Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Friday, September 26, 2014

Asamoah Gyan akana madai ya kafara



Ex-Sunderland-star-Asamoah-Gyan_c5e87.jpg
Nahodha wa timu ya taifa ya Ghana, Asamoah Gyan, amekanusha madai 
kuwa alimtoa 
 kafara yake ambaye pia alikuwa mwanamuziki mashuhuri nchini Ghana 
 Castro.

Gyan amesema tetesi hizo ni za kushangaza sana wala hazina msingi.

Mwanamuziki huyo aliyekuwa anaiimba nyimbo za mtindo wa Afrobeats, 
ambaye jina 
lake halisi ni Theophilus Tagoe, alitoweka pamoja na rafiki yake 
Janet Bandu,
 mnamo mwezi Julai.

Wawili hao walitoweka wakati walipokuwa wamekwenda likizo na Gyan 
ambaye alikuwa 
mchezaji wa zamani wa Sunderland, katika mji wa Ada.

Madai katika vyombo vya habari nchini Ghana yanasema kuwa kutoweka 
kwa rafiki 
 ya Gyan kumezua wasiwasi baadhi wakidai kuwa huenda alimtoa 
kafara mwanamuziki huyo.
BBC


Castro na rafiki yake Bandu, walionekana kwa mara ya mwisho 
wakielekea baharini na 
baadaye iliarifiwa kuwa walizama.

Miili ya wawili hao haikuwahi kupatikana na madai yaliendelea 
kusambazwa mwezi huu 
wakati ambapo kakake Gyan, Baffour Gyan alidaiwa kuwa mmoja wa genge 
 la 
vijana waliowashambulia wandishi wa habari waliohoji maswali kuhusu
 madai hayo.

Hata hivyo baadaye aliachiliwa na polisi waliokuwa wamemkata kwa lengo 
la 
kumfungulia mashitaka.

Tetesi hizo zilimfanya Gyan kuitisha mkutano na wandishi wa 
habari kuzungumzia madai 
hayo.

Wakili wake Kissi Agbyabeng alitoa taarifa akisema kuwa familia ya 
Gyan imeshangazwa
 sana na madai hayo na iliamua kutosema chochote ili polisi waendelee 
na uchunguzi wao.

Taarifa hiyo ilisema: " Tumekuwa kimya huku madai na tetesi zikienezwa 
kila upande 
katika vyombo vya habari. Tumekuwa kimya sio eti kwa sababu 
 tunaficha ukweli, bali
 kwa sababu hatuoni umuhimu wa kusema kilichojiri mjini Ada. Tumekuwa 
kimya kwa 
sababu tunataka polisi wafanye kazi yao bila kuingiliwa.''

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG