Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Thursday, September 4, 2014

BIG BROTHER AFRICA YAAHIRISHWA 'KWA MUDA'

  • Written by  Tupambane Blog
  • Email
  • Tuma Maoni
  • Share on facebook Share on google_plusone_share Share on twitter 
BBA_50119.jpg
Uzinduzi wa kipindi cha 'Big Brother Africa' umeahirishwa kwa muda baada ya moto mkali kuzuka katika jengo linalotumika kama studio za kuendeshea kipindi hicho jijini Johannesburg.
Kipindi hicho, kilichokuwa kianze siku ya Jumapili, sasa kimeahirishwa, wakati watayarishaji wakitafuta jengo mbadala. Hakuna aliyeumia katika tukio hilo, na sababu hasa za chanzo cha moto hazijajulikana, huku uchunguzi ukiendelea. Washiriki kutoka nchi 14 walitarajiwa kushiriki katika makala haya ya tisa. Kipindi hicho kingefanyika kwa siku 91 kabla ya mshindi mpya kutajwa, kuchukua taji kutoka kwa mshindi wa mwaka jana, Dilish Matthews kutoka Namibia. Mshindi wa mwaka huu atapewa zawadi ya dola 300,000, sawa na alizochukua mshindi wa mwaka jana. Watayarishaji wa kipindi hicho Endemol na M-Net wamesema juhudi za kutafuta studio na nyumba nyingine itakuwa ngumu katika kipindi kifupi kutokana na "miundombinu ya hali ya juu ya kiufundi" ambayo, "haiwezi kupatikana mara moja". Kipindi hicho tayari kilipata 'kwikwi' baada washiriki kutoka Ghana kukabiliwa na matatizo ya kupata visa na hivyo raia wa Ghana wanaoishi Afrika Kusini kuchukua nafasi zao. Ushiriki wa Rwanda, kwa mara ya kwanza, pamoja na Sierra Leone ulilazimika pia kutofanyika. Kipindi hiki kilikuwa kioneshwe barani Afrika kupitia televisheni za satellite. Big Brother Africa kimekuwa kipindi maarufu tangu kilipoanza mwaka 2003, na kimetoa washindi kutoka Tanzania, Angola, Nigeria, Namibia, Zimbabwe na Afrika Kusini. Mshindi wa kwanza, Cherise Makubale, (Pichani) alitokea nchini Zambia.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG