- Written by Tupambane Blog
- Tuma Maoni
-
Share on facebook Share on google_plusone_share Share on twitter
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Iringa(CCM) Rita Kabati akizungumza na wanawake viongozi wa chama hicho hawapo pichani.
Baadhi ya
wanawake walihudhuria mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyofanyika katika
ukumbi mdogo wa ccm mkoani Iringa. (Picha na Denis Mlowe)
Na Denis Mlowe,Iringa
WANAWAKE mkoani Iringa wameshauriwa kuwasomesha watoto wako bila kukata tamaa kwa faida ya familia na nchi kwa ujumla. FRIDAY SIMBAYA
Wito huo
umetolewa na Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa (Ccm), Rita Kabati
wakati akizungumza na viongozi wanawake wa ccm mkoani hapa katika semina
ya mafunzo kuwajengea uwezo katika kujiandaa uchaguzi wa serikali za
mitaa na uchaguzi mkuu.
Alisema
kuwa imekuwa kasumba ya mabinti wengi kukimbilia mijini na kuacha masomo
ambayo yangewasaidia katika maisha yao ya mbele na familia.
Aliwataka
wanawake kushirikiana katika malezi ya watoto hasa wa kike kwa
kuwapelaka shule kwa malengo ya kusaidia taifa na Familia kwa jumla
hivyo upendo na ushirikiano ni jambo .
Kabati
amewaasa wazazi kuipa kipaumbele suala la elimu na kuwaeleza kuwa
wasichague kuwasomesha watoto wa kiume na kuwaacha watoto wa kike na
kuwaona kuwa wao ndio wanaoweza kuwasaidia wazazi kuliko watoto wa kiume
"Watoto
wanahitaji elimu iliyobora hivyo watoto wanakuwa katika misingi iliyo
bora na wanawake wahakikishe wanalea katika maadili ya kanisa kuweza
kupata misingi bora ya maisha kwa vizazi vijavyo." Alisema Kabati
Aidha
aliwataka wanawake kuombea amani kwa lengo la kupata katiba iliyokuwa
bora na yenye kuondoa utegemezi na kumkandamiza mwanamke.
"Kila mtu
kwa nafasi yake mtii mungu kuweza kufanikisha malengo yake hivyo
kushikamana kwa pamoja katika kuweza kupata katiba iliyo bora na
ninawapongeza kwa kuweza kudumisha amani na upendo katika mkoa wa
Iringa" alisema Kabati
No comments:
Post a Comment