo
vililalamikiwa na wajumbe kuwa havitoshi, vinatoa sauti nje ya majengo
na kwa jinsi vilivyo, vinalazimika kutembezwa ukumbini, hivyo
kusababisha usumbufu.
Malalamiko ya gharama
Suala la gharama limekuwa likiibuka mara kwa mara
na wakati mwingine kutajwa kama sababu ya kuahirishwa kwa Bunge hilo kwa
kuwa hakuna uhakika wa kupatikana kwa akidi inayotakiwa kufikia uamuzi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana,
Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), Deus Kibamba
alilalamikia kile alichokiita “matumizi ya kufuru” ya Bunge Maalumu
wakati hakuna uhakika wa kupatikana kwa Katiba Mpya.
Kibamba alisema ikiwa Bunge litaendelea na vikao
vyake hadi Oktoba 31, mwaka huu kama ratiba inavyoonyesha, sehemu hiyo
ya mchakato itakuwa imeligharimu taifa Sh40 bilioni, fedha ambazo
zingetosha kugharimia maji kwa wananchi wote wa Wilaya za Kondoa mkoani
Dodoma na Kilindi, Tanga.
“Tatizo kubwa hapa ni posho, kila mara sheria na
kanuni zimekuwa zikibadilishwa ili kuongeza muda wa Bunge siyo kwa ajili
ya kitu kingine, bali kwa ajili ya posho, kwa hiyo gharama zinazidi
kuongezeka na haya ni matumizi ya kufuru ambayo hayapaswi kufanywa
katika nchi maskini kama yetu,” alisema Kibamba na kuongeza
No comments:
Post a Comment